UMUHIMU WA NDIZI KWA AFYA YAKO

UMUHIMU WA NDIZI KWA AFYA YAKO
UMUHIMU WA NDIZI KWA AFYA YAKO

UMUHIMU WA NDIZI KWA AFYA YAKO : Ndizi imejumuisha aina tatu za sukari ya asili ambazo ni glukosi, sukrosi na fruktosi.

Ndizi hutoa nishati muhimu, ya kudumu na ya kutumika wakati wowote mwilini

Utafiti umethibitisha kwamba ndizi mbili tu zinatosha kuzalisha nishati ya kuufanya mwili ufanye kazi ngumu kwa dakika tisini.

Hakuna shaka ndizi ndiyo kipenzi namba moja kwa wanariadha wanaoongoza duniani.

Ndizi pia yatupatia nguvu ili kulinda afya zetu.

Pia inaweza kutusaidia kukabiliana au kutulinda dhidi ya magonjwa

Sababu sita hizi ndizo zinazofanya ndizi kuwa muhimu katika mchanganyiko wa milo yetu ya kila siku.

MIONGONI MWA FAIDA ZA KULA NDIZI

KULETA FURAHA : Kutokana na utafiti uliowahi kufanyika, watu wenye matatizo au ukosefu wa raha maishani, wamejiona wakirudia furaha waliyokuwa nayo awali baada ya kula ndizi. Hii ni kwa sababu ndizi ina aina ya protini ijulikanayo kitaalam kama tryptophan ambayo mwili wetu huibadilisha na kuwa serotonin, ambayo hukufanya ujisikie mwenye furaha.

VITAMINI B6 iliyopo kwenye ndizi husaidia kurekebisha glukosi iliyopo kwenye damu na hivyo kuboresha hali ya mwili na kukufanya ujisikie vizuri.

ANEMIA: Ndizi pia ina kiasi kingi cha madini ya chuma ambayo husaidia kuchochea uzalishaji wa chembechembe nyekundu za damu, hivyo husaidia mwili kujikinga dhidi ya maradhi mbalimbali, kama anemia. Tafiti za Sehemu mbalimbali zimethibitisha uwezo wa ndizi kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kiafya.

SHINIKIZO LA DAMU: Tunda hili lina kiasi kikubwa cha madini ya potasi na kiasi kidogo cha chumvi na kuifanya kuwa bora katika kudhibiti maradhi ya shinikizo la damu. Hii imethibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.

PITIA
Pilipili Hoho: Umwagiliaji, Mbolea na Uvunaji

UWEZO WA KIAKILI: Ushahidi unaonyesha kwamba takribani wanafunzi 200 huko Marekani walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi wakati wa kufungua kinywa na mlo wa mchana. Hii ina maana kwamba huongeza uwezo wao kiakili. Kichocheo kikubwa cha kupata akili ni madini aina ya potasi yaliyomo.

KUVIMBIWA: Kambakamba za protini zilizomo kwenye ndizi zinasaidia kuzabua tindikali (antiacid). Hivyo kama mtu ana tatizo la kiungulila ajaribu kutumia ndizi ili kupata nafuu. Aidha ndizi husaidia kurejesha hali ya utendaji kazi wa kawaida wa tumboni. Ikiwemo kudhibiti kuvimbiwa bila kutumia kemikali.

KUHARISHA: Kula ndizi mbivu tatu kubwa na huzuia aina nyingi za miharisho na msokoto wa tumbo.

MAUMIVU YA KICHWA: Moja ya njia nyepesi na ya haraka ya kukabiliana na maumivu ya kichwa ni kwa kula ndizi iliyosagwa na kuchanganywa na maziwa. Hii husaidia kusawazisha sukari ya ziada kwenye damu.

Wataalam wamethibitisha kwamba kiafya ndizi ni tunda bora zaidi ya mengine .

Kusaidia mwili kuwa katika hali nzuri wakati wote. Wakati ikifanya hivyo vilevile hurudisha kiwango cha maji kinachohitajika mwilini.

HOMA NA UCHOVU WA ASUBUHI : Ulaji wa mara kwa mara wa ndizi husaidia kuongeza sukari mwilini, hivyo kuondoa hali ya homahoma na uchovu.

KUUMWA NA MBU: Kabla kutumia krimu kusugua sehemu yenye maumivu ya kuumwa na mbu, jaribu kutumia ndizi mbivu. Utashangazwa na matokeo yake.

KUONGEZEKA UZITO: Uchunguzi uliofanya katika Chuo cha Mambo ya Saikolojia nchini Australia, ulibaini kwamba shinikizo la kazi huchochea watu wengi kula vyakula kama chokoleti na mikaango mbalimbali. Ulitafiti kwenye wagonjwa 500 waliolazwa hospitalini, ulionyesha kwamba wengi wana vitambi na kutokana na kazi zenye shinikizo kubwa. Uchunguzi ukahitimisha kwamba watu wajihadhari na vyakula vinavyochochea mifadhaiko ya akili. Hivyo ikapendekezwa kula zaidi vyakula vya wanga. Ambavyo hupunguza kiwango cha sukari mwilini.

PITIA
Kilimo cha Kunde
NDIZI NI MUHIMU KWA AFYA BORA
NDIZI NI MUHIMU KWA AFYA BORA

VIDONDA VYA TUMBO: Ndizi hutumika kama mlo kwa wagonjwa wenye matatizo haya kwa sababu ya ulaini wake. Ndizi mbichi za kupika ndizo zifaazo hapa. Hizi husaidia kupunguza tindikali ya ziada tumboni, pia kusambaa kwenye kuta za tumbo na hupunguza maumivu.

UDHIBITI WA JOTO LA MWILI: Tamaduni nyingi zinakubali kwamba ndizi ni kipoozi cha joto la mwili ambalo husababisha na hali mbalimbali zisizo za kawaida mwilini. Mathalani huko Thailand akina mama waja wazito hutumia ndizi kuhakikisha watoto wanaowazaa wanakuwa katika hali nzuri na ya ubaridi.

UVUTAJI TUMBAKU: Ndizi huwasaidia watu wanaojaribu kuacha kuvuta tumbaku. Vitamini B6 na B12, potassium na maginesiam ipatikanayo kwenye tunda hili husaidia kuondoa athari ya sumu iitwayo nikotini.

UCHOVU: Madini ya potasi yaliyo kwenye ndizi husaidia kutuliza mapigo ya moyo na kuwa ya kawaida. Hupeleka hewa safi kwenye ubongo na kurudisha kiwango cha maji kinachohitajika mwilini. Wakati tukiwa wachovu kiwango cha utendaji kazi wa mifumo mbalimbali ya mwili huongezeka na hivyo hupunguza kiasi cha potasi mwilini, upungufu huu hufidiwa kwa kula ndizi mara kwa mara.

HITIMISHO: Hivyo ndizi ni dawa ya kuponya maradhi mbalimbali. Aidha zina utajiri mkubwa wa protini mara nne zaidi, mara mbili zaidi ya wanga, mara tatu zaidi ya madini ya fasifarasi, mara tano zaidi ya vitamini A na madini ya chuma, ukilinganisha na aina zingine za vyakula. Pengine ni wakati muafaka kuzingatia msemo “kula ndizi kila siku kuepuka kuonana na daktari”.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

MAGONJWA MAARUFU YA SUNGURA

Sungura huwa hawapati magonjwa mengi. Hata hivyo wakiwekwa katika mazingira machafu wanaweza kushambuliwa na magonjwa maarufu yafuatayo: MAGONJWA MAARUFU YA SUNGURA 1.COCCIDIOSIS Hushambulia sana sungura

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »