JINSI YA KUTUNZA BWAWA LA SAMAKI

JINSI YA KUTUNZA BWAWA LA SAMAKI : Mara unapopanda samaki kwenye bwawa, hakikisha unawatunza vizuri. Hakikisha bwawa limejaa maji wakati wote. Pima kiwango cha maji mara kwa mara kwa kutumia miti mirefu. Kama maji yaliyopo bwawani hayatoshi, fungua mifereji ili maji zaidi yaingie.

Hakikisha kwamba kuna chujio upande wa ndani wa kuingizia maji ili kuzuia samaki, takataka na wanyama wengine wadogo toka mtoni kuingia bwawani. Hakikisha pia kuna chujio au wavu upande wa kutolea maji ili kuzuia samaki waliopo bwawani wasitoroke. Bwawa likijaa funga mfereji wa kingizia maji ili lisifurike. Bwawa likifurika utapoteza samaki na vyakula vya asili vilivyopo majini. Ili kuzuia samaki, weka matawi ya miti ndani ya bwawa. Hii itazuia wezi kuvua samaki kwa ndoano au wavu kwa urahisi.

Usiruhusu magugu kuota ndani ya bwawa lako. Kama yakiota yang’oe. Kama magugu kwenye shamba la mahindi yanavyopunguza uzalishaji, ndivyo magugu kwenye bwawa yatakavyopunguza ukuaji na hatimaye mavuno ya samaki.

Fyeka magugu na nyasi juu ya matuta na kuzunguka bwawa ili yasiwe maficho ya maadui wa samaki. Panda majani yanayotambaa kama ukoka maeneo ambayo nyasi za awali zimekufa, ili kuzuia mmomonyoko wa matuta wakati wa mvua. Angalia kama kuna sehemu inayovuja kwenye matuta, ukiona sehemu inayovuja ziba kwa kutumia udongo mzuri wa mfinyazi.

TAI ADUI WA WAFUGAJI WA SAMAKI
TAI ADUI WA WAFUGAJI WA SAMAKI

Unaweza kuzuia maadui wa samaki kwenye bwawa lako kwa njia zifuatazo:

  • Kuchimba bwawa karibu na nyumbani ili kuwa karibu na bwawa mara kwa mara
  • Kuhakikisha kwamba maji yanakuwa na ukijani unaostahili wakati wote.
  • Kuweka matawi ya miti ndani ya bwawa.
  • Kujenga wigo wa miti unaokatisha bwawa.

Baada ya miezi 6 mpaka 8 samaki watakuwa tayari kuvuliwa. Njia nzuri na rahisi ya kuvua samaki, ni kwa kukata tuta upande wenye kina kirefu na kuruhusu maji yatoke taratibu. Maji yakipungua mpaka kufikia nusu ya magoti, unaweza kuvua samaki kwa kutumia ndoo au vipande vya nguo.

PITIA
KILIMO CHA UYOGA

Ni vema ukavua kwa kukausha maji kila baada ya miezi 6 mpaka 8. Kabla ya kufanya hivyo itabidi ufanye matayarisho kadhaa kabla ya kujaza maji kwenye bwawa kama, kuhifadhi vifaranga vya kupanda tena, kutoa tope liliozidi na kung’oa magugu yaliyoota.

Kuvua kwa kukausha maji kuna faida zifuatazo:

  • Una uhakika na idadi ya samaki utakaopanda tena hivyo kupunguza msongamano ambao utasababisha samaki wadumae
  • Unaweza kufanya matengenezo ya bwawa lako.
MUDA WA KUVULIWA SAMAKI
MUDA WA KUVULIWA SAMAKI

Angalia kama kuna nyufa zozote kwenye tuta na kuzirekebisha. Ni muhimu ufyeke au ukate magugu na majani kwenye matuta kuzunguka bwawa.

Tope la ziada ndani ya bwawa na mabaki yaliyooza kwenye sehemu ya kutunzia mbolea yaondolewe na kumwaga shambani kama mbolea.

Kama umekausha maji ya bwawa kwa kukata tuta, ziba kwa kufukia udongo sehemu uliyokata. Acha bwawa likauke kwa angalau wiki moja kabla ya kujaza maji tena.

Hakikisha unashindilia udongo vizuri kuzuia tuta lisivuje.

Ukimaliza kurekebisha bwawa, jaza maji na yarutubishe kwa mbolea ya samadi kama ulivyofanya awali.

Hakikisha maji yamerutubika kwanza kabla ya kupanda vifaranga.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

ZIFAHAMU AINA NNE ZA MTAMA

Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »