Faida za Drip Irrigation (Umwagiliaji wa matone)

Umwagiliaji wa matone ni mfumo wa kisasa kwa umwagiliaji wa mimea na hasa mazao. Maji hupelekwa polepole kwa mabomba au mipira yenye matundu madogo moja kwa moja hadi kwenye shina laa kila mmea, karibu na mizizi yake. Mfumo huu unapunguza sana matumizi ya maji na pia shida nyingine mbalimbali

Faida za umwagiliaji wa matone ni kama zifuatazo:
Matumizi ya maji ni kidogo
Mbolea za chumvichumvi zinaweza kuwekwa kupitia mfumo huu (fertigation), ambapo huchanganywa kwenye tenki la maji kisha kufikishwa karibu na mizizi,
Maji yanapelekwa pale amboko mimea inayahitaji, siyo pale ambako hayaihitajiki
Magugu yanapungua kwa sababu hayamwagiliwi (isipokuwa sehemu iliyo karibu sana na mazao)
Hatari ya magonjwa wa fungus inapungua kwa sababu majani yanabaki makavu
mfumo unahitaji pressure kidogo tu na hii inapunguza gharama za nishati (diseli, umeme) kwa ajili ya pampu hata pampu ni ndogo hivyo rahisi zaidi
Mmomonyoko wa ardhi shambani unapungua sana
Hatari ya kuongezeka kwa chumvi ardhini inapungua sana
Hupunguza gharama za wasaidizi shambani.
Kubwa zaidi njia hii Huokoa muda.

Vitu vinavyotengeneza mfumo huu.
1. Pump… Hii inafanya kazi ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha maji na kupeleka shambani moja kwa moja au kwenye tank au kwenye water reservoir (eneo la kuhifadhi maji).
2. Filters/ chujio… Filter zinachuja maji ili takataka na particles nyingne zisiingie kwenye mfumo wa umwagiliaji na kuleta shida kama za kuziba pipes na emmiters. Emitters ni ni vile visehemu (vitundu) vya kutolea maji kwa ajili ya kumwagilia.
3. Back wash controller/ back flow controller ni vivalve vinavyozuia maji kurudi nyuma ya mfumo hasa pressure inapokuwa ndogo. Maji yanatakiwa yawe na uelekeo mmoja tu (Unidirection). Hizi ni kama valves za mishipa ya vein zinavyozuia damu isirudi nyuma.
4. Pressure regulator au control valve… inafanya kazi ya kucontrol pressure ya maji inayoingia kwenye pipes. ni muhimu sana kuregulate pressure maana ikizidi tu unaweza kukuta sio drip tena ila pipes au tape zimeburst zote.
5. Water tank/ resouvr au chanzo cha maji. Kazi ni kusupply maji kwenye drip, lazima maji yawepo ndio uwe na mfumo wa umwagiliaji.
6. Main line/ pipe ni bomba kubwa linalotoa maji kwenye tank au kwenye source nyingine kwenda shambani kwa ajili ya kusambazwa.
7.Small poly tubes/tapes hizo ndio zile zinasambaza maji shambani na ndio zenye vitobo vya kudodondoshea maji sasa.
8. Kuna source ya power kama umeme au solar kwa ajili ya pump lakin pia unaweza kutumia mafuta tu
Ngoja nielezee kwa kina faida za kutumia mfumo huu wa umwagiliaji.
1. Matumizi mazuri ya maji
Mara nyingi wakulima hawajui kama kumwaga maji hovyo ni tatizo as long as yapo
Sasa drip inapunguza kupotea maji unnecessarily kwa sababu inadondosha maji kwenye mmea tu.
Kwa wenzangu wa kanda ya kati ambao kuna shida ya maji wataelewa kirahisi au kama unatumia ya DAWASCO yenye mita utaelewa zaidi
2. Kwa sababu mfumo huu unamwagia maji kwenye shina la mche tu… unasaidia sana kupunguza shida ya magugu shambani… wakati mmea unapata maji tena ya kutosha magugu yanalala njaa inapunguza usumbufu na gharama za palizi.
Ukimwagia kienyeji kwa sababu unamwaga maji mengi kwa wakati mmoja… yanapotea haraka sana na mengine ndio yanaenda kustawisha magugu
3. Matumizi mazuri ya mbolea… hapa patamu
Kwa mbolea za dukani zinazoyeyuka kwenye maji (water soluble fertilizers), unaziweka kwenye tank zinayeyuka (kutengeneza solution) na halafu zinaenda kwenye mimea kwa kupitia matone yanayotoka kwenye tubes… once again magugu yanalala njaa .
Tofauti na kumwaga shimon alafu unamwaga lita 5 za maji mbolea inayeyuka na kupotelea pembeni magugu nayo yanasherehekea
4. Haki sawa kwa kila mmea.
Mfumo wa umwagiliaji wa matone unatoa kiwango sawa sawa cha maji na mbolea kwa mimea yote shambani. Yani mmea ambao upo karibu na chanzo cha maji unapata kiasi cha maji sawa sawa na mmea ambao upo hukooo mwisho wa shamba, kwa sababu hii basi mazao yanatoka mengi uniform kama matikiti mengi yanakua makubwa na yanayokaribiana sana size.
Tofauti na umwagiliaji wa kawaida ambapo mmea karibu na kisima ndio hupendelewaa halafu ile ya mwishoni au mbali inakonda kwa sababu watu wanachoka sana pia kubeba ndoo nenda rudi.
5. Inapunguza gharama ya nguvukazi na kupunguza changamoto ya nguvu kazi
Watu wengi wanaishi mjini wana mashamba vijiji (bush) au mbali na wanakoishi, wanakua wameweka vijana wa kumwagilia shamba na vijana wanawadanganya sana kuwa wamemwagilia kumbe sio au wamemwagilia kumbe wamerashia tu… hii system kwa sababu ni ya kufungua tu na kufunga bomba hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kuelekezwa kufungua na kufunga bomba. Kama una kijana wa kazi safi angalau kwa sababu hatumii nguvu kubwa sio rahisi kukudanganya.
5. Mfumo wa drip unapunguza trembling/ kukanyaga kanyaga shamba ambapo kunasababisha compaction ya shamba na kupunguza mzunguko wa hewa ardhini.
6. KUONGEZA UZAAJI.
Nimeandika kwa herufi kubwa kabisa.
Drip irrigation bwana inaongeza uzaaji almost 3-4 times normal irrigation… natumia kwenye matikiti maji… kwa kawaida nilipata tani 4 kwa heka na tani 12 kwa drip. Hii inasababishwa na usawa kwenye maji na mbolea.
7. Drip zinapunguza mmomonyoko wa ardhi… tofauti na kumwagilia kienyeji au kwa mitaro
Yan kama unatumia drip na ukaweka matandazo ya plastic (Plastic mulch) umemaliza… no palizi… no energy… high yield.
8. Pia mfumo wa drip ni portable (Unabebaka) ambao unaweza kuutumia hata kwenye shamba la kukodi na kuutoa unaweka kwenye kirikuu mpaka home… kuwe na chanzo kizuri cha maji tu

PITIA
MIGOMBA - KANUNI ZA KILIMO BORA

source http://kilimobiashara.net

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA KOROSHO

Korosho ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae 16 century ndipo lilipo fika africa katika nchi ya msumbiji na baadae likafika nchini Kenya

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »