KICHAA CHA MBWA.

Habari wakulima na wafugaji, 

Kichaa cha mbwa (Rabies) ni ugonjwa unaowapata wanyama wote wanyonyeshao (Mbwa, Paka, Binadamu, Ng’ombe nk)
Ugonjwa huu unasababishwa na kirusi (Rabies Virus)
Virusi hawa wanashambulia mfumo wa fahamu.

USAMBAAJI/UENEAJI WA KICHAA CHA MBWA

img_4463-jpg.1048182

Ugonjwa huu Huenea kwa njia ya mate. 
Mate haya yanakua na Virusi yanaweza kumfikia mnyama mwingine kwa njia ya kuuma au kumtemea mate kwenye maeneo yenye vidonda,machoni, puani, mdomoni. 
Virusi Husafiri toka sehemu waliyoingilia/iliyong’atwa na kwenda mpaka kwenye Ubongo kisha huzaliana na kurudi tena kwenye tezi za Mate (Mdomoni).
Dalili hujitokeza kati ya siku 14- 80 tangu apate Maambukizi. 

DALILI. 

img_4464-jpg.1048206

1. Mabadiliko ya kitabia (kuwa na hasira kali, kula vitu kama karatasi, kinyesi,fimbo, nyaya na mawe /kushambulia watu na wanyama kwa meno, kucha,pembe na kwato bila hata ya kuwachokoza, kuona vitu visivyoonekana(maruweruwe) hataki kusikia kelele)
2. Maumivu na muwasho sehemu iliyoumwa na mnyama hujitokeza (50%) Wanyama wakiwa na hasira kali sana wanaweza kuuma watu na vitu bila ya kughadhibiwa. 

3. Dalili za mfumo wa upumuaji na chakula hujitokeza (kutoka mate mengi mdomoni, kuhema kwa nguvu, kushindwa kula)
4. Maumivu na muwasho sehemu iliyoumwa na mnyama hujitokeza (50%) Wanyama wakiwa na hasira kali sana wanaweza kuuma watu na vitu bila ya kughadhibiwa

5. Dalili za mfumo wa fahamu (Kupooza na kuanguka) Katika hatua hii maambukizi yamesambaa sana kwenye ubongo na virusi wameanza kuharibu. Kupooza huanza kuonekana kuanzia kwenye koo la chakula (kushindwa kumeza) na mashavu. Hali hii husababishwa kutokwa na mate mengi na machozi na kushindwa kufumba Mdomo. Mnyama huwa si mkali na hawezi kuuma.

PITIA
CHAKULA BORA CHA SUNGURA - Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

6. Kuchanganyikiwa na kupata kizunguzungu, kupooza kunakoongezeka, hatua kwa hatua kunakopelekea kifo cha mnyama.

Lakini wanyama wengine wanaweza kufa haraka bila hata ya kuonyesha dalili halisi za ugonjwa.
Kwa kawaida mnyama hufa ndani ya siku saba tangu kuonekana kwa dalili.

UTAMBUZI WA UGONJWA
Si rahisi kutambua ugonjwa huu kwa kutumia dalili. 
Dalili hizi zitasaidia kuhisi kuwa mnyama anaweza kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa. 
Utambuzi kamili unafanyika kwenye
maabara kwa kupeleka kichwa (ubongo) wa mnyama aliyehisiwa kuwa na ugonjwa.

JINSI YA KUKABILIANA/KUDHIBITI
1. Kutoa taarifa ya mnyama anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha umbwa kwa Daktari au Afisa Mifugo aliyeko karibu nawe.
2. Kumfungia mnyama mwenye kuhisiwa kua na ugonjwa wa kichaa cha mbwa ili asiweze kudhuru wanyama na binadamu.
3. Kuzuia wanyama katika eneo lililo na mnyama mwenye ugonjwa kwa kuweka karantini ili ugonjwa usisambae. 
4. Kuchanja mbwa na Paka wote kwa wakati mmoja na kuendelea kuchanja mbwa na Paka wote watakaozaliwa. 
5. Kudhibiti mbwa na Paka wanaotangatanga (mbwa wasitembee ovyo) na kuangamiza mbwa wote ambao hawajachanjwa.
6. Kutoa elimu ya kukabiliana na ugonjwa huu kwa Raia, wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari na Umuhimu wa kutunza Wanyama vyema.

CHANJO.
Chanjo ya kichaa cha Mbwa hutolewa kwa Mbwa na paka kuanzia wiki ya 12 na kisha kuridiwa kila mwaka ama kulingana na Sheria za nchi husika katika namna ya kukabiliana na Ugonjwa huu.

Mambo ya kuzingatia.
1. Usichanje Mbwa au Paka Mwenye kuonyesha dalili zozote za Ugonjwa Wowote.
2. Hakikisha Umepewa cheti cha kudhibitisha Mbwa au Paka wako amepewa chanjo.
3. Kwenye hiko cheti Tarehe ya kuchanja na kurudia chanjo lazima vionyeshwe.
4. Kuwepo na kibandiko (stika) ya Chanjo husika.
5. Muhuri au sahihi na Jina la Mganga/Daktari au Afisa mifugo aliyetoa chanjo hiyo.

PITIA
Ufugaji wa kuku aina kuloirel

img_4465-jpg.1048184

 (Mfano wa cheti cha kudhibitisha Mbwa amechanjwa)

TAMBUA KWAMBA NI TAKWA LA KISHERIA KUCHANJA MBWA NA PAKA DHIDI YA KICHAA CHA MBWA.

TUTAENDELEA SEHEMU YA PILI YA UGONJWA HUU KWA BINADAMU.

NB: Kama Hukumbuki au Hujawapatia chanjo Mbwa au Paka wako basi wasiliana nasi 
Sipy Vet centre, 
Kinyerezi Mbuyuni DSM, 

+255764667503

odhisjamach89@gmail.com

Source Jamii Forums mobile app

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Mpunga Tanzania

MPUNGAHili ni zao la chakula linalolimwa kwa wingi kwenye maeneo ya ukanda wa joto. Zao hili linastawi zaidi kwenye udongo wa tifu tifu na eneo

Read More »

Kilimo cha Karoti

KILIMO CHA KAROTI KILIMO CHA KAROTI : Zao la karoti asili yake ni Asia ya Kati. Zao hili lilienea nchi za Ulaya kwa kupitia Bahari

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »