KILIMO BORA CHA DENGU

UTANGULIZI
Dengu ni nafaka kama zilivyo nafaka zingine, ni zao la jamii ya mikunde pia ni zao la biashara, ni miogoni Mwa zao muhimu sana la biashara ukanda wa ziwa kwa sababu ya thamani yake Kuwa juu sana, zao hili hutumika pia kama zao la chakula kama mbonga , mchaganyo wa wali mseto , makande , kutegeneza Bagia , chiichiri namengineyo mengi.

Kanda ya ziwa hili ndiyo Zao llinalotegenewa zaidi likiogozwa na zao la choroko kwa kuwa na thamani kubwa, hivyo zao hili nizao muhimu kwa uchumi wa wanakanda ya ziwa.

Dengu ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini, vitamini A na B, Madini ya Potassium na chuma.  Zao hili likilimwa vizuri linaweza kutoa mavuno ya kilogram 200 hadi 500 kwa ekari. Zao hili huchukua wastani wa siku 135 kupandwa hadi kuvunwa.

HATUA MUHIMU KATIKA KILIMO CHAKE
Kilimo cha ndegu ni kilimo rahisi sana hakina usubufu sana kama yalivyo mazao mengine hasa ukifata utaratibu wa hatua za mwanzo
Mambo ya kuzingatia

  1. Kuwa makini na hali ya hewa ya mwaka husika kwa kuangalia ukame katika mbuga utaaisha lini pia hali ya mvua ikoje kwa maana kuwa msimu wa kulima huwa mwezi wa tatu mwishoni kwenye maeneo ambayo mbuga huwahi kukauka mapema yaani muda huo ndiyo watu huanza kuandaa shamba kwa kulilima mara ya kwanza kama hatua ya kukiandaa shamba pia hatua hii hufanyika mwenzi nne lakini iwe kwenye kumbukumbu sahihi kuwa ndegu kwa hali ya uzuri kabisa hulimwa mwezi nne na mwanzoni kabisa mwa mwezi wa tano kabla mbuga hazichakauka . 2. Uchaguzi wa Mbengu, mbengu bora za dengu ni muhimu kuzifahamu na kuzitumia katika kilimo hiki  Ziko mbengu ambazo hazihimili magonjwa lakini zipo zinazohimili magonjwa na zinakuwa na uzito hii husaidia katika swala la uuzaji kwa maana ya kuwa mara nyungi dengu kwa sasa huuzwa kwa kilo ili mkulima apate faida zaidi
PITIA
Faida za Drip Irrigation (Umwagiliaji wa matone)

3. Baada ya kulima mara ya kwanza kama kuliandaa shamba unapaswa kulima mara ya pili na kupanda mbengu kwa kufata misitari au kufata tumba au vitalu au misingi itakayokuwa imeadaliwa

4. Hakikisha dengu unapanda katika mbunga isiyo na maji yaliyotuama , unyevunyevu  wa udogo wa shambani ndiyo hitaji muhimu la uoteshaji dengu hairuhusiwi kabisa kupanda dengu kwenye shamba lenye maji.

5. Ardhi inayofaa kwenye kilimo cha dengu ni shamba nyeusi au udongo mweusi ambao hutumika pia katika kilimo cha mpunga, mahidi, choroko na mengineyo .

6. Baada ya dengu kuota hakijisha hakuna maji yaliyotwama katika shamba lako

7. katika ulimaji wa dengu palizi haina ulazima mara nyingi dengu haina palizi kabisa ukizigatia hatua za mwanzo za uandaaji wa shamba

  1.  Dengu hutumia miezi mitatu mpaka kuvuna hivyo inajulazimu kusubiri ikauke mpaka hali ujano itokee kwenye mmea, mavuno ya dengu mara zato hufanyika kwa kung’oa mmea wote na kukusanya sample dogodogo ili kumaliza mapema mavuno yake baada ya hatua hiyo unaleta mkokoteni shambani unajusanya kwa mkokoteni nakupeleka sehemu kavu iliyosafi kwa ajili ya kutoa maganda ya zao la dengu,hatua ya kutoa maganda ya dengu inaweza fanyika kwa kienyeji kwa kupiga na miti au ikatumika kwa kitaalamu kwa kupiga na Tractor yaan tractor inapita kwa mzuguko kwenye navuno ya  dengu yaliyosambazwa mpaka kuputua maganda ya juu ya dengu na kubaki dengu yenyewe tayari kwa biashara au kukoborewa tena kwa chakula.

9. Uhifadhi wa zao la dengu hauna chagamoto sana japo hushambuliwa na wadudu baada ya miezi mitatu bila kuweka dawa unapaswa kuhifadhi kwenye eneo la wazi yaan kama ni chumba kiwe na uwazi wa hewa ya kutosha  lakini pia kunagunia special nitazieleza kwenye utatuzi wa chagamoto.

CHAGAMOTO KATIKA KILIMO CHA DENGU
Zipo chagamoto kadhaa katika kilimo cha dengu kama ifatavyo
1. Wakati wa kupanda huwa kunachagamoto ya mvua ambazo hujitokeza na kuharibu zao la dengu kwa kisukuma tunaita SHIBOJA yaani mvua za kuozesha dengu chagamoto hiyo ikijitokeza subiri maji yakauke katia mbengu upya kama zao limeathiriwa kidogo kama limeathiriwa sana unarudia shamba lote.

PITIA
UMUHIMU MKUBWA WA KOMAMANGA (POMEGRANATE) JUU YA MARADHI YA KANSA

2 Chagamoto ya Funza baada ya mmea kutoa maua . mmea ukitoa maua funza hushambulia kwa kasi kama eneo hilo liko na funza   tiba ya funza hao nikupulizia dawa unaenda duka la kilimo watakupatia.

3 chagamoto ya wadudu wakati wakati mmea unatoa zao lenyewe Wakati huu pia unapulizizia dawa kama wakijitokeza Jambo la funza na wadudu hujitokeza mara chache sana hivyo ni vyema kuwa na.tahadhali hiyo.

4 Chagamoto ya panya   Panya hujitokeza kwenye shamba wakati zao Linaanza kukomaa wao hutafuna dengu kamili hivyo unaweza jikuta unapata hasara wakati dengu zilisitawi vyema
Utatuzi wa chagamoto hiyo ni kuwatega panya kwa sumu kwa ukanda wa mkoa wa shinyanga serikali hutoa dawa nasi huchaganya na mahidi nakusambaza pembezoni mwa shamba maana panya hutokea kwenye nyasi hivyo watakutana na mahidi nakuyala.

Chagamoto nyingine ni za masika unaweza lima mwishoni sana kwenye mavuno ukakutana na mvua.

5 Chagamoto ya uhifadh Hapo kunachagamoto ya kushambuliwa na wadudu ndani ya miezi mitatu ya mwanzo unashauriwa kuhifadhi kwenye magunia nasiyo mifuko ya plastic.

Unashauriwa kutia dawa inaitwa AKTERIA mapema kabisa unapohifadhi kama unahifadhi kwa muda mrefu baada ya miezi mitatu unatia tena Au unaweza hifadhi kwaifuko maalumu ambayo imetiwa dawa kabisa na dani inajuwa kama mfuko wa sukari na upaswa kuifuga kitaalamu kama maeelekezo yalivyo .

Chagamoto nyingine ni ya soko naieleza hapa chini na utatuzi wake

HALI YA HEWA NA UDONGO
Ni zao linalohitaji hali ya hewa ya kibaridi kiasi kwani joto kali na ukame sana huathiri mavuno yake, hupunguza wingi wa mavuno. Ni zao linalostahimili ukame, linaweza kukua katika hali ya hewa ya unyevunyevu tu.

Kama utakuwa unamwagilia basi epusha unyevu mwingi ikifikia kipindi cha maua hadi kuvuna. Zao hili linaweza kulimwa katika udongo wa aina tofauti tofauti wenye Ph 6-8. Udongo wenye asidi na base kidogo.

PITIA
Kilimo Bora Cha Alizeti

Kwa Tanzania zao hili linaweza kulimwa katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Mwanza, Singida, Morogoro, Shinyanga N.K. Lakini kwa sasa mikoa ya Shinyanga na Mwanza ndio wazalishaji wakubwa wa Dengu.

UPANDAJI NA NAFASI
Zao hili huitaji mbegu kiasi cha kilogram 15 hadi 40 kutegemea ukubwa wa mbegu husika. Zao hili hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua,unaweza kupanda baada ya kuvuna mazao mengine uliyopanda mapema.

Mbegu za dengu hufukiwa katika kina cha sentimeta 5 hadi 6 ili kufanya mazingira rafiki kwa bacteria wa rhizobia kufanya kazi. Zao hili usipande pamoja na vitunguu na tangawizi. Panda kwa kutumia drilling method-njia ya vifereji kwa nafasi ya mistari miwili ya sentimeta 15 na sentimeta 30 hadi 50 kwa mstari hadi mstari.

MBOLEA ZA VIWANDANI NA SAMADI
Mbegu unaweza kuzipanda baada ya kuziongeza inoculam kundi F na Pia Mbolea ya DAP kilogram 25 hadi 50 kwa ekari katika shamba lisilo na rutuba ya kutosha.

PALIZI-Palilia mapema shamba lako.

WADUDU WAHARIBIFU KWA DENGU
Dengu hushambuliwa na Mchwa wakubwa weusi, aphid wa njegere, funza wa vitumba, Inzi wa lucina n.k. wazuie wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu uonapo dalili za mashambulizi ya wadudu.

MAGONJWA YA DENGU
Dengu hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu ambayo. Hivyo kama eneo lako hushambuliwa na ukungu mara kwa mara basi puliza dawa za ukungu (FUNGICIDES)

UVUNAJI WA DENGU
Zinavunwa mara tuu pindi vitumba vya chini vibadilikapo rangi kuwa kahawia angavu na vitumba vikiguswa hutoa sauti Mavuno ya dengu kwa heka yanaweza kuwa gunia 6,5,4 Inategemeana na eneo ulilolima linarutuba kiasi ngani na umefata taratibu zote.

Soko la dengu ni la uhakika sana kwa maana ya uhitaji wa dengu katika soko la ndani na nje
Dengu ndiyo zao ambalo mkulima wa mkoa wa shinyanga na niko jirani hulitegemea kwa kipato cha juu.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO CHA VITUNGUU SWAUMU – garlic

[vc_row][vc_column][vc_column_text]   Udongo Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si

Read More »

CORONA VIRUS EDUCATIONAL POST

Naomba twende polepole Vyanzo vya vifo duniani na idadi (WHO, 2019) Heart diseases – mil 9.43Stroke – mil 5.73COPD – mil 3.04Pumu – mil 2.96Alzheimer’s

Read More »

MAGONJWA MAARUFU YA SUNGURA

Sungura huwa hawapati magonjwa mengi. Hata hivyo wakiwekwa katika mazingira machafu wanaweza kushambuliwa na magonjwa maarufu yafuatayo: MAGONJWA MAARUFU YA SUNGURA 1.COCCIDIOSIS Hushambulia sana sungura

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »