JINSI YA KUTAYARISHA MBOLEA ASILIA MASHAMBANI

JINSI YA KUTAYARISHA MBOLEA ASILIA MASHAMBANI : Mbolea asilia ni aina ya mbolea itokanayo na masalia ya mimea kama majani, mabua na takataka za jikoni. Masalia haya hukusanywa, kuchanganywa na kuachwa kwa kipindi fulani ili yaoze.

JINSI YA KUTAYARISHA MBOLEA ASILIA MASHAMBANI
JINSI YA KUTAYARISHA MBOLEA ASILIA MASHAMBANI

Japokuwa kitaalamu mbolea hii haina virutubisho vingi kama mbolea za viwandani bado bado ina faida kubwa ya kuboresha hali ya udongo kama vile:

• Kuboresha muundo wa udongo kwa kuruhusu chembechembe za udongo kushikamana,

• Husaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo;

• Kupunguza joto la udongo; na,

• Kuweza kuhifadhi kiasi kikubwa cha unyevunyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu.

Mbolea asilia hujenga msingi bora wa matumizi ya mbolea za viwandani ambazo kwa pamoja hutoa mazingira bora kwa mimea kukua na kustawi vizuri.

UTAYARISHAJI WA MBOLEA ASILIA:

Mkulima anapoamua kutengeneza mboji ni muhimu kukumbuka yafuatayo:

• Inabidi atayarishe shimo lenye urefu wa futi 26 (mita 8.5) na upana wa futi mbili (mita 0.6) Ili kuruhusu hewa iweze kupenya au kuzunguka kwa urahisi

Kuna njia kuu mbili za kutengeneza mboji nazo ni:

• Kupanga takataka (masalia) juu ya ardhi

• Kuchimba na kupanga takataka shimoni na kuacha zioze

Njia zote mbili zinafaa na utengenezaji wake unategemea mahali na upatikanaji wa maji. Mathalani sehemu ambapo kuna shida ya maji njia hii ya shimo inasemekana kuwa ni bora sana kwa ajili ya usafi wa mazingira na uzuiaji wa magonjwa mbalimbali kama vile kipindupindu, kuhara damu nakadhalika.

JINSI YA KUPANGA TAKATAKA NDANI YA SHIMO:

• Tandika mabua au manyasi ndani ya shimo kwa kina cha sentimita kumi na tano.

• Ongeza nyasi mbichi hasa zile zenye majimaji na aina yeyote ya masalia na matakataka ya jikoni, sentimita 10 kisha ongeza udongo kama sentimita mbili.

PITIA
UBUYU TUNDA LENYE FAIDA KUBWA MWILINI

• Baada ya kufanya hivyo unatakiwa uweke maji mengi na utakuwa umemaliza tabaka moja. Unatakiwa uendelee kuongeza tabaka lingine kwa mzunguko huo mpaka shimo lako lijae au kuwe na kina cha mita moja na nusu.

• Ukishamaliza au kujaza shimo lako ongeza maji juu na kama kuna uhaba wa maji tandaza mimea ambayo ina maji au utomvu kwa wingi. Kwa usalama funika mkusanyiko huu kwa majani ya aina yeyote na chomeka miti mibichi katikati ya mboji hii

• Baada ya siku tatu, chomoa na ushike kama una moto sana, ongeza maji na kama ni wa baridi mboji yako imeshaharibika, hivyo inabidi upangue na kupanga upya.

• Kama muozo unaendelea sawasawa baada ya wiki mbili unatakiwa ugeuze mbolea yako(Tazama mchoro)

UTAYARISHAJI WA MBOLEA ASILI
UTAYARISHAJI WA MBOLEA ASILI

• Kuiva kwa mbolea hii kunategemea aina ya takataka ulizotumia, hali ya unyevunyevu na mzunguko wa hewa kwenye mkusanyiko huo. Unatakiwa uzigeuze mara mbili takataka za juu nazo ili zipate nafasi ya kukauka.

• Iwapo utafuata taratibu zote hizi, mboji yako itachukua muda wa miezi tangu siku ya kwanza kufunikwa. Hii ina maana kwamba mkulima anashauriwa kutayarisha mbolea yake miezi mitatu kabla ya msimu.

Mbolea ambayo tayari imeiva huwa na dalili zifuatazo:

• Haina harufu kabisa,

• Huwezi kitambua kabisa zile takataka za mwanzoni, na

• Mboji huwa na rangi nyeusi hadi kahawia na uwingi wake hupungua sana ukilinganisha na mwanzoni.

MBOLEA ASILI IKIWA TAYARI KWA MATUMIZI
MBOLEA ASILI IKIWA TAYARI KWA MATUMIZI

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kahawa Inayoleta Utajiri

KAHAWA, ni zao kubwa la biashara, inachukua nafasi ya pili kwa  kuingizia taifa fedha nyingi za kigeni baada ya zao la Tumbaku, wakulima wengi wanaofuata

Read More »

KILIMO BORA CHA ULEZI

Ulezi ni punje ya mlezi au mwele (aina ya nafaka) ambao hulimwa katika sehemu zenye hali ya ukame. Ulezi ni zao la asili, shirika la

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »