AINA ZA MAGUGU NA MADAWA YA UDHIBITI

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

AINA ZA MAGUGU NA MADAWA YA UDHIBITI : Moja ya changamoto kubwa za uzalishaji wa mazao, upambaji wa maeneo ya wazi na kilimo cha bustani ni kudhibiti magugu. Magugu pamoja na kushindania maji mwanga na virutubisho vya ardhini lakini pia huifadhi wadudu waharibifu wa mazao na wadudu wanaobeba magonjwa ya mimea kama vile aphids.

Tafsiri fupi ya magugu ni “mimea iliyoota sehemu isiyo stahili.” Ukifikiria kwa tafsiri hii nyasi ni magugu katika shamba la Karanga lakini pia mimea ya karanga ni magugu katika bustani ya nyasi.

AINA ZA MAGUGU NA MADAWA YA UDHIBITI
AINA ZA MAGUGU NA MADAWA YA UDHIBITI

AINA ZA MAGUGU KULINGANA NA MZUNGUKO WA MAISHA

MAGUGU YA MSIMU:

Ni magugu ambayo yanakamilisha mzunguko wake wa maisha (kuota mpaka kufa) ndani ya msimu mmoja wa kuzalisha mazao, mifano ya dhahiri ya magugu haya itakua ni magugu aina ya nyasi, na baadhi ya magugu ya majani mapana. etc

MAGUGU YA MUDA MREFU:

Ni magugu ambayo hukamilisha mzunguko wa maisha kwa zaidi miaka kadhaa hivyo misimu kadaa ya uzalishaji mazao hupita kabla magugu kufa. Magugu ya aina hii kwa kiasi kikubwa huwa ni ya majani mapana. Mfano mzuri wa magugu haya ni magugu ya majani mapana yaliyo mengi mfano mimea ya jamii ya mchicha.

AINA ZA MAGUGU KULINGANA NA AINA ZA MAJANI

MAGUGU YA MAJANI MAPANA:

Kama jina lake linavyo jieleza magugu haya huwa na majani mapana ambayo hutokana na aina yake ya mbegu ambayo huwa daikotiledoni yaani huwa na pande mbili mfano ni magugu aina ya mchicha au striga.

MAGUGU YA MAJANI MEMBAMBA:

Ni aina ya mimea itokanayo na mbegu zenye pande moja ambayo huwa na majani membamba mfano mzuri wa mimea hii ni majani aina ya nyasi yote.

PITIA
KUFUGA KUKU WA KIENYEJI KUNALIPA

Aina zote hizi za magugu zina njia mbili za udhibiti ikiwamo ya matumizi ya nguvu za mkono au mashine kuyang’oa au matumizi ya kemikali za kuangamiza magugu (Viuagugu; Herbicides)

MATUMIZI YA KEMIKALI KWA UDHIBITI WA MAGUGU

Makala nyingi zimeandikwa na mengi yamesemwa kuhusu madhara ya kemikali kwa mazingira yetu, lakini kuna kitu kimoja ni cha muhimu na kutiliwa mkazo katika matumizi ya kemikali za aina zote duniani, ambacho hudharauliwa na watumizi wa kemikali nchini; “SOMA KIBANDIKO KABLA YA KUTUMIA.” Kwani matumizi ya kemikali kuangamiza magugu bado ni njia muhimu ya kupambana na tatizo hili, na kuongeza uzalishaji wa mazao.

Vibandiko vya mdawa haya huwa na maelezo mengi ya maana na ya muhimu katika matumizi ya kemikali hizi, hivyo ni jambo la msingi kuzingatia maelezo yaliyomo katika vibandiko hivi. Kwa ufupi nitataja baadhi ya mazingatio ya ujumla katika matumizi ya viua magugu;

o Soma kibandiko kabla ya kutumia Kemikali ya aina yeyote.

o Weka Madawa mbali na watoto

o Usitumie kinyunyizi kimoja kwa viangamiza magugu na viua wadudu, andika moja wapo MAGUGU.

o Tumia Nozle ya pressure ndogo ili kuepuka k u n y u n y i z i a kemikali za viua magugu kwenye mimea husika.

o N y u n y i z a kemikali za kuua magugu wakati wa utulivu usiokua na upepo wala mvua japo kwa masaa 24 yajayo isipokuwa kama kiuagugu husika kinahitaji kunyunyiziwa maji baada wa kutumika (Watering-in).

o Vaa mavazi maalumu ya kunyunyizia kemikali yanayo funika macho, ngozi, mikono na miguu ikiwezekana tumia kichuja hewa kilicho thibitishwa.

o Osha mara tatu au zaidi vyombo vya madawa na bomba ya kunyunyizia Madawa (Sprayer) kabla ya kuhifadhi au kutupa kwa utaratibu maalumu, usitumie kwa matumizi mengine yeyote.

PITIA
Zao la Muhogo Laongeza Ufaulu kwa Wanafunzi Handeni

AINA ZA VIUAGUGU KULINGANA NA AINA ZA MAGUGU

VIUAGUGU VINAVYOCHAGUA AINA ZA MAGUGU:

Hivi ni viua magugu ambavyo huua aina moja wapo ya magugu pekee, kama vile ya majani mapana peke yake mfano Farmbase 2-4 D Amine, viuagugu hivi vinaweza kutumika kuua magugu katika shamba au eneo lenye mimea ya majani membamba inayo takiwa kubaki peke yake. Matumizi ya viua gugu hivi huweza kukamilisha lengo hili bila kusabisha madhara kwa mimea husika. Lakini maelezo ya vipimo vya dawa vinatakiwa kuzingatiwa kwani kuzidi kwa kipimo kunaweza kusababisha matokeo yasiyo tegemewa.

VIUAGUGU VISIVYOCHAGUA AINA ZA MAGUGU:

Hivi ni viuagugu ambavyo vinauwezo wa kuua kila aina ya mmea bila kuchagua, mfano wa Madawa haya ni ALLROUND na GUGUZOT. Mara nyingi viua gugu hivi hutumika katika maeneo ambayo hayana mazao bado au katika maeneo ya kando ya barabara, reli na chini ya nguzo za umeme. Matumizi ya Madawa haya yanatakiwa kuzingatia vipimo vilivyo pendekezwa kulingana na aina za mimea iliyopo eneo husika ili kuepuka matokeo yasiyo tarajiwa.

AINA ZA VIUAGUGU KULINGANA NA KIPINDI CHA KUTUMIKA:

PRE-ERMERGENT (VIUAGUGU VYA KABLA YA MIMEA KUOTA):

Hivi ni viuagugu ambavyo huangamiza magugu yakiwa bado mbegu au kabla hayajachomoza juu ya udongo. Baadhi huua ya kemikali hizi huangamiza magugu kwa kuua mizizi michanga mara tu inapotoka kwenye mgegu.

POST-EMERGENT (VIUAGUGU VYA BAADA YA MIMEA KUOTA):

Hivi ni viuagugu mabavyo huangamiza magugu ambayo tayari yameshaota. Kwa kiasi kikubwa aina nyingi za Madawa ya kuua magugu yapatikanayo nchini ni aina hii. Mfano wa Madawa madhubuti ya aina hii ni ALLROUND,
GUGUZOT na FARMBASE 2,4- D kutoka kwa wasambazaji wa Madawa ya mifugo na mazao kama FARMBASE Ltd.

PITIA
UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA [ BROILER ]

Viuagugu vya aina ya post-emergent mfano ALLROUND, FARMBASE 2,4 – D na vinginevyo, vitafanya kazi kwa ufanisi mkubwa iwapo vitatumika kipindi cha ukuaji wa magugu “active growth” (sio kipindi cha ukame mkubwa au kipindi
ambacho mmea umesimamisha ukuaji). Madawa haya mengi huwa ni systemic hivyo usafirishwaji wa kutoka kwenye majani hadi kwenye mizizi na kinyume huwa rahisi sana wakati wa ukuaji wa haraka wa mmea.

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo