KILIMO CHA BAMIA

 BAMIA
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines.

Urefu wa mmea huwa kati ya meta moja na mbili. Matunda yake hufikia urefu wa sentimeta 10 hadi 20, na huchumwa kabla hayajakomaa sana na hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Majani yake huchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za majani.

Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

Ustawishaji: Zao hili hustawi katika mete 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

Kupanda: Kwa kawaida mbega za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).

Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.

Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini. Mimea ifikiapo urefu wa nusu meta hivi wakulima wengine huondo ncha zake kwa kuamini kwamba wingi na ubora wa matunda huongezeka. Bamia huwa tayari kuchumwa baada ya miezi 2 tangu kupandwa na huendelea kwa muda mrefu.

PITIA
Fahamu Gharama Katika Kilimo cha Nyanya

Magonjwa: Mosaic Virus- Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA MPUNGA

Mpunga ni zao ambalo hupendwa na watu wengi sana hususani katika bara la Afrika na ni zao la pili kwa uzalishwa kwa wingi sana. Kilimo

Read More »

KILIMO BORA CHA UFUTA

Ufuta (sesamum indicum)ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »