BANDA BORA LA SUNGURA – Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Ufugaji wa sungura unaweza kufanywa mahali popote. Wafugaji wengi wanatumia mabanda, maeneo ya nyuma ya nyumba au kwenye maghala yasiyotumika kama mahali sahihi pa kuweka vizimba vya sungura.

Kumbuka: vizimba hivi ni sawa na vile vinavyotumiwa katika ufugaji wa kuku ingawa hivi vya sungura vinakuwa vipana na kimo kikubwa. Unaweza kujenga banda kubwa la kawaida kwa kutumia miti inayopatikana kwenye eneo lako, mabanzi au mbao, ambazo pia zinapatikana.

Ikiwezekana, unaweza kujenga ukuta wa matofali na kuacha madirisha na kuziba kwa nyavu nene pamoja na nyavu ndogo (kama za mbu) ili kuzuia wadudu wasiingie. Kumbuka kwamba, sungura wanahitaji kupata hewa ya kutosha, lakini pia wanapenda sehemu zenye kiza kidogo. Banda hilo lazima liezekwe vizuri ili lisivuje hasa nyakati za masika.

Ukubwa wa banda ambalo unaweza kulitumia kuweka vizimba vya sungura linategemea na idadi ya sungura unaotaka kuwafuga. Wale wa kuanzia hawana shida, lakini nazungumza kuhusu malengo ya mradi wako.

Sungura husimama kwa miguu yao ya nyuma ili kuangalia kama mazingira yao ni salama, na kizimba chako lazima kiwe na urefu unaomruhusu kusimama bila kujigonga kichwani ama masikio yake kugusa juu ya dari.

Kimo cha futi 2′ (60sm) mara nyingi kinafaa kwa sungura wa ukubwa wa kati lakini aina kubwa za sungura zinahitaji kimo cha futi 3′ (90sm).

NB: Mabanda mengi ya sungu mara nyingi watu hawaruhusiwi kuingia ovyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuepuka kuleta magonjwa ndani. Kama utatembelea kwa mfugaji akakwambia huruhusiwi kuingia bandani, tafadhali heshimu uamuzi wake.

Kama mfugaji atakataza kuingia ndani, tafadhali muombe walau akuruhusu uingie na kuangalia sungura walivyo unaotaka kuwanunua na namna ya kuwahudumia. Tafadhali usinunue ikiwa hawatakuruhusu kabisa kuingia ndani.

Kama mnunuzi, unapaswa kuwa na haki ya kuona kile unachotaka kukinunua. Unapaswa kuruhusiwa kuona miondombinu na mazingira ambayo sungura hao wanaishi. Hiyo itakuwa elimu tosha pia kwako kuweza kumudu kuwatunza.

PITIA
Umuhimu wa kitunguu swaumu katika kutibu magonjwa ya kuku

Unaponunua sungura unaotaka kuwafuga, tafadhali angalia walio na afya njema. Hakikisha sungura hao wamechangamka; wakiwa na macho maangavu. Hakikisha wana manyoya laini na safi; Hakikisha hakuna machozi au unyevunyevu wowote kwenye macho yao, pua au midomo. Pia, hakikisha kwamba mfugaji huyo anazo taarifa muhimu pamoja na rekodi za sungura wake.

Ninashauri kwamba yeyote anayetaka kuingia kwenye ufugaji wa sungura kwa mara ya kwanza afanye hivyo taratibu kwa kuanza kidogo kidogo. Unaweza kupanua ufugaji wako baadaye utakapoona inafaa.

Unaweza kujenga banda lenye upana wa futi 16 na urefu wa futi 24. Kimo cha paa la katikati ni lazima kiwe futi 12 kuanzia kwenye sakafu na pembeni ni lazima liwe na kimo cha futi 8.

Gharama za ujenzi wa banda la aina hiyo zitategemea na rasilimali ulizotumia kujengea. Kama unafuga kibiashara, weka sakafu nzuri kwa sababu utatumia njia bora za kukinga mkojo ambao ni mali. Lakini kama hutaki kukinga mkojo, basi usisakafie ili mkojo ukidondoka uweze kuzama ardhini na inakusaidia katika kusafisha na kuondoa harufu. Sakafu imara ya kawaida inakupasa usafishe kila wakati, hasa kama hukutumia njia bora za kukinga mkojo.

Lakini nakushauri, kinga mkojo kwa sababu ni mali. Utapata fedha nyingi bila kutegemea. Kama hutaki kutumia vizimba, kamwe usiwaweke sungura wako kwenye sakafu ya udongo, kwa sababu sungura wana kawaida ya kuchimba na unaweza kukuta wametoboa ardhi na kutoka nje.

Sakafu ya udongo itakufanya upate shida pia wakati sungura wanapozaa, kwani wanaweza kuzalia kwenye mashimo. Hivyo basi, kama utawafuga bila kutumia vizimba, weka sakafu na uweke matandazo sakafuni.

VIZIMBA
Vizimba (hutches au cages) lazima vitengenezwe kabla ya kuwaingiza sungura wako wa kwanza. Sungura mmoja anapaswa kuwa na nafasi ya upana wa futi mbili, urefu wa futi tatu na kimo cha futi tatu – pamoja na eneo la kutosha la kuchezea.

PITIA
MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI WA MIFUGO

Unaweza kujenga vizimba vikubwa kuwezesha kuweka sungura wengi ambao unapanga kuwalisha tu kwa ajili ya kuwauza kwa nyama. Kwa kadiri kizimba hicho kitakavyokuwa, ni vyema kukiinua kutoka usawa wa ardhi ili kukusaidia kuondoa takataka unapofanya usafi.

Eneo la kuishi – wastani wa 12 sq. ft (6 x 2) ambalo linaweza kuwa na sungura wadogo na wa maumbile ya kati wanne. ikiwa sungura wako ni wa aina ya wale wakubwa, basi unatakiwa kuongeza ukubwa wa banda.

Eneo la kuishi la sungura wako kwenye kizimba ni lazima lihusishe eneo la kulala, eneo la kudondoshea kinyesi na vifaa vya chakula na maji na nafasi ya kutosha ya kuweza kucheza. Ni vyema sungura wako wakawa na eneo la kutosha kujinyoosha katika kila upande. Eneo la kuishi la sungura wako likiwa dogo litaathiri afya yake – na kumsababishia matatizo ya uti wa mgongo, kupoteza nyama na utapiamlo.

Sungura aliye huru lazima atajinyoosha anapokuwa amepumzika, hivyo kizimba chako kinatakiwa kiwe kipana kuwezesha sungura alale huku akiwa amenyoosha miguu yake yote. Hii inatoa nafasi ya kutosha kuweza kujigeuza.

Wastani wa upana unatakiwa kuwa futi 2 (60sm) kwa sungura wadogo na wa kati na futi 3 (90sm) kwa sungura wakubwa kama wa aina ya Flemish Giants.

KIMO CHA KIZIMBA
Sungura husimama kwa miguu yao ya nyuma ili kuangalia kama mazingira yao ni salama, na kizimba chako lazima kiwe na urefu unaomruhusu kusimama bila kujigonga kichwani ama masikio yake kugusa juu ya dari. Kimo cha futi 2′ (60sm) mara nyingi kinafaa kwa sungura wa ukubwa wa kati lakini aina kubwa za sungura zinahitaji kimo cha futi 3′ (90sm).

NB: Mabanda mengi ya sungu mara nyingi watu hawaruhusiwi kuingia ovyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuepuka kuleta magonjwa ndani. Kama utatembelea kwa mfugaji akakwambia huruhusiwi kuingia bandani, tafadhali heshimu uamuzi wake.

PITIA
AINA MBALIMBALI ZA SUNGURA (RABBIT BREEDS)

Kama mfugaji atakataza kuingia ndani, tafadhali muombe walau akuruhusu uingie na kuangalia sungura walivyo unaotaka kuwanunua na namna ya kuwahudumia. Tafadhali usinunue ikiwa hawatakuruhusu kabisa kuingia ndani.

Kama mnunuzi, unapaswa kuwa na haki ya kuona kile unachotaka kukinunua. Unapaswa kuruhusiwa kuona miondombinu na mazingira ambayo sungura hao wanaishi. Hiyo itakuwa elimu tosha pia kwako kuweza kumudu kuwatunza.

Unaponunua sungura unaotaka kuwafuga, tafadhali angalia walio na afya njema. Hakikisha sungura hao wamechangamka; wakiwa na macho maangavu. Hakikisha wana manyoya laini na safi;

Hakikisha hakuna machozi au unyevunyevu wowote kwenye macho yao, pua au midomo. Pia, hakikisha kwamba mfugaji huyo anazo taarifa muhimu pamoja na rekodi za sungura wake.

Ninashauri kwamba yeyote anayetaka kuingia kwenye ufugaji wa sungura kwa mara ya kwanza afanye hivyo taratibu kwa kuanza kidogo kidogo. Unaweza kupanua ufugaji wako baadaye utakapoona inafaa.

MUHIMU

UFUGAJI WA NDANI
1 – Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha.

2 – Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa.

3 – Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri.

4 – Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi

5 – Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki.

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo