BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE – Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi


BANDA BORA.
Band alijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-

  1. Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi.
  2. Kuta imara zenye matunda au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha,
  3. Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.
  4. Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.
  5. Paa lisilovuja na

NG’OMBE ANAHITAJI  BANDA ZURI AMBALO LITAKUA:

  • Na sehemu ya kulala yenye paa kumlinda ng’ombe wako kutokana na mvua au jua.
  • Likisafishwe kila asubuhi.
  • Linapigwa dawa kila siku 7 kutumia Kupacide kutoka Coopers au Ultraxide kutoka Ultravetis.
  • Kavu. Tengeza sakavu iwe na mwinuko kidogo kutoa samadi na maji. Ng’ombe kwenye banda lenye unyevu watapata homa ya mapafu, kuoza miguu na ugonjwa wa chuchu/kiwele.
  • Kuwa huru kutokana na kupe,viroboto,chawa na mchwa.
  • Na sehemu ya malisho makavu, kinyeo cha maji na sehemu ya madini, ambavyo ni futi 3 kutoka kwenye ardhi. Weka maji safi kwenye sehemu ya maji kila siku.

Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa  kuzingatia yafuatayo:-

  1. Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama.
  2. Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na wanyama hatari.
  3. Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.
  4. Zizi lifanyiwe usafi  mara kwa mara na
  5. Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na maji ya kunywa.UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA NG’OMBE WA MAZIWA KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI

UTUNZAJI WA NDAMA
Mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa.  Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na

  1. Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tincute of Iodine) mara baada ya kuzaliwa na
  2. Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.  Aidha, aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:-
  • Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
  • Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
  • Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oili).
  • Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na
  • Yai moja bichi
PITIA
UCHANGANYAJI WA VYAKULA VYA MIFUGO

Koroga mchanganyiko huo, weka katika chupa safi na ndama anyweshwe kabla haujaopoa.  Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 3 mfululizo na kila mara mchanganyiko uwe mpya.  Wakati wa kunywesha chupa iwekwe juu  kidogo ili asipaliwe.

Endapo ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe maziwa kwa njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa  Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1, Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa na, Ndama aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3.  Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya nzuri.

JEDWALI NA. 1  KIASI CHA MAZIWA NA CHAKULA MAALUMU KWA NDAMA

UMRI (WIKI) KIASI CHA MAZIWA KWA SIKU (LITA) KIASI CHA CHAKULA MAALUM CHA NDAMA KWA SIKU (KILO)
1 3.0 0.0
2 3.5 0.0
3 4.0 0.0
4 4.5 0.0
5 5.0 0.1
6 5.0 0.2
7 5.0 0.3
8 4.0 0.4
9 3.0 0.7
10 2.0 1.0
11 1.5 1.25
12 – 16 0.75 1.5

Vyombo vinavyotumika kulishia ndama visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.

MATUNZO MENGINE YA NDANI NI PAMOJA NA:-

  1. Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,
  2. Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike
  • Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa ajili kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika kwa ajili ya kuendelea kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
  1. Kuweka alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa udhiti wa umiliki na utunzaji kumkukumbu na,
  2. Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.
PITIA
MBINU ZA KUZINGATIA KATIKA UANDAAJI WA CHAKULA KWA KUKU WAKO

Huduma hizi zifanyike chini ya maelekezo ya mtaalam wa mifugo. Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula mchanganyiko kuanzia kilo 2 4 kwa siku kutegemea umri wake na Ndama wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi.

UTUNZAJI WA MTAMBA
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya kwanza.  Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la ng’ombe.  Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe:-

  • Malisho bora
  • Maji ya kutosha
  • Madini  mchanganyiko na
  • Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.

UTUNZAJI WA NG’OMBE WAKUBWA
Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume.  Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la kumpatia malisho bora na maji safi ya kutosha kila siku.  Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ng’ombe wakubwa ni pamoja na:-

Ng’ombe apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10 au majani mabichi kilo 40 kwa siku kutegemeana na uzito.  Iwapo malisho hayatoshi hususan wakati wa kiangazi apewe masalia ya mazao (viwandani na mashambani) kama molasisi, mabua, maharage, mpunga n.k

Ng’ombe apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini mchanganyiko, unga wa mifupa na chokaa) kulingana na hatua na kiwango cha uzalishaji na,Ng’ombe apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

UCHAGUZI WA UTUNZAJI WA DUME BORA LA MBEGU
Dume ndilo linalojenga ubora wa kundi  la ng’ombe katika masuala ya uzalishaji kutokana na uwezo wake wa kupanda majike 20 – 25 wakati wa msimu wa uzalianaji (breeding season). Ili kundi la ng’ombe liwe bora, mambo yafuatayo yazingatiwe

  • Chagua dume kutoka kwenye ukoo ulio bora kwa kuzingatia kumbukubu za uzalishaji wa maziwa au nyama za wazazi wake
  • Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora
  • Lisha dume malisho bora na maji safi ya kutosha.  Pia apatiwe chakula cha ziada.
  • Katika ufugaji shadidi dume la ng’ombe  lifugwe kwenye banda imara lenye sehemu za kuwekea chakula maji na kufanyia mazoezi.
  • Katika ufugaji huria dume atengewe sehemu na kupatiwa chakula cha ziada.
  • Dume livalishwe pete puani kwa ajili ya kupunguza ukali na kuwezesha urahisi wa kumshika.
  • Dume apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingan ana ushauri wa mtaalam wa mifugo na
  • Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora.
PITIA
ZITAMBUE KABILA TOFAUTI TOFAUTI ZA KUKU WA KIENYEJ

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Tufaa

Tufaa ni tunda moja maarufu duniani ambalo hupendwa kuliwa na watu wa jamii zote, hii inatokana na utamu wake pamoja na faida za kiafya zinazopatikana

Read More »

Afisa Kilimo

Afisa kilimo Mkoa wa Mbeya  akipokea maelezo ya kilimo cha mboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na

Read More »

Kilimo cha Kabichi

Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »