Kilimo cha Binzari

tangulizi
Jina la kitalaam ni Curcuma
domestica na kwa kiingereza
ni turmeric. Zao hili asili
yake ni Mashariki ya Mbali,
na linalimwa zaidi katika
mkoa wa Tanga, Kagera,
Kilimanjaro, Morogoro na
Zanzibar.
Matumizi
Binzari hutumika kwa
mapishi ya nyama, samaki na
mapishi mengine kwa kuweka
rangi yake ya njano.
Hutumika zaidi na nchi za
mashariki kama India; nchi za
Ulaya hutumia kidogo sana.
Uzalishaji
• Hali ya hewa
Humea vizuri maeneo yenye
kiasi cha joto la nyuzi 24-26
za sentigredi na huzalishwa
maeneo ya mwambao.
• Udongo
Udongo wenye rutuba na
unaopitisha maji na usio na
mawe au changarawe.
Mahitaji ya mvua ni milimita
1200-2000 kwa mwaka.
Epuka kusimama kwa maji
shambani. Umwagiliaji
unaweza kufanywa endapo
maji hayatoshelezi. Binzari
inafanya vizuri ikipandwa
sehemu ya uwazi. Ingawa pia
inaweza kuchanganywa na
mazao mengine kama minazi.
• Uchaguzi wa mbegu
Mbegu zinazotumika hapa
nchini ni za kienyeji bado.
Tunguu kubwa zenye ukubwa
wa sm 2.5 hadi sm 3
hutumika kama mbegu.
Kiasi cha tani1.7 za
vipando huhitajika kwa
hekta. Tunguu za
kupandwa zisihifadhiwe
kwa zaidi ya mwezi
mmoja kabla ya kupanda.
• Nafasi ya
upandaji
Nafasi ya kupanda ni sm
30-45 kati ya mmea na
mmea.
• Mahitaji ya
mbolea
Matumizi ya mbolea
hapa Tanzania si
makubwa katika kilimo
cha viungo. Tafiti
zimeonesha kuwa
binzari hazioneshi
kufanya vizuri kwenye
mbolea za viwandani.
Mbolea za samadi
zinaweza kutumika.
Uvunaji
Uvunaji hufanywa kwa
kutumia majembe au
uma. Binzari huvunwa
wakati majani
yamegeuka rangi na
kuwa njano au kahawia.
Binzari isiyo na
kambamba huvunwa
kipindi cha miezi sita
toka kupandwa na miezi
18 hadi 21 kwa binzari
iliyokomaa
kutegemeana na mahitaji
ya soko.
Mavuno ya tani 7
hupatikana endapo
binzari ikipandwa peke
yake. Mavuno hupungua
kiasi binzari ikipandwa
mchanganyiko na mazao
mengine kwa mfano
mavuno ya tani 4.8 kwa
hekta yatapatikana binzari
ikipandwa na minazi.
Utayarishaji
.Kabla ya kuhifadhiwa
binzari huchemshwa,
huanikwa juani kisha
hutwangwa/husagwa.
Mashambulizi ya wadudu
na magonjwa
Tatizo kubwa ni ugonjwa
wa ukungu unaosababishwa
na vimelea vinavyoitwa
Colletotrichum sp. na
Glomerella cingulata. Dalili
ni madoa ya kahawia
kwenye majani ambayo
husambaa na kisha jani
hukauka. Magonjwa haya
yanaweza kudhibitiwa kwa
kupiga dawa za ukungu
kama Dithane M-45 kila
baada ya wiki mbili.
Masoko
Soko la binzari linapatikana
ndani na nje ya nchi. Bei ya
ndani ni kati ya Sh 350-
600/- kwa kilo. Zao hili
huuzwa katika nchi za
Uganda, Kenya, Uingereza,
Ujerumani, Mashariki ya
Kati, n.k.
Ushauri
Wakulima wanashauriwa
kukausha binzari kwa
uangalifu ili kutoharibu
ubora wake.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na :
Sehemu ya Uinuaji Mazao,
Wizara ya Kilimo Chakula
na Ushirika,
S.L.P. 9192,
DAR ES SALAAM.Simu: 022 2864899
Fax : 022 2864899/2862077
E-mail: cps@kilimo.go.tz

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO CHA BAMIA

 BAMIA Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama

Read More »

KILIMO BORA CHA SOYA

Soya ni zao jamii ya mikunde ambayo ina baadhi ya sifa za mbegu zinazozalisha mafuta. Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »