Badili Maisha Yako Kwa Kuwekeza Kwenye Kilimo Hiki Cha Vitunguu Saumu

Kitunguu saumu ni moja kati ya zao bora lenye manufaa mengi kwa matumizi ya kila siku kwa maisha ya mwanadamu, kiafya, Kitabibu na kwa ajili ya kutengeneza au kuchanganyia katika dawa tofauti. Pia ni kiungo mahusui katika mambo ya mapishi.

Zipo aina tisa za vitunguu swaumu ambazo hulimwa hapa
duniani katika maeneo mbalimbali.

Aina za vitunguu saumu maalufu kwa matumizi ya kawaida ni tatu,

1. SOFT NECK – ni nyeupe huzaa kwa muda mfupi.

2. SILVER SKIN – vina rangi ya silver vikikaushwa vinaweza kukaa hadi mwaka mmoja.

3. ANTICHOKE – vina rangi nyekundu kwa mbali.

katika nchi yetu ya tanzania vinapatikana vitunguu swaumu ya aina tatu

1. Kitunguu saumu chenye mafuta makali.

2. Kitunguu saumu chenye madini ya protini

3. kitunguu saumu chenye madini, protini na mafuta mepesi.
Hiki ndicho tulacho kila siku hapa kwetu na wengi hutumia kama dawa wakati hakina sifa za kuwa dawa.

NAMNA YA KULIMA
Kitunguu hiki hulimwa katika maeneo yenye baridi uwanda wa jua hafifu, mvua za wastani na joto hafifu, aridhi iwe nyeusi yenye rutuba na mfinyanzi, kusiwe na upepo mkali au ukungu mwingi.

Hulimwa kwa kuandaa kitaluna kupandikizwa baada ya miche kufikia urefu wa inchi 6-14, hupandwa kwa mstari na mche hadi mche ni nchi 3-4 na mstari kwa mstari ni nchi 12.

Kwa kifupi kitunguu swaumu ni kati ya zao gumu sana kulilima kwani hustawi katika maeneo machache sana hapa duniani. Kwa hapa tanzania hustawi katika mkoa wa manyara wilaya ya Mbulu, Hanang na babati kidogo, pia kidogo mkoa wa kilimanjaro na kwa eneo lolote ambalo hali inaendana na maeneo tajwa hapo juu.
kwa morogoro vinalimwa maeneo ya mgeta.

PITIA
Kilimo bora cha nyanya

UANDAAJI WA SHAMBA

Tifua udongo kidogo kisha ufanye hallowing ili kurahisisha upandaji na ukaaji wa mimea tu. Tengeneza tuta za mita 1 hadi 1.5, upana mita 10 urefu. Kwa upande wa mbolea Inashauliwa utumie WINNER

UPANDIKIZAJI

Vibanguliwe vipandwe kwa kuelekezea mizizi chini na kina cha wastani 2.5 inchi, mbolea ya samadi hushauriwa zaidi kutumika, Huvunwa baada ya miezi 4 -6 kulingana na hali ya hewa na aina ya mbegu iliyotumika.

SPACING/ MUACHANO WA MBEGU NA MBEGU

Mstari hadi mstari ni inchi 8 na mmea hadi mmea ni inchi 6 yaani  (8*6)inchi

KIWANGO CHA MBEGU
Kiwango cha mbegu ni kilo 200 – 300 kwa heka moja

MAVUNO
Ni tani 5 -6 kwa heka moja

UANDAAJI WA MBEGU
Kitunguu swaumu hupandwa “BULB” na  sio mbegu kama vitunguu maji. Ni ile Punje ambayo Imekuwa na kukomaa vizuri na isyoathiliwa na magonjwa

Moja ya shamba la vitunguu

MAGONJWA
1. Vitunguu saumu havishambuliwi na magonjwa kama ilivyo mazao mengine.
2. Mimea ikianza kutoa maua, yaache yawe marefu hadi yajikunje kisha utayakata ili kuongeza uzalishaji.
Wadudu wasumbufu ni THRIPS na ukungu upande wa magojwa.
Kwa upande wa ukungu anza na  RIDOMILL GOLD upulizie mara nne kisha malizia na score kwa ajili ya Thrips tumia ACTARA au MATCH.

Hushambuliwa na magonjwa kuanzia wiki ya Tatu hadi ya saba, Tumia madwa ya kupuliza yatumikayo kwa nyanya na vitunguu vya kawaida.

SOKO
Kwa kariakoo kilo moja ni kati ya TSH 4000 hadi 6000. Ila kwa ujumla ni bidhaa ambayo inahitajika kwa wingi ndani na nje ya nchi.

Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya kilimo bora.

PITIA
KILIMO-BIASHARA

MAKALA HII IMEANDALIWA NA SAID MALOGO, MTAALAMU WA MASUALA YA KILIMO.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

UFUGAJI WA KAMBARE KITAALAMU 2

Katika toleo liliotangulia, tulizungumzia kuhusu utayarishaji wa mabwawa na matangi ya kufugia kambare, muda na kiasi cha mbolea na chokaa kinachohitajika kuongezwa kabla ya kuingiza

Read More »

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI : Watu wengi duniani hudhania kwamba faida ya nyuki ni uzalishaji wa asali tu, na si vinginevyo. Lakini karne za hivi

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »