CHAKULA BORA CHA SUNGURA – Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Kwa uzoefu wangu wa ukulima na ufugaji wa asili, na hata wataalam wanathibitisha hili, sungura ni mnyama rahisi wa kufuga kwani hana gharama kubwa na ndiyo maana shughuli hii inaweza kufanywa na mkulima mdogo asiye na mtaji mkubwa.

Chakula cha sungura ni kama nyasi, mboga kama vile sukuma, spinachi, kabichi, karoti, mchunga na pia unaweza kununua chakula halisi cha sungura kutoka maduka ya vifaa vya wanyama.

Sungura akila vyakula hivi vibichi anakojoa mara kwa mara, na nilivyodokeza katika makala iliyotangulia, mkojo wake ni mali unaweza kukuleta kipato kikubwa kwa sababu unatumika katika maabara.

Hata hivyo, kama unataka kumkinga na magonjwa ya tumbo, unashauriwa kukausha chakula chake, jambo ambalo pia husaidia asikojoe hovyo.

Kama nilivyoeleza hapo awali, kila kizimba cha sungura lazima kiwe na eneo ama chombo cha kuwekea chakula, tena unaweza kuongeza chemba maalumu kwa ajili ya kuwekea nyasi.

Chemba hiyo ni vyema iwe na nyasi maalumu kila wakati – na wataalamu wa ufugaji sungura wanapendekeza majani aina ya Alfalfa, lakini kama unapata majani ya mchunga ni mazuri sana kwa sababu hawa jamaa wanayapenda mno kwani yana viinilishe vingi.

Sungura wanakula vyema nyasi zikiwa zimekatwa katwa katika kipimo cha inchi tatu au nne. Kusanya kitita cha majani na ukikate kwa panga kwa urefu huo.

Unaweza pia kumlisha sungura wako mikundekunde na jamii yake, kabichi, spinachi na Sukuma wiki. Usisahau kwamba wanakula pia mizizi na ikiwa karoti zinapatikana wapatie.

Hata hivyo, hakikisha unaondoa mabaki yote ya chakula ambacho wameshindwa kula. Ondoa kila siku kwenye kizimba na baada ya muda utagundua wanapendelea nini zaidi, kwa sababu unaweza usikute mabaki.

PITIA
UCHANGANYAJI WA VYAKULA VYA MIFUGO

Walishe sungura wako mboga mboga kwa taratibu kama hawajazowea mpaka watakapokuwa wamezowea. Wakati mwingine wakil asana wanavimbiwa au hupata ugonjwa wa kuhara.

Pia uwalishe vyakula maalumu vya sungura vinanvyopatikana kwenye maduka ya vyakula vya mifugo. Unaweza kuwalisha hata njugu mawe kwa sababu wanazipenda pia.

Unaweza kupata mwongozo wa awali hata kwa mtu ambaye amekuuzia sungura hao namna anavyowalisha, lakini kama kuna ofisa ugani karibu yako, mtumie ili akuelekeze vyema. Sungura mmoja mkubwa huweza kula chakula kiasi cha gram 100 had 130 kwa siku nahii   ni kwa chakula chake maalumu special kwa sungura. Pamoja na chakula cha ziada kama vile majani mabichi majani makavu nk.

MFANO WA MCHANGANUO WA CHAKULA BORA CHA SUNGURA

Namba AINA YA CHAKULA KIASI
1 Pumba za Mahindi 40kg
2 Mashudu ya Alizeti 30kg
3 Pumba za Mpunga 15kg
4 Soya 5kg
6 Chumvi 0.5kg
Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo