FAHAMU: KILIMO BORA CHA KUNDE

1. UTANGULIZI

Kunde ni zao ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula na bishara pia. Ni zoa lenye kiasi kukubwa cha protini na majani yake yanaweza kutumika kama mboga za majani. Ni zao ambalo linatoa mavuno ya Kiasi cha kilogram 500 hadi 1500 kwa ekari. Kwa soko, zao la kunde limekuwa na soko zuri muda mwingi ukilinganisha na mazao mengine kama mahindi.

2. MAANDALIZI YA SHAMBA LA KUPANDA KUNDE

maandalizi ya shamba la Kunde
Maandalizi ya Shamba la Kunde

Shamba la kunde linapaswa liandaliwe mapema kabla shughuli ya upandaji kuanza, Kama ni la kukata miti mikubwa miti ikatwe mapema,Kama ni la kufyeka nyasi na miti midogo shughuli hii ifanyike mapema kabla hatua ya kulimwa kwa shamba kwa kutumia trekta,Pawatilla,jembe la ng’ombe au la mikono.shamba lisawazishwe na kukusanywa mabaki ya mimea au visiki na mawe madogomadogo kama yapo.

3. HALI YA HEWA IFAAYO

Kunde ni zao linalostahimili ukame, Kunde hukubari vizuri katika mwinuko wa mita 0 hadi1500 kutoka usawa wa bahari. kunde huweza kulimwa katika maeneo yapatayo mvua kidogo kiasi cha milimita 500 hadi 1200 kwa mwaka. Hukuwa vizuri katika joto la nyuzi 28 hadi 32 C.

4. ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA KUNDE

Kunde huweza kulimwa katika udongo usiotuamisha maji  wa aina tofauti tofauti kuanzia kichanga hadi mfinyazi.Zinaweza kupandwa katika udongo usio na rutuba ya kutosha lakini hustawi vizuri katika udongo wa tifutifu kichanga au tifutifu mfinyanzi au  mchanganyiko wa mfinyazi na kichanga wenye uchachu kati ya 6 hadi 7

5. NAFASI YA UPANDAJI

Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za kunde ambazo zimegawanyika katika makundi makubwa mawili.Kunde zinazosimama na kunde zinazotambaa.

Unaweza kutumia nafasi zifuatazo kwa kupanda kunde zako:

KUNDE ZINASOSIMAMA-Tumia sentimeta 45 hadi 50 mstari hadi msatari na sentimeta 15 hadi 20 shina hadi shina katika mstari. Shamba lilimwe na kusawazishwa vizuri kwa vile mbegu ni ndogo. Aina hii hupandwa katika mvua fupi. Inashauriwa aina hizi zipandwe wakati wa mvua kubwa (mwezi mmoja kabla ya mvua kwisha), ili zikomae kukiwa hakuna mvua. Panda kwa kutoboa vishomo kwa fimbo. Panda katika nafasi za sm 50 x sm 20, kwa kuweka mbegu 2 kila shimo kiasi cha mbegu kwa hekta ni kilo 20. Hikikisha shamba lako halina magugu kwa wiki sita na baada ya hapo palilia inapobidi. Unaweza kuchanganya na mazao mengine ya kunde kwa mbaazi.

KUNDE ZINAZOSAMBAA-Tumia nafasi ya #Sentimeta 70 hadi #75 mstari hadi mstari Kwa#sentimeta 25 hadi #30 shina hadi shina katika mstari. Lima na kusambaza udongo shambani hadi uwe laini kwa vile mbegu ni ndogo. Aina hii ya kunde hupandwa wakati wa mvua nyingi, na ipandwe miezi miwili kabla ya mvua kumalizika. Panda kwa kutoboa mashimo kwa fimbo /kijiti. Panda kwa nafasi ya sm 75 x sm 20, mbegu moja kwa shimo. Kiasi cha mbegu kwa hekta ni kilo 8. Shamba lipaliliwe lisiwe na magugu kwa wiki sita. Baada ya hapo palizi ifanyike kama itabidi.

Kumbuka…

Wakati wa kupanda kunde zinatakiwa kufikiwa kiasi cha #sentimeta 2.5 hadi #5 ardhini pia mkulima anashauriwa kupanda mbegu mbili hadi mbegu tatu kwa kila shimo na baadaye punguza uache 2 kwa kila shimo kama unauhakika wa mbegu zako unaweza kupanda moja kwa moja mbili mbili kwa shimo

PITIA
Kilimo cha Kunde

6. AINA ZA KUNDE

Tumaini – Sifa za jumla:

Hukomaa kwa muda wa #siku 75 – 90. Aina hii ya kunde husambaa ina maua yenye rangi za zambarau na mbegu zake ni mviringo. Maeneo yanayoshauriwa kupanda ni yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Inahitaji udongo mwepesi wenye rutuba na usiotuamisha maji. Kunde hizi hutoa mazao hadi tani tatu kwa hekta moja. Huvumilia virusi vya mozaiki vinavyotokana na wadudu mafuta wa kunde na bakiteria.

Fahari – Sifa za jumla:

Aina hii hukomaa kwa siku kati ya 75 – 90. Mmea husambaa na maua yana rangi ya zambarau. Mbegu zake ni za mviringo. Hustawi maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500kutoka usawa wa bahari. Hutoa hadi tani 3 kwa hekta moja. Huvumilia magonjwa ya virusi wa CABMV na mabaka.

Vuli – 1 Sifa za Jumla:

Inakomaa kwa #siku 55 – 65. Hukua ka kunyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake ni nyekundu na za mviringo. Inastawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa #mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Ikipataiwa matunzo mazuri huto hadi tani 2 kwa hekta moja.

Vuli – 2 Sifa za Jumla:

Inakomaa baada ya #siku 65 – 70 baada ya kupandwa inaota ikiwa imenyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake zina weupe uliofifia na ni mviringo. Aina hii husitawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa #mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Katika matunzo mazuri aina hii huzalisha hadi tani 3.5 kwa hekta moja

WADUDU WAHARIBIFU KATIKA KUNDE;

Wadudu waharibifu wa zao la Kunde wako katika makundi mawili:-

(i) Kundi la kwanza ni la wadudu wanaoshambulia mimea ikiwa shambani. Ina maana mmea hushambuliwa baada ya kuona hali inapokomaa na kutoa mbegu. Kundi la wadudu hawa lina tabia ya kufyonza (Sap = supu) yam mea kwenye majani, matawi, mashina, maua hata mbegu hasa zikiwa changa kama vitunda. Njia hii ndiyo pekee kwa wadudu wa kundi hili kujipatia mlo ili waishi na kuzaliana. Katika kundi la pili kuna wadudu wenye tabia ya kukata mashina na kuangusha mimea michanga na wengine hutafuna majani na maua. Zaidi ya uharibifu katika kula mimea, wadudu wengi ni hifadhi ya viini vya magonjwa ya virusi.

(ii) Kundi la pili nila wadudu waharibifu baada ya mavuno kuwekwa ghalani. Athari ya wadudu hawa inapelekea wakulima kupoteza mazao ghalani, kupunguza chakula ghalani pia kupunguza ubora wa mazao yanapopelekwa sokoni  kwani yanapofunguliwa soko lake ni duni.

Wadudu hao wa haribifu katika kunde ni

 • Foliage beetle (Ootherca mutabilis)

Wadudu hawa hushambulia mimea ya kunde baada ya mbegu kuota (Seedling stage). Wakiwa kwenye hatua ya mdudu kamili (adult stage) hushambulia majani kwa kula sehehmu kati ya vihimili vya jani (area between leaf veins). Mashambulizi ya wadudu wengi (haye number hutokea mmea kupoteza majani yote na hatamaye mmea kufa.

PITIA
Fahamu zaidi kuhusu sumu kuvu

Kuzuia jamii ya wadudu hawa:

Dawa za chemikali aina ya enolosulfan, Karate n.k. huangamiza mashambulizi kwa mpulizo mmoja.

 • Aphids (Aphis gaccivora)

Hawa ni kati ya wadudu wenye kusababisha hasara kubwa katika zao la kunde. Wanapendelea kula mvunga wa majani (under leaf), sehemu za vishina na hata vitumba vya mbegu. Athari za mashambulizi: Mmea hudumaa, majani husinyaa na kukunjamana pia hupukutika kabla hayajazeeka hatimaye mmea hufa.

Kuzuia Aphids: Dawa za chemikali aina ya phosphomiolon na dimethroate kwa sentimita za ujazo 40 katika lita 10 za maji (40 cm3kwa kila lita 10 za maji).

 • Thrips wa mauwa ya kunde (Megalurothrips sjostedti)

Hatua ya mdudu kamili hushambulia maua. Mimea ikishambuliwa sana haizai matunda kwasababu maua yameharibika. Mashambulizi yakiwa makubwa zao lote huangamia.

Kuzuia: Kwa kutumia chemikali aina ya Cypermethrin – kiwango cha sentimita za ujazo 40 katika lita 10 za maji.

 • Podsborer (Maruca testulalis)

Wadudu hawa hula mvungu wa majani, ganda la shina na vitumba vya mbegu katika hatua ya kukomaa. Athari: Mmea hudumaa, umbo la majani huharibika na hupukutika kabla ya kuzeeka. Mimea mingi hasa michanga hufa.

Uzuiaji: Kwa kutumia chemikali aina ya phosphomidon na dimethoate kwa kiwango cha sentimita za ujazo 40 katika lita 10 za maji.

 • Podsucking bugs (Anoplemenia, Riptortus, dentires, Acanthomia spp)

Wadudu hawa hushambulia mikunde katika hatua ya kuweka vitumba (pods formation). Hasara, inayosababishwa, na wadudu hawa hufikia 90%. Madhara makubwa huletwa na hatua ya wadudu kamili (adult stage/ kwa kufyonza “Sap = Supu” ya vitumba teketeke ambavyo husinyaa na kukauka bila kukomaa wala kuwa na mbegu.

Kuzuia: Kwa kutumia chemikali za Endosulfan au dimethoate kwa kiwango cha sentimita za ujazo 40 katika lita 10 za maji.

 • Kunguni wa kufyonza mifuko ya mbegu ya kunde (Hemiptera spp.)

Kunguni wa kufyonza mifuko ya mbegu ni kundi la wadudu waharibifu wakubwa wa kunde katika Afrika kusini mwa Sahara. Ni vigumu kuwadhibiti kutokana na uwezo wao wa kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine. Si rahisi kwa mkakati mmoja wa udhibiti dhidi yao kufaulu. Mbinu jumuishi zinazochanganya mbinu za kitamaduni, kama vile kupanda mapema na matumizi ya mbolea, zikichanganywa na utumiaji makini na kwa wakati muafaka wa madawa ya kuua wadudu zinaweza kuzuia wadudu hawa.

 • Cowpea storage weevils.

Mashambulizi ya wadudu hawa wawili huanzia shambani wakati kunde zimekaribia kukomaa. Wadudu hutaga mayai kwenye vitumba vilivyokomaa. Mayai yakiangauliwa, funza hupenya kupitia kwenye matobo yanayosababishwa na wadudu wengine. Funza wakianguliwa hushambulia mbegu na uharibifu hufikia 70% ya mbegu safi.

Kuzuia: Tumia chemikali aina ya Acteric Super Dust 100mg za unga wa dawa katika 10 Kg za mbegu safi (Seed grain).

 MAGONJWA YA ZAO LA KUNDE NA NAMNA YA KUZUIA:

Magonjwa hatari yanasababishwa na vimelea vya virusi na vya bacteria aina tabia na uzuiaji wa magonjwa haya ni kama ifuatavyo:-

 • Cowpea aphid-born mosaic virus:
PITIA
KILIMO BORA CHA ULEZI

Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hupelekea mkulima kupata hasara ya 13 – 87% ya zao. Dalili; za ugonjwa huu ni michirizi ya rangi ya kijani iliyochanganyika na njano au ya ugoro (mosaic & mottling) kwenye majani.

Kuzuia: Kwa kutumia aina za kunde zenye kustamili ugonjwa huu kama Tumaini, Fahari na Vuli.

 • Bacterial bligh (Xanthomonas Spp)

Ugonjwa hushambulia aina ya kunde pori na zinazolimwa. Ugonjwa huu hushambulia sana miche na kiasi cha 60% ya miche yote yaweza kufa kama ugonjwa huu hautadhibitiwa mapema.

Dalili: Vidonda vidogo huonekana uvunguni mwa majani. Katika mimea dhaifu (more susceptible) vidonda huungana na kuwa na umbo la duara lenye ukubwa wa kipenyo cha 1-3 cm. Mwanzoni vidonda huonekana kufutuka mvunguni mwa jani kadiri vinapokomaa huwa na rangi ya kahawia upande wa juu na majani. Baada ya muda vidonda hukauka na hubakisha migonyeo sehemu zilizoathirika. Majani mengi yaliyathirika hubadilika kuwa njano na baadaye huanguka / hupukutika.

Ueneaji: Ugonjwa huenea kwa kasi wakati wa mvua nyingi na umwagiliaji unapokuwa wa juu. (Overhead irrigation). Kimelea cha bacteria huyu hudumu kwenye punje (mbegu). Kwa hiyo mbegu za namna hii huota zikiwa na viini vya ugonjwa.

Kuzuia: Kutumia mbegu zenye kustahimili ugonjwa huu kama Tumaini, Fahari na Vuli.

 • Anthracnose ya kunde (Colletotrichum destructivum)

Anthracnose ya kunde ni ugonjwa wa kuvu unaoathiri mashina, matawi, na mashina ya majani na maua. Ugonjwa huu huanza wakati mbegu zilizoambukizwa zinapopandwa. Madoa ya kahawia hutokea kwenye majani na kuzalisha idadi kubwa ya mbegu za kuvu, zinazosambazwa kupitia matone ya mvua na kwa mvua yenye upepo.

Ugonjwa huu hutokea katika sehemu zenye mvua nyingi. Hatua muhimu za usimamizi zinahusisha matumizi ya mbegu zinazohimili au sugu, mbegu zilizotibiwa na dawa za kuua kuvu na kwa kilimo mseto na nafaka.

 •      Doa jani cercospora (Mycosphaerella cruenta)

Doa jani cercospora ya kunde ni ugonjwa wa kuvu. Husababisha majani kuanguka na hasara kubwa ya mavuno ya kunde ya hadi asilimia 40. Aina nyingiza kunde ni sugu lakini pia ziko ambazo hushambuliwa, kwa hivyo kunahitajika uangalifu katika kutambua aina zifaazo kwa ajili ya kupanda.

Ugonjwa hutokea kwa aina nyingine za mikunde, ikiwa ni pamoja na mimea inayohusiana kwa karibu kama vile, maharagwe ‘kweli’ (Phaseolus) na maharagwe ya soya. Ugonjwa huu hausambazwi kupitia mbegu lakini huendelea kuishi na kufikia msimu ujao kwa kutumia wenyeji mbadala, pamoja na mabaki ya mazao. Dawa za kuua kuvu zinaweza kutumika kusafisha mbegu na kuzuia kuzuka kwa ugonjwa. Ugonjwa huu ni muhimu katika nchi ambazo kunde hupandwa kwa wingi.

Wewe Kama Msomaji wetu wa Kilimo Cha Kunde Tumeona Pia unaweza Pitia Nyaraka Hizi :-

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo bora cha nyanya -Tz

Utangulizi Nyanya ni zao la mboga linalolimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Nyanya ni aina

Read More »

KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO

UTANGULIZI Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »