FAHAMU KUHUSU CHANJO YA MDONDO, KITALAMU 1-2 VACCINE

Chanjo hii ina virusi hai vya mdondo vinavyotengeneza kinga dhidi ya ugonjwa wa mdondo/kideri. Virusi hivi vimeoteshwa kwenye mayai ya kuku wasiokuwa na magonjwa anuwai.Chanjo hii inapatikana katika chupa zenye ujazo wa dozi ya kuku 100 na kuku 200.

Image result for UGONJWA WA MDONDO

HifadhiChanjo ya 1-2 imehifadhiwa katika chupa za plastiki ambazo ni rahisi kusafirisha na zina mfuniko wenye sili. Ukishafungua mfuniko mdomo wa chupa unatumika kudondoshea matone ya chanjo kwa urahisi na kwa usafi zaidi.UtunzajiChanjo ya 1-2 inasambazwa katika hali ya majimaji. Chanjo hii ni stahimilivu kwa joto, ikihifadhiwa kama inavyoelezwa hapo kwa njia zifuatavyo;Chanjo ndani ya jokofu kamwe isiwekwe kwenye sehemu ya kugandishia barafu (freezer), Kama hakuna jokofu, chanjo hii itunzwe kivulini, kwenye hali ya ubaridi na kutumiwa haraka iwezekanavyo.Hifadhi ya chanjo na muda wa matumiziChanjo ihifadhiwe kwenye nyuzi joto kati ya 2-8 (jokofu) muda usiozidi miezi mine, nyuzi joto kati ya 25-30 muda usiozidi siku 7 na nyuzi joto zaidi ya 30 kwa siku 2. Chanjo iliyofunguliwa itumike ndani ya siku 2.UsafirishajiChanjo isafirishwe kwenye hali ya ubaridi ndani ya kasha la barafu lenye barafu, vinginevyo chanjo isafirishwe kwenye chombo baridi kama kasha la karatasi lenye magazeti na barafu au chupa za plastiki za maji ya chumvi nyingi yaliyogandishwa.Katika hali ya vijijini, chupa yenye chanjo iviringishwe kutambaa cha pamba kilichowezeshwa maji baridi na huku isafirishwe kwenye kijikapu kidogo kilichofunikwa chenye matundu makubwa yapitishayo hewa pande zote.MatumiziChanjo itumike moja kwa moja toka kwenye chupa ya chanjo bila kuchanganya na kitu chochote. Weka tone moja la chanjo kwenye jico moja la kila kuku.Muda wa kuchanjaKuku wa umri wowote wanaweza kupatiwa chanjo. Chanjo ifanyike kila mara baada ya miezi mitatu (3)Kumbuka

  • Epuka kuweka chanjo kwenye joto la juu na mwanga wa jua.
  • Chanjo hii ni kwa kukinga ugonjwa wa mdondo au kideri tu.
  • Chanja kuku wenye afya tu (Epuka kuchanja kuku wagonjwa).
  • Hii ni chanjo na wala siyo tiba, hivyo isitumie kuchanja kuku wagonjwa.
  • Chanjo hii haina madhara kwa vifaranga, wala ukuaji au utagaji wa mayai.
  • Kuku hupata kinga ya kutosha dhidi ya ugonjwa wa mdondo au kideri siku 7 hadi 14 mara baada ya kuchanjwa.
  • Kuku wachanjwe kila baada ya miezi mitatu (3).
  • Dozi (tone moja kwa kuku wa umri wowote (kuanzia kifaranga wa siku moja hadi kuku mzee) au wa jinsia yeyote.
  • Kama tone halikuingia vizuri kwenye jicho, rudia kwa kuweka tone la pili.
  • Kwa maelezo zaidi muone mtaalamu wa mifugo aliye karibu na wewe kwa utaalamu.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA MAPAPAI

KILIMO CHA MIPAPAI •Kwa jina la kisanyansi ni Carica papaya,jina la kawaida ni papai. •Tunda la mpapai lina virutubisho vya vitamin A,B na C kwa

Read More »

Kilimo Bora Cha Bilinganya

Bilinganya  imo  katika   jamii   ya  mimea   inayohusisha   nyanya,  pilipili,  viazi  mviringo  na  nyanya  mshumaa.    Mboga  hii  ina   viini lishe

Read More »

UFAHAMU UGONJWA WA KUKU WA KUVIMBA MACHO

Chanzo cha maambukizi •Maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na kwenye vimelea•Kupitia mfumo wa hewa kutoka kuku wagonjwa•Kupitia mayai, hivyo maambukizi huendelea kutoka kizazi

Read More »

Njoo ujifunze kilimo cha nyanya

NYANYA ni zao linalopendwa kutumiwa….kunogesha chakula, chakula kilichowekwa NYANYA huwa na radha nzuri inayomvutia mlaji Wakulima wengi hutamani kulima zao hili wengi huandika FAIDA na

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »