ASILI
Kiasili ni mbuzi wa Afrika ya kusini ingawa ndani yake kuna damu toka baraUlaya na India, hii ndio Mbegu kubwa Zaidi ya mbuzi wa nyama ukilinganisha na wengine. Pia wanazalisha kiwango kikubwa cha maziwa ingawa wanafaa Zaidi kwa nyama.
RANGIWana mwili wenye rangi nyeupa na kichwani wana rangi nyekundu au hudhurungi (brown) ingawa wapo weupe kabisa au wekundu/hudhurungi kabisa na hii hutokea kwa 0.001%
UMBOWana umbo kubwa kufikia kilo 110-135kwa madumeKilo 90-100 kwa majikeWana masikio yaliyolala kama mbuzi wa kinubi (Nubians)
UZAZIHuwa wanazaa mapacha na huweza kuzaa mara 2 kwa mwakaMajike ni wazazi na walezi wazuri wa watoto sababu wana maziwa ya kutoshaWatoto hukua haraka sana, na nia aina ya mbuzi ambao sio wakorofi (docile)Kwenye baridi kali au joto kali huwa inawaathiri kwenye kubeba mimba