FAHAMU KUHUSU UFUGAJI WA KUKU WEUSI KUTOKA MALAWI (AUSTRALORP)

Australorp wanastahimili mazingira tofauti, kama kuku wa kienyeji aliye zoeleka nchini Tanzania. Na ni wazuri kwa ufugaji huria, kwa kuwaachia nje wajitafutie chakula wenyewe. Ingawa wanajulikana kwa sifa yao ya utagaji mayai mengi, lakini kuku hawa wanafaa kwa nyama pia, kwani huwa na nyama nyingi sana (dual purpose chickens)


Kuku hawa huweza kumpatia mfugaji faida kubwa, kwani ni wazuri kwa biashara ya mayai na nyama pia. Hawana sifa nzuri ya kulalia mayai, lakini akilalia hutotoa vifaranga vingi, na ni wazuri kwa uleaji wa vifaranga hivyo.


Utagaji wao wa mayai unakaribia ule wa kuku wa kizungu. Kuku hawa ni wakubwa, wazito, na wanamvuto sana kuwaangalia. Wanapendeza pia kwa ufugaji mdogo, katika mazingira ya nyumbani. Wana michirizi ya kijani pale wanapomulikwa kwenye mwanga mkali wa jua.

Kwa wastani Black Australorp, hufikisha mayai 250 kwa mwaka, wakiwa katika mazimgira mazuri. Kuku hawa ni wapole na rafiki kwa binadamu. Black Australorp ni wagumu, hawapati magonjwa mara kwa mara, hivyo basi huvumilia magonjwa ya aina nyingi, na hawachagui chakula. Wanakula vyakula wanavyo kula kuku wengine wa kienyeji. Huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi mitano na nusu hadi sita.


Jogoo hufikisha kilo 3.5 – 5.0 na

Temba/hen hufikisha kilo 3.0 – 3.7

PITIA
UFUGAJI BORA WA BATA

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo Bora cha maharage

UTANGULIZI Maharage ni moja kati ya mazao ambayo yanalimwa sana na ni moja kati ya mazao yanayo waongezea kipato wakulima wengi sana nchini Tanzania lakn

Read More »

Kilimo cha Pilipili Manga

Kilimo cha Pilipili Manga, kuanzia mbegu bora, magonjwa, utaalamu mpaka masoko Katika kuabarishana fursa lukuki zilizoko kwenye maeneo tofauti tofauti ndani ya inchi yetu leo

Read More »

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI : Watu wengi duniani hudhania kwamba faida ya nyuki ni uzalishaji wa asali tu, na si vinginevyo. Lakini karne za hivi

Read More »

Kilimo bora cha nyanya -Tz

Utangulizi Nyanya ni zao la mboga linalolimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Nyanya ni aina

Read More »
UFUGAJI WA NG'OMBE

UFUGAJI WA KISASA WA NG’OMBE

UTANGULIZI Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi.  Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »