FAHAMU MAMBO MAWILI KABLA HUJAANZA KILIMO BIASHARA

Habari za leo ndugu msomaji wangu na pole kwa shughuri mbalimbali za ujenzi wa Taifa. Jumatatu iliyopita nilikuandikia nilikuandikia makala inayokufahamisha Kilimo bora cha zao la muhogo lakini leo nimekuletea kitu cha tofauti kidogo. Unapoanzisha mradi unatarajia mwisho wa siku uumalize kwa kupata faida, sasa basi leo nataka nikufahamishe mambo makubwa mawili unayotakiwa kuyajua kabla hujaanza mradi wako wowote wa kilimo.

Jambo la kwanza: Farming master-plan

Hili ni jambo la kwanza na muhimu sana kulifahamu. Farming master-plan ni muongozo wa shughuri zote unazotakiwa kuzifanya katika kilimo chako tangu kuandaa shamba mpaka kuvuna. Hii ijumuishe shughuri kama kupanda, kudhibiti magugu, uwekaji wa mbolea na kupulizia madawa ya wadudu na magonjwa. Unatakiwa kujua shughuri hizi zote, muda wa kuzifanya, namna ya kuzifanya na mahitaji yake ili uzifanye.

Kwa mfano uwekaji wa mbolea: wakati gani uweke? kiasi gani? uwekeje? Unatakiwa ufahamu haya yote kabla hujaanza mradi wako wa kilimo ilii usipate usumbufu wakati wa utekelezaji.

Jambo la pili: Gharama za uzalishaji na makadirio ya faida

Hili ni jambo lingine muhimu sana. Najua hujaamua kulima ili ujifurahishe tu, unatafuta faida hivyo basi unatakiwa ujue mradi wako utakugharimu kiasi gani katka utekelezaji wake na mwisho wa siku utakulipa kiasi gani? Pengine hutopata gharama halisi lakini ni lazima ufahamuu japo makadirio ya gharama ili kwanza uweze kujipanga lakini pia usikwame katika utekelezaji wa mradi wako.

Kwanini ni muhimu kufahamu mambo haya?

  1. Utajua mahitaji muhimu unayotakiwa kuwa nayo kabla hujauanza mradi wa kilimo 
  2. Utapata fursa ya kuuona mradi wako katika hatua mbalimbali hata kabla hujauanzisha
  3. Utaweza kujua makadirio ya gharama za uzalishaji na faida tarajiwa 
PITIA
KILIMO BORA CHA SOYA

Kwa hiyo nikunasihi ndugu yangu usianzishe mradi wako wa kilimo mpaka ujiridhishe kuwa unayafahmu mambo haya mawili.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »