FAHAMU NAMNA NZURI YA KUVUNA MAJI YA MVUA KWA AJILI YA KILIMO NA MIFUGO

Lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi mvua iliyokuwa ikitegemewa sana na wakulima kama chanzo cha maji kwa mimea imekuwa sio ya kuaminika tena kwani hainyeshi tena kwa wakati, hunyesha kwa kiasi kidogo sana(450mm-600mm), maeneo mengine hunyesha kwa kiasi kikubwa sana mpaka kusababisha mafuriko ambayo huharibu vibaya mazao ya wakulima mashambani, pia baadhi ya vyanzo vya maji vimekauka na hivyo kusababisha uhaba mkubwa sana wa maji sio tuu kwenye kilimo bali hata kwenye upatinaji wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani

KWA NINI TUVUNE MAJI YA MVUA

Kama nilipoeleza hapo awali kuwa kuna baadhi ya maeneo mvua hunyesha kwa kiasi kidogo sana na hivyo hazitoshelezi kumalizia msimu mzima ili mazao yaliyo shambani yaweze kukomaa mfano wa maeneo hayo ni Rombo, Same, Lushoto,Baganoyo,kisarawe,mkuranga n.k pia maeneo ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora n.k ambapo mvua inayonyesha katika maeneo haya inakadiriwa kuwa 550mm kwa mwaka, hali hii imesababisha matatizo makubwa sana katika maeneo hayo kama kukosekana kwa maji safi, baa la njaa, kipato kidogo kwa wakulima kwani hutegemea sana kilimo

Kwa kuliona hilo makala hii itakusaidia kujua namna ya kuvuna maji ya mvua ili yatumike katika umwagiliaji pale mvua zinapokatika ili kuongeza mavuno kwa wakulima na waweze kuondokana na umaskini pia utegemezi kwa serikali kwa kutoa chakula cha msaada

MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA KUTENGENEZA LAMBO

        I.Sura ya eneo husika(topography and terrain)

Hili ni la muhimu sana katika kuangalia sehemu ya kutengeneza lambo la kuhifadhi maji ya mvua, itabidi kuangalia kwa kitaalamu eneo ambalo maji yanatoka ili yaje kwenye lambo lenyewe(catchment area) pia lazma ifanyike survey ya eneo ambalo lambo litajegwa ili kuzuia mchanga au udongo kujaza lambo lako inabidi utaalamu wa kihandisi utumike.

PITIA
BANDA LA KULELEA VIFARANGA

     II.Kiasi cha mvua kinachonyesha katika eneo husika

Hii itakusaidia kujua na kukadiria kiasi cha maji unachoweza kuvuna pia ukubwa wa lambo  kwa ajili ya kutosheleza mahitaji yako

   III. Aina ya udongo

Udongo ni muhimu zaidi katika kuchagua na kuweza kujua kiasi cha maji kitakacho hifadhiwa katika lambo lako, pia data za udongo zitamsaidia mtaalamu kukuambia ni zao gani unatakiwa ulime pia ni kiasi gani cha maji kinachotakiwa wakati wa kumwagilia ili kupunguza upotevu wa maji na kusaidia mimea kukua vizuri

NAMNA YA KUTENGENEZA LAMBO

Awali ya yote kabla ya kuanza kutengeneza lambo lenyewe ni kuandaa njia ya kuyakusanya maji(runoff concentration) kutoka kwenye sehemu mbalimbali kama kwenye mifereji ya barabara, maeneo ya wazi kama maeneo ya kuegesha magari, maji yanayotoka kwenye makazi ya watu(rooftop water concentration) kwa hapa unaweza kutumia mawe (stonebudds) matuta  ili kuzuia maji na kuyaelekeza kwenye mrefeji unaoingia kwenye lambo ila matuta hayo lazima yapimwe kitaalamu ili yasiharibiwe na maji endapo mvua itakuwu nyingi

Kinachofuata baada ya hapo ni namna ya kutengeza mfereji unaopeleka maji maji kwenye lambo(grit channel design and filter drain), kwa kuwa maji yanayokuja huwa na michanga, udongo au tope ambayo yakiingia kwenye lambo lako husababisha lambo kujaa mapema na kuhifadhi kiasi kidogo cha maji, kwa hyo sasa mfereji huu inatakiwa uwe na usanifu mkubwa hasa kwenye mteremko wake(slope) ili kuzuia mchanga,matope na udongo kuingia kwenye lambo lako

Baada ya hapo lambo linatakiwa lichimbwe kwa ustadi kwa kufuata vipimo husika ili kuweza kuhifadhi kiasi cha maji kinachotakiwa pia kulingana na aina ya udongo katika eneo lako kitaalamu tutakuambia ni aina gani ya material yanayohitajika kwa ajili ya kuweka kwenye lambo lako ili maji yasipotee mfano unaweza kuweka karatasi ngumu za nylon (polythene papers) pia maeneo mengine yanahitaji tuu kushindilia vizuri ardhi ya chini ili iwe imara na isiruhusu maji kuzana chini.

PITIA
UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU

 

Kuzuia matope yasiingie kwenye Lambo

FAIDA ZA KUVUNA MAJI YA MVUA

  1. a)Kuvuna maji ya mvua inahitaji gharama ndogo sana lakini maji yanayovunwa ni mengi na huweza kutosheleza mahitaji ya mimea yako hata kama una shamba la hekari kumi endapo utaalamu utamika vizuri
  2. b)Maji yanayovunwa humpa mkulima uhuru wa kuyatumia atakavyo pasipo kubugudhiwa kwa sababu hayana bili wala malipo unapotumia
  3. c)Maji huvunwa na kutumika mahali husika kwa hiyo hakuna gharama sana za kuhitaji mabomba ya kusafirishia maji hayo

Pia kwa ujumla uvunaji wa maji ya mvua ndio suluhisho pekee la kutatua matatizo ya maji katika maeneo ammbayo yana uhaba wa maji na yanayokubwa na ukame kwa kipindi kirefu

Pia kuna utaalamu mwingine wa uvunaji wa maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya mifugo

Katika jamii zetu kama utaalamu huu utakuwa endelevu tutasaidika kwa kupata chakula cha kutosha, kuongoze kipatao na pia kuboresha maisha ya watanzania wengi kwa ujumla

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Karoti

KILIMO CHA KAROTI KILIMO CHA KAROTI : Zao la karoti asili yake ni Asia ya Kati. Zao hili lilienea nchi za Ulaya kwa kupitia Bahari

Read More »

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI : Watu wengi duniani hudhania kwamba faida ya nyuki ni uzalishaji wa asali tu, na si vinginevyo. Lakini karne za hivi

Read More »

Kilimo Bora Cha Alizeti

Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya

Read More »

Kilimo cha Binzari

tangulizi Jina la kitalaam ni Curcuma domestica na kwa kiingereza ni turmeric. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »