FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI : Watu wengi duniani hudhania kwamba faida ya nyuki ni uzalishaji wa asali tu, na si vinginevyo. Lakini karne za hivi karibuni jinsi binaadamu walivyoanza kujihusisha na tafiti za wadudu mbalimbali, walianza kupata habari nyingi za nyuki na hivyo kugundua mazao mengine zaidi ya asali.

FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI
FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI

• ASALI : Binaadamu alianza kuitumia asali kwa chakula na tiba takribani tangu kuwepo kwake ulimwenguni. Kwa mfano, asali na maziwa viliaminika kama vyakula vya uhai wa binaadamu. Vilevile historia inathibitisha kwamba wamisri walitumia asali kutibu magonjwa mbalimbali. Miaka ya hivi karibuni, matokeo ya tafiti za kisayansi zimebaini
kwamba licha ya asali kutumika kwa chakula na tiba dhidi ya magonjwa mbalimbali hasa yale sugu, uwezo wa kuzuia vitu visiharibike (antimicrobial properties) pia huweza kutumika kama chakula badala ya sukari.

• NTA : Ni zao la pili litokanalo na nyuki. Nta ni ute unaotolewa na nyuki wachanga unaochanganyika na vitu vingine ili kutengeneza masega ya nyuki. Unapoyeyusha masega na kuyachuja, nta hubaki na binaadamu huitumia kwa shughuli mbalimbali kama vile kutengeneza mishumaa, vipodozi vya akina mama, viwanda vya nguo kuimarisha nyuzi, na mambo mengine mengi ya kisasa.

• GUNDI : Gundi ya nyuki hutumika kusiliba mzinga wao na kuziba mianya ili kuzuia maji na vijidudu vidogo vyenye madhara ambavyo hupatikana kwenye mimea mbalimbali. Binaadamu huitumia gundi hiyo kuzuia mazaliano ya bakteria na fangasi ambavyo ni hatari kwa maisha ya binaadamu mwenyewe, mifugo na mazao yake.

• SUMU : Nyuki huitumia sumu hii kushambulia maadui wanaoingia kwenye viota vyao. Sumu hujulikana kitaalamu kama Bee venom ambayo hutengenezwa kwenye tezi za nyuki vibarua kwa ajili ya kujilinda wakiwa nje au ndani ya kiota. Binaadamu baada ya kugundua uwezo wa kuangamiza chembechembe za damu(red and white carpulcels) wakatafiti zaidi na kugundua kuwa huponyesha yabisi (rheumatism) na kutibu donda ndugu.

PITIA
JINSI YA KUJITENGENEZA CHAKULA CHA KUKU NYUMBANI KWA AJILI YA KUONGEZA UZALISHAJI

• MAZIWA YA NYUKI : Huzalishwa na nyuki vibarua wachanga ambao hula asali na chavua nyingi ili kutengeneza chakula chenye virutubisho vingi ambacho kitaalamu hujulikana kama (royal jelly). Chakula hiki hulishwa mabuu wachanga ili waweze kukua haraka na malkia aweze kutaga mayai na asizeeke haraka. Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba wazee watumiapo chakula hiki huwafanya kuonekana bado vijana na huwaongezea nguvu za kiume (libido).

• CHAVUA : Hili ni zao lingine litokanalo na nyuki, kitaalamu hujulikana kama pollen. Zao hili hutumika kama protini kwa ajili ya kujenga mwili kwenye kundi la nyuki, na ni moja ya chakula kikubwa cha nyuki. Binaadamu baada ya kugundua virutubisho vilivyomo ndani ya chakula hiki walianza kukitumia kwenye lishe za wanyama na sasa hivi imetokea kuwa biashara nzuri na yenye faida. Vilevile tafiti mbalimbali za kisayansi zimethibitisha kwamba ili mimea yetu iweze kutoa mazao bora na mengi ni lazima mbegu zisafirishwe toka sehemu ya kiume (anthers) kwenda za
kike (stigma) na pale kutoka ua moja kwenda ua jingine kwa namna ileile (Cross pollination). Kazi hii hufanywa vizuri zaidi na nyuki kuliko viumbe vingine vyote ulimwenguni. Hii ina maana kwamba ukitaka kufanikiwa kwenye kilimo cha mazao yako basi ni vema pawepo na nyuki karibu waweze kufanya kazi ya kuchavusha mimea yako.

Hivyo kutokana na faida mbalimbali zitokanazo na asali kwa maisha na maendeleo ya binaadamu, tunashauriwa kujikita kikamilifu katika ufugaji wa nyuki na kwa kutumia mbinu za kisasa ambazo tunaweza kuzipata kutoka kwa maafisa wa maliasili ambao wanapatikana sehemu zote nchini.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO

                                               UTANGULIZI Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita

Read More »

Kilimo cha Tangawizi

Kilimo cha tangawizi kimekuwa kikiwapa unafuu wakulima wa sehemu nyingi hapa nchini hasa katika mkoa wa Kilimanjaro katika wilaya ya same Tukisema kuna mikoa iliyo

Read More »

KILIMO CHA BAMIA

 BAMIA Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »