FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI

FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI
FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI

FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI : Samadi ni aina ya mbolea ambayo hutokana na vinyesi vya wanyama mbalimbali kama ng’ombe, kuku, mbuzi, kondoo na wengine. Hii ni miongoni mwa mbolea ambazo wakulima wengi wanaweza kumudu kirahisi.

Vilevile mbolea zingine ambazo wakulima wanaweza kuzipata kwa urahisi ni masalio ya mimea shambani (mabiwi). Mfano wa masalio hayo ni kama mabua ya mtama, mahindi na mimea ya jamii ya kunde au kitaalamu hujulikana kama (leguminas). Masalio haya yakishaoza hurutubisha udongo kwa kurejesha chumvichumvi za madini zilizokuwa zimechukuliwa na mimea wakati inastawi.

Hata hivyo mbolea yenye manufaa zaidi ni samadi, kwani wataalamu wanakadiria kuwa tani moja ya vinyesi vya fahali (madume ya ng’ombe) huwa na thamani karibu kilo 6.3 za chumvichumvi za nitrates; tani moja ya samadi ya vinyesi vya ng’ombe majike huwa na kilo 5.1 za chumvi za nitrates.

Mbolea zinazotokana na masalio ya mimea kwa mfano, mabua ya mahindi tani moja hutoa mbolea inayoweza kurejesha ardhini karibu kilo 4.0 za chumvi za nitrates.

Hivyo samadi yenye mchanganyiko wa vinyesi vya ng’ombe majike na madume wanaofugwa kwa pamoja (wanaolala katika zizi moja) huwa na thamani kubwa.

Ili upate kustawi na kutoa mavuno mengi na bora, mimea huhitaji chumvichumvi za madini ya nitrates, phosphate na potash pamoja na kiasi kidogo sana cha chumvi za nitrates, phosphate na potash pamoja na madini ya boron, copper, manganese, zinc na nyinginezo.

Kwa hiyo rutuba ya udongo huwa inategemea sana kiasi cha chumvichumvi zilizomo udongoni.

Ubora wa samadi hukadiriwa pia kwa kiasi cha chumvi za madini zinazopatikana mathalani ng’ombe 50 wanaweza kutoa karibu tani 600 za samadi kila mwaka. Kiasi hiki cha samadi kinaweza kurejesha ardhini karibu kilo 3048 za chumvichumvi za nitrates, kilo 544 za phosphate na kilo 2722 za Potash, pamoja na kiasi kidogo cha Boron, Copper, Manganese na Zinc.

PITIA
FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI

Wakulima au wafugaji wengi hufuga ng’ombe hata zaidi ya 50, lakini kwa wastani wengi huwa na idadi hiyo kama ni wastani wa ng’ombe ambao kila mkulima anaweza kuwa nao.

Mbolea yenye kilo 3048 za nitrates, kilo 544 za phosphate na kilo 2722 za potash kwa uwiano huo haziwezi kutengenezwa kiwandani kwani itakuwa ghali sana kiasi kwamba hakuna mkulima anaweza kununua.

Samadi kiasi hicho italeta manufaa mengi kwani licha ya kuongeza rutuba ardhini vilevile itaubadili udongo uwe katika hali nzuri zaidi kwa kustawisha mimea.

Kadhalika samadi unaufanya udongo ushikamane kwa nguvu zaidi hata usiweze kupeperushwa na upepo au kumomonyolewa na maji ya mvua.

MATUMIZI YA MBOLEA SHAMBANI
MATUMIZI YA MBOLEA SHAMBANI

Manufaa mengine ya mbolea ya samadi ni kuwa inaufanya udongo kuwa katika hali nzuri ya kuweza kuyashikilia maji au unyevu kwa muda mrefu.

Minyoo waishio udongoni ambao husababisha kuwepo nafasi kwa ajili ya hewa kupenya kwa urahisi na vijidudu vya bakteria ambavyo huozesha mbolea na kubadili hewa kuwa katika hali ya chumvichumvi zinazotumiwa na mimea, hupata mazingira mazuri kwa maisha yao katika udongo uliotiwa samadi.

Wataalamu wanasema kuwa ubora wa samadi inategemea jinsi ilivyokuwa imetunzwa zizini au kibandani kwani chumvi nyingi hasa zile za nitrates huwa zinapotea kwa urahisi kwa maji ya mvua, kutokana na kitendo chake cha kuyeyuka mara tu zinapolowa maji.

Ili tuendelee kuwa na thamadi kubwa ni muhimu zizi liwe na paa lisilovuja kusudi maji ya mvua yasilowanishe, la sivyo ng’ombe wafugwe katika vibanda.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO CHA UYOGA

Kwa kuwa #uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za #kuoteshea, urahisi wa

Read More »

SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO

SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO KUTOA KINGA KWA KUKU INGAWA WAMECHANJWA : Uzoefu umeonyesha kuwa wafugaji wengi wa kuku wa kisasa(Commercial Chicken)

Read More »
UFUGAJI WA NG'OMBE

UFUGAJI WA KISASA WA NG’OMBE

UTANGULIZI Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi.  Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe

Read More »

KILIMO BORA CHA UFUTA

Ufuta (sesamum indicum)ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »