FANYA YAFUATAYO KUANZISHA MRADI WA KUFUGA KUKU

Tanzania ni nchi yenye walaji wa nyama wengi na kuku huliwa kwa kiasi kikubwa sana. Hata kama bei zinapanda, ulaji unaendelea kukua. Matokeo yake ni kwamba kufuga kuku inaweza ikawa biashara yenye faida kubwa kwako kwa kuwa yanahitajika kwa wingi.

Kwa nini ufugaji wa kuku inafaida sana?

Kuku haina madhara mengi ya kiafya kama nyama ya ng’ombe na watu wengi wanazidi kutambua hilo Kuku wanakua kwa kasi kwa hiyo unaweza ukapata mapato makubwa kwa kipindi kifupi.

Kuku hailiwi nyumbani tu lakini pia kwenye migahawa, baa, hoteli na huduma zingine mbalimbali za chakula.

Kwa hiyo kama una nia ya kuanzisha biashara ya kufuga kuku, inabidi uchukue hatua zifuatayo:

1. Chagua aina ya kuku.

Kuna aina nyingi ya kuku, zikiwemo:

Kuku wa kienyeji
Bata
Bata Mzinga
Kanga
Bata Bukini
Tombo

Kwa sasa, tutaweka maelezo yetu kwa Kuku wa Kienyeji.

2. Amua unataka kufuga kuku kwa malengo gani ya kibiashara

Unaweza kufuka kuku kwa ajili ya biashara nyingi, zikiwemo:

• Kuku wa kuuza
• Kuku wa mayai
• Kuzalisha nyama ya kuku ya kuuza
• Kuzalisha chakula ya kuku ya kuuza
• Kuzalisha nyama na mayai ya kuku ya kisasa.

PITIA
UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU

Fanya maamuzi kwa kuangalia kiasi cha pesa ulionayo kuanzisha biashara pamoja mahitaji ya eneo yako.

Ni muhimu sana kufanya utafiti wako (uliza wafugaji wengine wa kuku) kujua ni aina gani ya ufugaji wa kuku utakaokuletea faida zaidi pamoja na gharama za kuanzia.

Kwa hapa, sisi tunalenga ufugaji kwa ajili ya kuzalisha mayai na nyama.

3. Una pesa ya kutosha?

Ukubwa wa shamba lako la kuku litategemea mtaji wako. Kwa ujumla:

• Shamba ndogo itahitaji mtaji wa TZS 1.5m – TZS 3m.
• Shamba ya saizi ya kati itahitaji mtaji wa TZS 4m – TZS 10m.
• Shamba kubwa itahitaji mtaji wa TZS 20m au zaidi

4. Shamba yako itakuwa maeneo gani?

Ukiwa unachagua eneo ya kuweka shamba lako, zingatia yafuatayo

• Bei ya kiwanja utakiweza?
• Gharama za kusafirisisha mayai na nyama ni za chini? Iko karibu na soko lako na wanunuaji?
• Watu wengi wanaishi kwenye hiyo eneo? Hii inaweza ikawa tatizo ukizingatia harufu litakalo kuwa linatoka shambani

Kuna usalama?
• Badala ya kutafuta kiwanja kipya, watu wengi wanafunga kuku kwenye eneo lao la nyumbani. Hii inapunguza gharama ila kabla ya kufanya hivi, kumbuka kufikiria majirani pamoja na kama kuna kanununi za kufuata.

5. Utatumia mfumo gani kwenye kibanda cha kuku?

Jinsi utakavyo wapanga kuku wako kwenye kibanda chao kitachangia faida yako kwa sana.

Kuwaachia huru-Mfumo huu umetumika tangu biashara ya kufuga kuku ulianza. Inawaachia kuku watembee wanavyopenda, ila kwa kuwaachia hivi inaweza ikawa na madhara yake, kama:

• Mahasimu wanaweza wakawaumiza
• Watu wanaweza wakawaiba
• Kuku wanaweza wakapotea
• Magonjwa yanaweza kusambaa
• Ni ngumu zaidi kufuatilia ukuwaji wao

PITIA
MAGONJWA MBALIMBALI YA NGURUWE NA TIBA

Ila, ni rahisi kuweka mfumo huu na haina gharama kubwa.
Mfumo wa Chicken Liter/Deep Litter: Hii ni mfumo maarufu kwa shamba ndogo na za ukubwa wa kati. Kuku wanwekwa kwenye eneo iliyozungukiwa na fensi au ukuta, alafu vipisi vidogo vidogo vya mbao vinasambazwa chini kutumiwa kama kitanda.

Mfumo huu unamsaidia mkulima huyu kusimamia idadi kubwa ya kuku. Ila, ubaya ni kwamba ni rahisi kwa magonjwa kuenea.

Mfumo wa Battery Cage: Kwa kawaida, mfumo huu unatumika kwenye mashamba makubwa ya ufugaji kuku ila ina gharama kubwa. Kuku wanaingizwa ndani ya ngome ya chuma, zikiwa na sehemu maalum za kula na kunywa maji. Pia, kuna nafasi maalum ya kutaga. Kwa kuwa idadi ya kuku wanaowekwa kwenye kila ngome sio kubwa, ni rahisi kujua kuku yupi anaumwa au hatagi.

6. Unahitaji vifaa gani?

Zaidi ya kuwajengea kibanda, kuku wako watahitaji vifaa vingine kama:

• Vifaa vya kunywa
• Vifaa vya kula
• Viota
• Taa
• Makreti
• Inkubeta
• Pechi
• Mfumo wakutoa takataka
• Trei ya mayai
• Hita
• Ngome

Tafuta vifaa vya kufuga kuku, hapa.

7. Utawalisha nini kuku wako?

Je, utanunua chackula chao au utiakitengeneza mwenyewe?
Kutengeza chakula cha kuku kinahitaji mtaji mkubwa zaidi, ila, kadri muda unavyoenda, gharama yake inakuja kuwa china ya kununua chakula chao kila mara ikihitajika. Pia, unaweza ukajiongezea mapato kwa kuwauzia wafugaji wengine wa kuku.

Mwisho wa siku maamuzi yatategemea na kufanya utafiti wa zote mbili na kujua gharama zake dhidi ya maslahi yako.

8. Inabidi umwajiri mtu?

Kama ufugaji wa kuku haitakuwa kazi yako ya kudumu, utahitaji kumwajiri mtu/watu kukusaidia na usiamamizi. Baadhi ya watu utakawahitaji ni:

PITIA
KILIMO BORA CHA CABBAGE

• Msimamizi wa biashara kwa ujumla
• Mhasibu
• Msimamizi wa kuku
• Mlinzi

Mtu wa kutangaza biashara yako – we unaweza kufanya kazi hii. Itabidi utafute namna ya kutangaza biashara yako kwenye intaneti kwa kupitia

orodha za biashara kama iliyopo ZoomTanzania , kwenye mitandao ya kijamii, kwa kuchapisha vipeperushi n.k

9. Chanjo za kuku na upimaji wa afya mara kwa mara.


Kadri biashari yako itakavyokuwa, ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa mganga wa mifugo na kuchanja kuku wako kuzuia magonjwa kusambaa.

Kumbuka, afya ni muhimu kuliko bei ya kuku wako. Ila, weka bei inayoeleweka.

Biashara inayolipa


Kufuga kuku inahitaji subira na kujitolea ila, faida zikianza kuingia utafurahi sana!

Tafuta kila kitu unachokihataji kuanza kufuga kuku hapa.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »