IJUE TANGAWIZI NA FAIDA ZAKE

IJUE TANGAWIZI NA FAIDA ZAKE
Tangawizi ni zao ambalo hustawi sehemu mbalimbali duniani na hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali, dawa kwa tiba ya magonjwa ya binadamu na wanyama na pia kiambato muhimu kwenye vinywaji mbalimbali. Zao hili lilianza kulimwa katika nchi za Asia, Afrika Magharibi na katika visiwa vya Caribbean. Tangawizi ni zao linalotumiwa na walaji wote ulimwenguni, hii inatokana na baadhi ya watu kutambua faida zake ki-lishe na kitiba.

FAIDA ZA TANGAWIZI KWA LISHE

Tangawizi ikichemshwa na maji na kuongezwa sukari hutoa kinywaji ambacho ni kitamu na chenye ladha nzuri sana. Baadhi ya watumiaji
hupendelea kuongeza asali, vipande vya machungwa au limao ili kuweza kupata ladha nzuri zaidi. Vilevile hutumika katika utayarishwaji wa vinywaji vingine viwandani kama soda, chai, kahawa nakadhalika.

Hutumika kama kiungo muhimu cha kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali kama biskuti, mikate, keki, nyama na vingine vingi.

FAIDA ZA TANGAWIZI KWA TIBA

Utomvu unaotokana na zao hili umeonekana kusaidia sana katika kuondosha maumivu ya sehemu mbalimbali za viungo vya binaadamu. Unapochua utomvu huu mara mbili kwa siku sehemu zenye maumivu huweza kuondosha maumivu mbalimbali haraka, kwa mfano maumivu ya misuli, magoti, maumivu ya kichwa nakadhalika.

Hukinga na kutibu kuwashwa na kukereketwa koo (Sore throat) na ugonjwa wa mafua ya sehemu ya juu (Upper respiratory truck infection).

Tafiti mbalimbali ulimwenguni zimethibitisha tangawizi kuwa na uwezo mkubwa katika kuondosha homa za kutapika na kizunguzungu (motion fever) kwa wasafiri wa vyombo mbalimbali baharini na nchi kavu.

Pia huondosha kichefuchefu na kutapika kwa akinamama wajawazito na hata kwa wagonjwa wanaofanyiwa operesheni.

Inasadikika kijiko 1 cha tangawizi iliyosagwa kinatosha kumuondolea kichefuchefu na kutapika mgonjwa baada ya kufanyika operesheni.

Tangawizi pia imegundulika kupunguza kwa kiasi kikubwa lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa hiyo, hivyo kuzuia kutokea madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu jambo ambalo linazaweza kusababisha maradhi ya moyo na kupooza kwa viungo vya mwili.

Tangawizi pia imegundulika kuwa dawa muhimu kupunguza au kuondosha kabisa maumivu wanawapata kinamama wengi wakati wa hedhi.

PITIA
Teknolojia kuwasaidia wakulima wa miwa

Vilevile tangawizi imedhihirisha kuwa na uwezo mkubwa kuponya haraka maumivu makali ya tumbo yanayowapata mara kwa mara watoto wadogo.

[mc4wp_form id=”665″]

Katika baadhi ya nchi tangawizi inatumika katika kuhifadhi chakula kwa muda mrefu, hii inatokana na ukweli kwamba ina uwezo mkubwa wa kuua aina nyingi za bakteria kama vile E.coli, Salmonella na wengine wengi ambao huharibu vyakula vyetu.

Tangawizi hukiamasisha kimengenyo mwilini kilichopo mwetu kiitwacho Gastric juice kufanya kazi ipasavyo na hivyo husaidia kuzalisha joto la mwili ambalo huwapa nafuu wagonjwa wengi wa mafua na maumivu ya tumbo.

Watu wengi ulimwenguni hutumia mmea huu kama dawa ya kuondoa harufu mbaya kinywani.

Hutumika katika utengenezaji wa siki (vinegar) ambayo huhamasisha hamu ya kula.

Nchini China wanawake wengi wajawazito hutumia juisi ya tangawizi ili kujiepusha na adha ya kutapika mara kwa mara (Morning sickness).

Tangawizi pia hutumika kama dawa ya kushusha joto la mwili na homa za mara kwa mara zinazosababishwa na malaria au mashambulizi ya bakteria na fangasi ambayo mara nyingi huchochea joto la mwili kupanda zaidi ya kiwango cha kawaida.

Pia husaidia kushusha presha ya damu mwilini (hypertension) kwa watu wanaosumbuliwa na presha ya kupanda.

Tangawizi pia hutumika kupunguza maumivu yanayosababishwa na matatizo ya mawe kwenye figo, vilevile hupunguza kibofu cha mkojo iwapo itatumika kuchuliwa kwa nje sehemu za mwili zilizo karibu na kiungo hiki.

Virutubisho vilivyomo kwenye zao hili pia huhamasisha utendaji mzima wa vimengenyo mbalimbali katika usagaji wa chakula mwilini na pia kutuongezea hamu ya kula chakula.

Lakini itabidi izingatiwe kwamba isitumiwe kwa watoto chini ya miaka 2, itumiwe kwa watoto zaidi ya umri huo kuwaondolea adha kama vile za kuumwa vichwa, kichefuchefu na kuumwa matumbo. Dozi ya tangawizi itolewe kulingana na uzito wa mtoto husika. Dozi nyingi za dawa za mitishamba hutolewa kwa kulinganishwa na na dozi ya mtu mzima wa kilo 70, hivyo mtoto wa kilo 20 hadi 25 hupatiwa 1/3 ya dozi ya mtu mzima. Kwa ujumla kwa dozi ya mtu mzima huwa isizidi gramu 4 kila siku.

PITIA
Faida zitokanazo na Mapapai

Ni vyema tukajenga mazoea ya kutumia dawa zitokanazo na mimea kama tangawizi kwa ajili ya kinga na tiba mbalimbali za miili yetu kwa sababu licha ya kuwa zinapatikana kirahisi pia si ghali na hazina madhara yeyote kwa afya zetu kama zilivyo dawa nyingi za viwandani.

CHAI YA TANGAWIZI
CHAI YA TANGAWIZI
[mc4wp_form id=”665″]

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

CORONA VIRUS EDUCATIONAL POST

Naomba twende polepole Vyanzo vya vifo duniani na idadi (WHO, 2019) Heart diseases – mil 9.43Stroke – mil 5.73COPD – mil 3.04Pumu – mil 2.96Alzheimer’s

Read More »

Ujue Muhogo

MUHOGO ni moja ya mazao ya mizizi na lenye umuhimu katika mazao makuu ya chakula baada ya zao la mahindi nchini Tanzania. Umuhimu wa zao

Read More »

UFAHAMU UGONJWA WA KUKU WA KUVIMBA MACHO

Chanzo cha maambukizi •Maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na kwenye vimelea•Kupitia mfumo wa hewa kutoka kuku wagonjwa•Kupitia mayai, hivyo maambukizi huendelea kutoka kizazi

Read More »
Udongo

Njia sahihi za kilimo bora

Njia sahihi za kilimo chochote kile ambacho unatamani sana kukifanya zipo kanuni na taratibu zake za kuweza kufanya hivyo. Baadhi ya mambo ya msingi ambayo

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »