Kilimo Safi cha Mahindi

MAHINDI ni nafaka ambayo ni chakula muhimu sana na huzalishwa na kutumika kwa wingi katika mataifa ya Afrika yaliyomo kusini mwa jangwa la Sahara.

Ni chakula cha matumizi ya nyumbani kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo muhimu cha madini na huongeza nguvu mwilini, protini, madini ya chuma (iron) vitamini na madini mengine asilia.

Jamii nyingi za kiafrika hutumia mahindi kwa njia mbalimbali kutengeneza vyakula na vinywaji kama vile uji, ugali na pombe.

Wakati mwingine pia mahindi huchomwa na kuliwa. Thamani ya mmea huu ni kubwa mno kwani Kila sehemu yake ina thamani fulani kiuchumi mfano : punje, majani, shina na magunzi huweza kutoa kiasi kikubwa cha bidhaa nyinginezo zilizo chakula na zisizokuwa chakula.

Vile vile mahindi ni chakula muhimu cha mifugo (ng’ombe) na huhifadhiwa kama silage. Pia mabaki ya mimea ya nafaka hii pia hutumika viwandani kutengeneza wanga na mafuta.

Mahitaji ya mahindi katika hali ya hewa, udongo na Mahindi ni mimea ambayo hustahimili mabadiliko mengi ya hali ya hewa na humea katika maeneo mengi tofauti.

Zipo aina nyingi za mahindi yakitofautiana katika muda wa kukomaa. Mahindi huwa na ustahimilivu mkubwa katika kukabili viwango vya joto na hali ya hewa.

Mahindi ni mmea ambao hustawi katika ya joto ambako unyevu yenye unyevu wa kutosha.

Mmea huu unahitaji kiwango cha joto cha kila siku cha nyuzi joto 20º ili ili uweze kuumea vyema.

Joto la juu sana kwa mazao mazuri ni kama nyuzi joto 30º. Hupandwa sana katika sehemu zilizo katika kimo cha mita 3000 kutoka usawa wa bahari hadi kwenye ukanda wa pwani. mahindi yaweza kupandwa kama chakula cha mifugo pia

KUTAYARISHA SHAMBA

 • Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.
 • Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
 • Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.

FAIDA ZA KUANDAA SHAMBA MAPEMA. 

 • Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
 • Masalia yatakayofunikwa chini ya udongoi huoza mapema.
 • Hupunguza magugu.
 • Hupunguza wadudu waharibifu

KUPANDA.

Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua hayatabiriki,Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.

 1. Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.
 2. Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
 3. Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
 4. Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni. Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa.
PITIA
KILIMO BORA CHA ULEZI

Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua. Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu,panya,ndege na wanyama wengineo.

FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA

 • Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
 • Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
 • Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.

 KUCHAGUA MBEGU BORA

 1. Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
 2. Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
 3. Huzaa mazao mengi.
 4. Hustahimili magonjwa.

AINA ZA MBEGU.

 • Mbegu aina ya chotara(hybrid)
 • Mbegu aina ya OPV (Open Polinated Variety)
 • Aina ya ndugu moja(synthetic)
 • Mbegu aina ya composite. Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80au tani 5 – 7.5 kwa hekta moja au gunia 20-35kwa hekari.

MAPENDEKEZO YA MBEGUZA KUPANDA

Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa SEEDCO ,PANNAR, PIONEER, KITALE kutoka KENYA n.k Ni vyema kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo.

KUPANDA

Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani uzoefu unaonyesha wakulima wengi hawapati kiwango kinachotakiwa kutokana na upungufu wa idadi ya miche katika eneo husika. Na athari zake ni:-

 • Mazao hupungua.
 • Mmea huangushwa na upepo
 • Mabua mengi hayazai.

Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababisha mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu na kupanda kwa wakati na kwa umakini.

KIASI CHA KUPANDA

Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali na kiasi cha 10kg hutosha kupanda ekari moja.

Nafasi za kupanda.

75cm x 30cm mche mmoja

75cm x 60cm miche mawili

90cm x 45cm miche miwili

Mahindi huwa yanaathirika na ukosefu wa unyevu wakati wa kutoa maua na matunda. Pia yanahitaji maji ya kutosha wakati wa kupanda.

Katika nchi za joto jingi (tropiki), mahindi hufanya vyema katika mvua ya kiwango cha milimita 600 hadi 900 wakati wa kukua. Mahindi yanaweza kukuzwa kwenye aina nyingi za udongo lakini hukua vyema zaidi katika mchanga, usiotuamisha maji mengi, ulio na hewa ya kutosha na ulio na rutuba na madini ya kutosha.

Kuwepo kwa mazao mengi ya mahindi kunapelekea kunyonywa sana kwa madini kwenye udongo. Mahindi yaweza kukuzwa katika udongo ulio na hali ya mchanga na (PH) kutoka 5 hadi 8 ingawa 5.5 hadi 7 ndio mwafaka.

Mahindi yako katika kikundi cha mimea kinachoaminika kuathirika na hali ya chumvi katika maji na udongo. Kwa vile mimea ambayo ni michanga huwacha sehemu kubwa bila kuzingirwa na ardhi, mmomonyko wa udongo na kupoteza maji hutokea sana sana hivyo basi ni bora umakini uzingatiwe katika uhifadhi wa udongo na maji kwa kuweka matandazo (mulching).

PITIA
Kilimo bora cha Ndizi

MATUMIZI YA MBOLEA
Mahindi hustawi zaidi yakiwekwa mbolea, iwapo mambo mengine yanayosaidia katika kukua pia yapo kwa kiwango kinachostahili. Mbolea inayotumiwa na wakulima wadogo mara yingi huwa haitoshi. Mahindi ya kiwango cha juu yaweza tu kufikia kiwango cha juu cha Uzalishaji iwapo yatapewa lishe na madini ya kutosha. Mahindi ya tani 2 kwa hekta na tani 5 kwa hekta hutumia karibu kilo 60 N, kilo 10 za P205 na kilo 70K20 kutoka katika udongo. Mahindi hunyonya Nitrogen pole pole katika miezi ya kwanza baada ya kupanda, lakini huongezeka hadi kiwango cha juu kabisa wakati wa kutoa maua na kukuza tunda (gunzi). Mahindi huhitaji nitrogen kwa kiwango cha juu na ukosefu huwa ndio kizingiti. Kiwango cha juu cha nitrogen kinahitajika mara tatu; kwanza wakati wa kupanda, pili, wakati ambapo mmea umefikia sentimita 50 za urefu na tatu, wakati matunda ya mahindi yanaanza kutoa zile nyuzi nyuzi nyororo (silking).

Udongo mwingi huwa na madini ya phosphorous (P205) na potassium (K20) lakini sio kiwango kinachotosheleza mahitaji haswa ya mbegu za mahindi zinapochipua. Nyunyuzia P205 karibu na mbegu ili ziote kwa haraka. K20 hutumika kwa kiwango kikubwa lakini hitaji la mimea hubainika baada ya upimaji wa hali ya udongo kujua kiasi cha mahitaji (soil test).

DALILI ZA UPUNGUFU WA MBOLEA
Ukosefu wa K20 husababisha ncha za majani kuwa na rangi ya njano na kuunda gunzi (cob) lisilo na punje hadi juu. Ukosefu wa P205 hufanya matawi kuwa na rangi ya samawati na mbegu zisizo laini. Dalili za ukosefu wa nitrogen ni majani ya rangi ya manjano na mimea dhaifu mifupi. Phosphate haifyonzwi haraka na mahindi na pia udongo mwingi wa nchi za joto hukosa madini hayo ya phosphate. Inashauriwa unyunyuzie mbolea ya kiasili kama samadi kabla ya kulima ili uboreshe hali ya udongo na kuongezea madini.

Katika ukulima wa kiasili, (organic farming, Nitrogen (N) hutiwa kwenye udongo kupitia kwa upandaji wa mimea ya jamii ya mikunde (legumes) ambayo hutoa nitrogen katika hewa, Hata hivyo mapendekezo ya kimbolea yaliyo katika misingi ya uchunguzi wa udongo hutoa nafasi nzuri ya kupata kiasi kizuri cha mbolea bila kuweka kiwango cha chini au juu. Omba msaada kutoka kwa mafisa ugani wa kilimo waliyo katika eneo lako.
Katika maeneo yanayo tegemea mvua kukuza mahindi, panda mbegu wakati wa mvua ya kwanza. Hii itaruhusu mizizi kunyonya madini yaliyotengenzwa na bakteria katika udongo. Maji yaliyosimama huyeyusha na kuondoa madini ya nitrogen kutoka katika udongo na kusababisha ukosefu wa Nitrogen.

PITIA
MIGOMBA - KANUNI ZA KILIMO BORA

KUDHIBITI MAGUGU
Udhibiti wa magugu ni muhimu sana. Katika wiki 4 hadi 6 za mbele baada ya kumea, mahindi huathiriwa sana na magugu.

Ni lazima mahindi yapandwe mara moja baada ya kutayarisha shamba. Unaweza kulima katikati ya laini za mahindi ili udhibiti magugu. Nchini Tanzania, kupalilia mara mbili kunahitajika kwa aina nyingi za mahindi, ingawa kupalilia kwa mara ya tatu kutahitajika kwa aina ambazo zinahitaji miezi 6 hadi 8 kukomaa. Kupalilia kwa mikono kunahitaji siku 15 kwa hekta la mikono (power tiller) ni masaa mawili mpaka matatu kwa ekari.

UHUSIANO WA NIPE NIKUPE
Desmodium (desmodium uncinatum) nyasi ya Molasses (melinis minutifolia) zikipandwa kati kati ya laini za mahindi huzuia wadudu kama stalk borers moths.

Mimea hii hutoa kemikali ambazo huwafukuza wadudu aina stem borers’ moths. Zaidi ya hayo Desmodium huzui gugu haribifu,witchweed striga hermonthica. Napier grass (pennisetum purpureum) na Sudan grass (sorghum vulgare sodanese) ni mimea mizuri sana inayonasa wadudu aina ya stem borers. Napier grass ina njia yake madhubuti ya kujikinga dhidi ya wadudu wanaotoboa mmea kwa kutoa utomvu kutoka kwenye shina, ambayo huzuia wadudu kufyoza mmea na kusababisha uharibifu. Nyasi hizi pia huvutia adui wa stem borers kama mchwa, earwigs na buibui. Nyasi aina ya Sudan pia husaidia maadui asilia, kama nyigu (parasitic wasp)

Mahindi huweka kivuli kwenye mimea ya mboga mboga ikipandwa safu moja katikati ya mboga kwenye maeneo yaliyo na jua kali.

Hii huongeza mazao ya mboga zilizopandwa hivi. na mimea jamii ya mikunde huongeza nitrogen kwenye udongo ambayo huitajika zaidi katika ukuaji wa mahindi pia hupunguza wadudu aina ya (leafhoppers, leafbeatles, stalk borers na fall army worm), upandaji wa mimea jamii ya mikunde ufanyike mara baada ya palizi ya kwanza.

UVUNAJI
Uvunaji hufanyika kwa kutumia mikono kwa mashamba madogo na mashine (combine harvester) hutumika kwa ajili ya mashamba makubwa, Zao la wastani la mahindi ulimwenguni mnamo mwaka 2000 lilikuwa kilogramu 4255 kwa kila hekta. Zao la wastani nchini Marekani ilikuwa kilo 8600 kila hekta, huku mataifa yaliyo chini ya jangwa la Sahara la Afrika yakivuna kilo 1316 kwa kila hekta ya shamba. Zao la wastani katika taifa la Tanzania kati ya mwaka 2001-2005 lilikuwa kati ya gunia 15-19 kwa hekta (sawa na kilo 1350-1750) Ukilima kwa kuzingatia ukulima wa kisasa na kanuni zake kwa Tanzania utavuna kilo 5000 kwa hecta (ukanda wa pwani) na kilo 7500 kwa nyanda za juu kama Iringa, Mbeya, Ruvuma, Arusha n.k

Hakikisha baada ya kuvuna mazao yako yanahifadhiwa sehemu kavu baada ya kuyakausha vizuri ili kuepuka mahindi kuvunda.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo bora cha Ndizi

Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa

Read More »

KILIMO BORA CHA ALIZETI

ALIZETI-SUNFLOWER (Helianthus annus) UTANGULIZI Alizeti ni zao mojawapo kati ya mazao muhimu yanayotoa mbegu za mafuta. Hutoa mafuta kati ya asilimia 35– 45 na mashudu

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »