JINSI YA KUDHIBITI VIWAVIJESHI KWA KUTUMIA VIUTILIFU.

Kiwavijeshi Vamizi ajulikanae kama Fall Armyworm au kwa jina la kitaalamu “Spodoptera frugipedra” asili yake ni Bara la America. Mdudu alionekana kwa mara ya kwanza katika nchi za Africa Magharibi (Nigeria) mwishoni mwa mwaka 2016.
Hadi mwezi February 2017, kiwavijeshi huyu alikuwa ameshavamia nchi za Afrika Kusini, Kati na Mashariki zikiwemo Zimbabwe, Msumbiji, Zambia, Congo na RwandaHapa nchini kiwavijeshi vamizi aliripotiwa kwa mara ya kwanza katika wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa mwezi Machi 2017.
Hadi mwezi Disemba 2017 kiwavijeshi huyu alisharipotiwa kwenye mikoa zaidi ya 15 Maarufu kwa kilimo cha mahindi ikiwemo Mbeya, Shinyanga,Ruvuma, Iringa, Geita, Manyara,Arusha, Kilimanjaro, Morogoro,Tanga, Kigoma, Kagera,Mwanza,Pwani na Lindi.Udhibiti wa kutumia Viuatilifu

  • Kagua shamba kubaini uwepo wa lava wa Kiwavijeshi Vamizi kwenye shamba
  • Tumia viatilifu vilivyosajiliwa Tanzania kwa kufuata maelekezo kwenye kibandiko kilichopo kwenye kifungashio.
  • Kiuatilifu kipulizwe wakati wa asubuhi au jioni kwenye eneo lililoshambuliwa na Kiwavijeshi Vamizi
  • Kwa ushauri unaweza kutumia kiuatilifu chenye usajili wa jina la DUDUBA EC, Belt 480SC, Emamectin benzoate au Mupacron 50EC, DUDUALL, PROFECRON n.k
  • Matumizi ya kiuatilifu iwe ni hatua ya mwisho baada ya mbinu nyingine kushindwa
PITIA
Kilimo cha bamia sehemu ya pili (02)

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo bora cha nyanya -Tz

Utangulizi Nyanya ni zao la mboga linalolimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Nyanya ni aina

Read More »

Kilimo bora cha Mtama

UTANGULIZI Mtama ni miongoni mwa mazao ya nafaka yanayolimwa kwa wingi nchini na duniani kote. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mtama

Read More »

KILIMO BORA CHA KARANGA

UTANGULIZI Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. hulimwa lengo kubwa likiwa ni uzalishaji wa mafuta, chakula na malisho kwa ajili ya mifugo. Katika Tanzania

Read More »

ZIJUE FAIDA ZA KULIMA MAPAPAI

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papayaPapai ni moja ya matunda ambayo huchukua

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »