JINSI YA KUJITENGENEZA CHAKULA CHA KUKU NYUMBANI KWA AJILI YA KUONGEZA UZALISHAJI

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......
Kuku wa Kienyeji wa Mayai

Kutokana na kuongezeka kwa gharama za chakula cha kuku iwewawia vigumu wafugaji wa kuku kupata faida kupitia ufugaji wa kuku. N akwa jinsi utengenezaji wa chakula cha kuku hasa hasa kuku wa kisasa kama broiler na layers kwa wafugaji ni ngumu leo nakuja na somo jepesi la jinsi ya kutengeneza chakula kwa kuku chotara (hybrid) or kuku wa kienyeji wanaofugwa ndani ya banda kwa kutumia Pearson Square method nah ii yote yawezekana kama mkulima atakuwa na raw materials zinazohitajika katika utengenezaji wa chakula.

Njia HII ya pearson square mara nyingi ina base sana katika Digestable crude protein (DCP) ya malighafi husika katika utengenezaji wa chakula. Na malighafi zinazotahitajika hapa ni kama vile Mahindi, mashudu ya pamba, mashudu ya alzeti, maharage ya soya na dagaa.

Jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku wa mayai (70kg) (chotara) unahitaji vifuatavyo;

34 kg Mahindi

12 kg Soya beans

8 kg Dagaa

10 kg pumba za mahindi

6 kg Chokaa (kwa ajili ya calcium)

Jinsi ya kutengeneza chakula(70kg) kwa ajili ya kuku wa nyama

Mahindi= 40 kg

Dagaa = 12 kg

Maharage ya soya = 14 kg

Chokaa = 4 kg

NB: Hakikisha unaongeza chumvi 250g katika kila mfuko wa 70kg wa chakula chako

Ndondoo muhimu ya jinsi ya kuwalisha kuku wako Nyumbani

· Kuku anaetaga mayai anahitaji kula angalau 130g za chakula kwa siku. Kumbuka kuwapa maji masafi muda wote.

· Kifaranga kimoja anahitaji 2.2 kg za chakula kwa wiki 8 (hivyo basi vifaranga 100 = 2.2 kg x 100=220 kg. Vifaranga wanahitaji kula muda wote na pia suala la maji ni muhimu kwao pia na unakumbushwa kuwapa mboga mboga baada ya mlo wao kuisha.

PITIA
Ujue Muhogo

Kuku mdogo anayekaribia kutaga anatakiwa kula 4.5 kg ya chakula kwa muda wa miezi miwili na nusu mpaka watakapoanza kutaga yai kwa mara ya kwanza. Baada ya hapo wanabadilishiwa chakula na kupewa chakula cha utagaji (layer diet).

· Malighafi zinazotakiwa katika utengenezaji wa chakula zinatakiwa zile za kiwango cha juu kabisa usitumie mahindi yenye uozo maana utafanya kuku wako kupata ugonjwa wa aflatoxins poisoning.

Ukitumia dagaa hakikisha ni wasafi na hawana mchanga ama shells wa aina yoyote.

· Na mwisho hakikisha chakula hicho unakichanganya vizuri kabisa ili kuleta uwiano au mchanganyo ulio sahihi.

Hitimisho

Kwa formular za Chakula za Kuku wa kisasa kama Broiler na Layer tunaweza wasiliana kwa namba zangu hapo chini na hakika zitakuongezea uzalishaji maradufu ya chakula cha kununua.

Imeandaliwa na Dr of Veterinary Medicine

Phone: 0712784472

theriogenology

Newton Deus

Newton Deus

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo