KAHAWA, ni zao kubwa la biashara, inachukua nafasi ya pili kwa kuingizia taifa fedha nyingi za kigeni baada ya zao la Tumbaku, wakulima wengi wanaofuata kanuni na mbinu za kitaalam wananufaika, wanaboresha maisha yao kupitia kilimo bora cha Kahawa.
Faines, Katelina na Jesta ni wanawake wajane wa familia moja ya marehemu Josta Mwanalubisya kutoka kijiji cha Shongo, ni wanachama wa kikundi cha Nkuyu katika kata ya Igale wilaya ya Mbeya kusini Magharibi mwa Tanzania
Kwa sasa sehemu kubwa ya maisha yao yanategemea Kahawa, shirika HRNS (Hanns R. Neumann Stiftung Africa linasaidia kuendeleza zao la Kahawa nchini Tanzania ili kuinua hali ya maisha ya wakulima na familia zao.
Ndio maana wanawake hao wanasema “ tunapata faida kuliko mara ya kwanza, kwa miti michache tunapata hadi zaidi ya kilo 300 za Kahawa, hii nikutokana na mbinu bora zilizotuongezea ujuzi wenye tija ya uzalishaji, tunazo jifunza kwa HRNS”
“Hakika kupitia Kahawa nyumba nzuri zimejengwa, watoto wanasoma pia nimenunua mashamba mengine kwa ajili ya mazao ya chakula, kwa sasa nina shauku ya kununua usafiri wangu hasa gari”, aliongea kwa furaha Katelina Josta.
Meneja wa mradi wa shirika la HRNS nyanda za juu kusini, Webster Miyanda amesema HRNS linaendelea na jitihada za utafiti wa hali ya hewa ya eneo la kilimo cha Kahawa ili kutafuta suluhisho la maji, kutoa vitendea kazi, elimu na mbinu chanya za kilimo kibiashara.
“Tunaendesha mafunzo kwa shirikisha wadau wengine kutoka kwenye mashirika tofauti yakiwemo TACRI, CMS, TCB ili kuwasiadia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”
Lazima watumie mbinu mpya kama kilimo hifadhi, kupanda miti ya kimvuli na mazao yanayofunika udongo ndani ya mashamba ya Kahawa, pia matumizi ya mbolea ya samadi au mboji na kupanda mimea inayoongeza viini lishe vya udongo ni muhimu ili kutunza Ardhi” Alisema Miyanda.
Edmond Zani ni meneja wa bodi ya Kahawa kanda ya nyanda za juu kusini, amesema kwa Tanzania ikiwa mche wa kahawa utatunzwa vizuri una uwezo wa kuzalisha hadi kilogram 8 za kahawa na takribani kaya 450,000 zinategemea kilimo cha zao hilo kama ajira yao.
Elizabeth Nyivambe na Debora Mwanyanje.
Elimisha Tujenge Jamii Imara.