KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI

 

KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI

KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI :

Moja kati mbinu ambazo zitakufanya uweze kulima kilimo chenye tija kujua kanuni ambazo zitakuzaidia kuweza kulima kilimo hicho, na kanunia hizo nitazieleze katika Makala haya. Mahindi ni zao muhimu linalo limwa katika maeneo ya kitropiki. Pia zao hili hulimwa katika udongo wenye uchachu pH 6-6.5. lakini pia hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa 2500.

KANUNI YA KWANZA – KUTAYARISHA SHAMBA MAPEMA

 • Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.
 • Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
 • Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.

FAIDA YA KUANDAA SHAMBA MAPEMA

 1. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
 2. Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
 3. Hupunguza magugu.
 4. Hupunguza wadudu waharibifu.

KANUNI YA PILI ; kujua wakati wa kupanda mbegu sahambani.

Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki, Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.

 1. Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.
 1. Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
 1. Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
 1. Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.

Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua.

PITIA
Kilimo Bora cha maharage

Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu, panya, ndege na wanyama wengineo.

FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA

 1. Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
 2. Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
 3. c) Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.

KANUNI YA TATU KUCHAGUA MBEGU BORA

Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.

 1. a) Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
 2. b) Huzaa mazao mengi.
 3. c) Hustahimili magonjwa.

AINA ZA MBEGU

 1. Mbegu aina ya chotara (hybrid)
 2. Aina ya ndugu moja (synthetic)
 3. Mbegu aina ya composite

Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja au umi kwa hekari.

MAPENDEKEZO YA MBEGU ZA KUPANDA

Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa

SIDCO ,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k Ni vyema

kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo

KANUNI YA NNE KUPANDA

Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikazidi

 1. Mazao hupungua.
 2. Mmea huangushwa na upepo
 3. Mabua mengi hayazai.

Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.

KIASI CHA KUPANDA

 1. Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu
 2. Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (Hii hutegemea na aina ya mbegu)

Nafasi za kupanda.

75cm x 30cm

75cm x 60cm

90cm x 25cm

90cm x 50cm

KANUNI YA TANO; KUTUMIA MBOLEA

Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwambolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.

PITIA
KILIMO BORA CHA KOROSHO (CASHEW NUT)

KUNA AINA MBILI KUU ZA MBOLEA

 1. Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na virutubisho vya kutosh ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani
 1. Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Pilipili

Pilipili   hoho  ni  moja  ya  mazao   ya  viungo  ambalo  hulimwa  kwa   wingi    Mikoa  ya   Arusha,  Kilimanjaro,  Tanga,  Morogoro, Mbeya  na   Iringa. Zao   hili   hutumika    kama 

Read More »

ZIFAHAMU AINA NNE ZA MTAMA

Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »