KANUNI NA ULIMAJI WA KILIMO BORA CHA ZAO LA MAHINDI.

Misingi na kanuni za kilimo bora.

Neno Msingi lina maana ya mwanzo wa kufanya shughuli yeyote inayokusudiwa ili kuweza
kufikia malengo, kwa hiyo katika kilimo ipo misingi muhimu ifuatayo:

Kuwa na mipango thabiti inayotekelezeka kabla ya kuanza kufanya kazi yeyote ya maendeleo ni
vyema kuweka mpango kazi ili iwe dira wakati wa utekelezaji. Hivyo wakulima wanatakiwa
waweke malengo yao ya kilimo kwa kuangalia usalama wa chakula na kipato

Mipango bora.

Ni mipango ambayo inamsaidia mkulima kupata chakula cha kutosha na fedha ili kuondokana na
umaskini.

Mipango inatakiwa iwe shirikishi kwa kuona kuwa wakulima wana shiriki katika kupanga,
kutekeleza, kufuatilia pamoja na kutathmini.

Kuchagua eneo linalofaa kwa kilimo.

Kwa kuwa kilimo ni kazi ya kisayansi, eneo linalofaa kwa kilimo

Udongo

liwe na rutuba, mteremko wa wastani, liwe sehemu inayopitika ili kurahisisha usafirishaji wa
mazao na pembejeo wakati wa uzalishaji.

Uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu.

Ni muhimu mkulima kujiwekea kumbukumbu za uzalishaji, mapato na faida ili kupima
mafanikio ya kazi yake.
Matumizi ya kanuni za kilimo bora.
Neno kanuni lina maana ya utaratibu wa kisanyansi uliofanyiwa majaribio kwa muda mrefu na
ambao umekubalika utumike wakati wa uzalishaji wa mazao.

Kanuni za kilimo bora

  • Kutayarisha shamba mapema Kwa kutifua.
  • Kupanda mbegu bora kwa nafasi inayostahili.
  • Kupunguzia miche na kubakiza inayoshauriwa
  • Palilia mapema-si zaidi ya wiki mbili baada ya kuota mazao..Plazi ziwe mbili au zaidi.
  • Weka mbolea ya kukuzia mara baada ya palizi.
  • Weka dawa ya kuua wadudu wa mimea.
  • Vuna mazao yako baada ya kukomaa vizuri.
  • Sindika mazao yako na kuyaweka kwenye mifuko inayoingiza hewa baada ya kuweka
  • Hifadhi mazao mahali pazuri pasipo vuja au kufikiwa na wanyama waharibifu.( Panya)
PITIA
KILIMO BORA CHA PAMBA

Zao la mahindi

Utangulizi:

Mahindi ni zao muhimu la chakula hapa nchini.Mbinu muhimu za uzalishaji wa zao hili ni kama
ifuatavyo.

Aina za mahindi.

Zipo aina mbali mbali za mahindi ambazo hustawi hapa wilayani nazo ni: TMV-1, Staha, Stuka,
kilima, kito na mahindi jamii ya chotara kama kitale, SC 513, 627, na 407

Utayarishaji wa shamba.

Chagua eneo lenye rutuba na anza kutayarisha shamba mapema. Utayarishaji hufanywa kwa
jembe la mkono au matrekta na ardhi hutifuliwa kiasi cha sm15-30 au kutumia matuta.

Upandaji na nafasi ya kupandia.

Mahindi hupandwa wakati wa mvua za masika au vuli. Mbegu hupandwa katika mashimo yenye
kina cha sm 5 na kufukia udongo vizuri.

Mbolea za kupandia hutumika ambazo ni SP, DSP, Minjingu fosfet na DAP kiasi cha kilo 30-40
kwa eka. Pia samadi hutumika kiasi cha tani 4-5 kwa eka.
Mahindi hupandwa kwa nafasi ya sm 90×30, sm75x60 na 60×30.
Ekari moja huhitaji mbegu kiasi cha kilo 8-10 na idadi ya mimea kwa eka moja ni miche 17,600.

Palizi na upunguziaji miche.

Palizi ni budi ianze mapema wiki mbili toka kupandwa mahindi na hufanywa kwa jembe la
mkono au madawa ya kuua magugu. Palizi 2 hadi tatu zinatosha kwa msimu. Madawa ya
magugu yanayoweza kutumika ni Gesaprim na Pioneer

maize 30H83 lita moja inatosha kwa eka moja.

Punguzia miche na kubakiza mmoja au miwili kwa shina kutegemea na nafasi ya kupandia.

Matumizi ya mbolea za kukuzia

Zipo mbolea za aina nyingi ambazo hutumika kwa kukuzia mahindi nazo ni: SA, UREA, ASN
na kiasi cha kilo 50-80 zinatosha kwa eka moja.

PITIA
Fahamu zaidi kuhusu sumu kuvu

Dhibiti ya wadudu na magonjwa

Mimea ya mahindi hushambuliwa na aina mbali mbali za wadudu ambao ni: Viwavi jeshi,
Bungua wa mahindi, Panzi, minyoo inayokata majani. Wadudu hawa hudhibitiwa kwa dawa aina
ya Actellic 50 EC cc 125 za dawa kwa lita 20 za maji.

Magojwa ya mahindi ni: Ugonjwa wa milia, kutu ya majani, kuungua majani Bakajani, kuoza
mashina na mizizi. Magonjwa haya hukingwa kwa kutumia mbegu zenye ukinzani na magonjwa
pia kuzingatia kanuni za kilimo bora.

Mkulima anashauriwa kutumia mbegu bora zinazovumilia magonjwa kama vile milia, kutu,
bakajani na uozaji wa mashine na masuke.

Ukomaaji na uvunaji

Inashauriwa uvunaji uanze mapema mara baada ya mahindi kukauka vizuri. Mahindi ya muda
mfupi hukomaa baada ya siku 90 na mengine huchukua siku120 uvunaji hufanywa kwa kutumia
mikono au mashine .

Hifadhi na uuzaji

Baada ya kuvunwa mahindi yanatakiwa yapukusuliwe na kupetwa tayari kwa kuhifadhiwa,
wakati wa kuhifadhi inashauriwa kutumia madawa. Madawa yanayo shauriwa ni actellic super
dust kiasi cha gram 100 za dawa kwa kilo 100 za mahindi. Pia mkulima anaweza kutumia stocal
super dust kwa gram 100 za dawa kwa kilo 100 za mahindi.

Kimsingi mahindi ni zao la chakula. Hata hivyo mkulima anashauriwa kuuza kiasi ili kupata
fedha kwa matumizi mbalimbali iwapo amepata ziada.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

UFUGAJI WA NG'OMBE

UFUGAJI WA KISASA WA NG’OMBE

UTANGULIZI Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi.  Zaidi ya asilimia95 ya ng,ombe

Read More »

Kilimo Bora cha Mahindi

MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI ABDUL A. MKONO (MWL ABUU), Bsch AEA, SUA Engineer OCTAVIAN J LASWAY BSc Irrigation and water resources (SUA) UTANGULIZI Mahindi

Read More »

CORONA VIRUS EDUCATIONAL POST

Naomba twende polepole Vyanzo vya vifo duniani na idadi (WHO, 2019) Heart diseases – mil 9.43Stroke – mil 5.73COPD – mil 3.04Pumu – mil 2.96Alzheimer’s

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »