KANUNI SAHAHI YA ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU

Habari za wakati huu ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa blog yetu,leo tutaangalia namna ya kulea vifaranga.Zifutazo ni hatua mbali mbali za maandalizi na mapokezi ya vifaranga.

1.MAANDALIZI YA BANDABanda ni jambo la kwanza kwa mfugaji yoyote.banda la kuku huweza kujengwa kwa matofali,mbao,au hata miti na matope.mfano wa banda la matofali lenye dirisha kubwa.Banda la kuku linatakiwa liwe safi wakati wote.

Image result for banda la kuku

1.Sifa za banda la kuku

 1. Lipitishe mwanga wa kutosha
 2. Lisiwe na nafasi ya wadudu hatari na hata wanyama kupita
 3. Liwe karibu na makazi ya mfugaji
 4. Sakafu yake isiwe na matobo tobo mengi(iwe imesakafiwa vizuri kwa njia tofauti)
 5. Banda liwe na ukubwa wa kutosha sawa na idadi ya vifaranga.(mita 2 kwa 3)
 6. Ndani ya banda kuwepo mabox madogo madogo kwaajili ya kuwekea vifaranga.mabox hutunza joto na chini ya mabox hayo au vitalu kuwepo na pumba za mahindi au mpunga ili kuongeza joto.2.Andaa vyombovyombo kwaajili ya maji na chakula.unaweza kununua vyombo ua ukatumia sahani  za kawaida za nyumbani.kwa maji weka mawe madogo madogo  masafi katika vyombo hivyo ili vifaranga wasitawanye sana maji au wao kuloana na maji hayo.mfano wa vyombo katika picha

Related image


3.Andaa taa ya chemli au bulbTaa hutumika kwaajili ya kuongeza joto katika box au kitalu cha vifaranga.taa huwekwa ndani ya box hilo.Kwa wafugaji wakubwa hutumia bulb katika mabanda yao.joto katika vifaranga liongezwe wakati wa usiku na mchana liwe la kawaida.

4.Fahamu ratiba na chanjo kwa vifaranga kama ifatavyo.

 • siku 1-5 –dawa ya kufunga vitovu-
 • siku 7 –NEWCASTLE
 • siku 8, 9,10,11–VITAMIN 
 • siku 14–Gomboro
 • Siku ya 15-20-VITAMIN
 • siku 21–gomboro Baada ya hapo endelea na vitamin hadi siku ya 27
 •  Siku ya 28-NEWCASTLE Kisha endelea na vitamin
 • wiki ya 5 chanjo ya ndui
 • wiki ya 6–Ampronium + ctc (siku tano)
 • wiki ya 7–Vitamin
 • wiki ya 8–dawa ya minyoo
PITIA
JIFUNZE UFUGAJI MSETO WA SAMAKI KATI YA KAMBALE NA SATO

ANGALIZO.EPUKA UCHAFU KATIKA BANDA ILI KUEPUSHA MAGONJWA KATIKA BANDA AMBAYO HUPELEKEA KUKU KUUMWA HIVYO KUTAFTIWA DAWA NYINGI ZAIDI NA KUPELEKEA KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA UFUGAJI.

5.CHAKULA

chakula cha kuku kiwe na mchanganyiko ufuatao.

 1. nafaka(mahindi,uwele,mtama,ulezi nk)——-kg 40
 2. pumba za nafaka_———————-kg 27
 3. chumvi ya jikoni————–kg 0.5
 4. virutubisho———————-kg 0.05
 5. unga wa chokaa na mifupa—–kg 2.25
 6. mashudu ya alizeti ufuta au karanga –kg 20
 7. dagaa na mabaki ya samaki—kg 10

6.ANDAA KUMBU KUMBU MUHIMU IWE NA;

 1. Tarehe ya kutotoresha
 2. Idadi ya vifaranga
 3. Kiasi cha chakula
 4. vifo
 5. Vifaranga vilivyo uzwa
 6. Tarehe ya siku ya kurekodi
 • matibabu
 • ugonjwa
 • mfano wa ratiba hiyo

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

HIZI NDIZO TOFAUTI YA ASALI YA NYUKI WADOGO NA ASALI YA NYUKI WAKUBWA

Watuwengihuwatunatumiaasalipasipokujuawametokananaasaliwaainagani, hivyokilaasaliambayounaitumiakuanzialeonilazimaujuewanatakonananyukiwaainagani. AsalizaNYUKI WAKUBWA na WADOGO zinatofautianakatika mambo kadhaanahvyonimuhimukujuatofautihizokablahujanunuailikuanauhakika. NYUKI WADOGO 1. Ni nyepesizaidikwaniinakiwango cha majikuanziaasilimia 24 2. Ina ladhaya UCHACHU ingawanitamusana. 3. Mara nyingiinarangiya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoendakwenye WEUSI

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »