Kanuni salama za ufugaji wa ng`ombe wa maziwa

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ni moja kati ya ufugaji unao wakomboa wafugaji wengi sana endapo watazingatia kanuni za ufugaji bora, mimi mwenyewe nimekua shahidi nikiona watu wengi wana piga hatua kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia sana wakati unataka kuanza na hata kama umeanza kufuga ng’ombe wa maziwa;

Uchaguzi wa aina bora ya ng’ombe
Hili ni jambo la msingi sana kabla ya kuanza kufuga unatakiwa ujue je ni aina gani ya ng’ombe bora ambaye anaweza kunifaa .

Lakini kwa ufupi kuna aina tano kubwa ambazo zinatumika sana
Fresian
Guersey
Jersey
Ayrshire
Brown swiss

Hivyo unaweza fanya uchaguzi wako kulingana na mahitaji yako kwa kua kila aina ina sifa tofauti na nyezake japo kua fresian ndio aina inayopendwa sana na ndio aina ambayo inatoa maziwa mengi sana kuliko aina zingine zilizo bakia.

Ujenzi wa banda
Wafugaji wengi hua wamezoe kufuga ng’ombe kienyeji ndo maana wanakua hawapati kulingana na jinsi walivyo tarajia. Banda ni lazima liwe bora ili kuongeza uzalishaji

Banda unaweza kuweka  zege chini ili kuwezesha usafi na pia hii inapunguza magonjwa mengi kama vile kuoza kwa kwato.

Pia banda la ng’ombe wa maziwa unatakiwa kuweka paa juu ili kuzuia mvua na jua kufukia moja kwa moja kwa ng,ombe na hii pia inapunguza maamukizi ya magonjwa pamoja na stress kwa ng,ombe.

Lazima banda bora liwe na mifereji ambayo itasaidia kutoa uchafu nje ya banda wakati wa kusafisha hii itasaidia kuounguza uchafu ndani ya banda.

Madilisha pia yanatakiwa kua makubwa kuwezesha hewa na mwanga wa kutosha kuingia ndani ya banda.

PITIA
UFUGAJI WA KISASA WA NG’OMBE

Sehemu ya kulia chakula na pamoja na sehemU ya kunywea maji ni lazima ziwepo.

Kitu kingine lazima sehemu ya kukamulia maziwa iwepo ili iwe rahisi wakati wa kukamua maziwa

Pia ndama lazima walazwe sehemu tofauti na ng’ombe wakubwa.

Chakula
Ili ng’ombe aweze kutoa maziwa ya kutosha ni lazima apewe maji safi na chakula bora na pia lazima  chakula kiwe cha kutosha. kabla ya kuanza kufuga lazima ujiahakikishie chakula cha kutosha na chakukidhi mwanzo hadi mwisho.

Watu wenye eneo hua wanapanda majani ili kuahikisha chakula hakikosekani(pasture). Pia unaweza kukata majani wakati wa masika na kuyatunza vizuri ili kuwalisha wakati wa kiangazi pale malisho yanapokua ya shida.

Pia ng’ombe wa maziwa ni lazima apewe chakula maalumu ambacho kinaongeza maziwa kila siku na hua wanapewa kilo 1 hadi 3 kulingana na uzito wake asubuhi na jioni. n

Pia unaweza kumlisha mapumba au mashudu mabaki ya mazao kama viazi mahindi pia pale majani yanapo kua shida.

Muhimu
Natumaini umejifunza kitu kutoka mwanzo mpaka hapa tulipo fikia, japo kua ufugaji wa ng’ombe sio mgumu sana lakini kunavitu muhimu ambavyo nilazima wewe kama mfugaji uvizingatie ili kuongeza uzalishaji

Ng’ombe ni lazima waoshwe kwa dawa ili kupunguza kushambuliwa na wadudu ambao wanaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa kama ECF, na unaweza kuwaosha ng’ombe kila wiki kutokana na ratiba yako pia unaweza kutumia dawa kama TICK FIX, PARANEX  na zingine nyingi.

Lazima banda liwe safi ili kuzuia maambukizi ya magonjwa kama FOOT ROUT  na usafi unaweza kufanyika kila siku asubuhi au jion.

Ng’ombe lazima apewe chakula na maji safi  ili kuongeza uzalishaji

PITIA
Ufugaji wa nyuki kwa njia ya kisasa

Pia ni lazima kuwatibu au kuchukua hatua pale ng’ombe anapoonekana kua na ugonjwa ili kuepusha maambukizi kwa wengine na pia ili kumuokoa.

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo