KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

UTANGULIZI
Karoti ni aina ya mboga yenye vyanzo vingi vya calcium, iron na wingi wa vitamin B. Kwa jina la kisayansi inajulikana kama Daucus carota, na hustawi sana kwenye udongo wa tifutifu wenye pH ya 6-6.5 na joto (temperature) la 18-24
karoti inalimwa maeneo mengi sana nchini ikiwa pamoja na mbeya, morogoro( maeneo ya uluguru na mgeta), iringa pamoja na kilimanjaro.

aina za caroti

  1. Nantes. hi inapatikana maeneo mengi na inalimwa sana hapa Tanzania. inakuwa kwa haraka na nitamu sana.
  2. Chantenay. hii pia ina ladha nzuri nainataka kufanana na Nantes lakini mizizi yake ni dhaifu ukilinganisha na Nantes.

UANDAAJI WA SHAMBA.
shamba linatakiwa liandaliwe vizuri kuondoa magugu yote na udongo unatakiwa kutifuliwa vizuri kurahisisha mizizi kupenya vizuri kwenye udongo  na maji kupenya vizuri. na pia matuta yake yawe yameinuka kuzuia maji kutuama kwenye tuta, kwani maji kutuama husababisha mizizi kuoza na mmea kutokukua vizuri.

UOTESHAJI.
karoti hupandwa kwa kutumia mbegu moja kwa moja shambani (direct sown), kiasi cha mbegu kinachotumika kupanda (seed rate) ni3.5-4 kg per ha. na mara nyingi hairuhusiwi kuhamisha miche (no transplanting) kwa sababu mizizi yake ni dhaifu ambayo haitastahimili kukua baada ya kuhamishwa.
baada ya wiki ya nne kutoka kupandwa hufuatia kungolea miche iliyorundikana kuipa nafasi kwaajili ya kufanya miche iwe na afya nzuri(thinning).
mbegu za karoti ni ndogo sana ambazo zinatakiwa kupandwa kwenye urefu wa ( 1.9 -2.5) cm.

UMWAGILIAJI
Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha hasa siku za mwanzo. Karoti zilizokosa maji kwa muda mrefu huzaa mizizi midogomidogo. Pia udongo mkavu ukipata maji mengi ghafla husababisha karoti kupasuka. Hivyo mwagilia shamba mara kwa mara kuhakikisha udongo una unyevu wa kutosha wakati wote, kama hali ya hewa m yajua kali.

PITIA
KILIMO BORA CHA KAROTI

UTUNZAJI.

  1. mmea unatakiwa umwagiliwe kwa siku asubuhi na jioni kuupa mmea maji ya kutosha ili uweze kukua vizuri.
  2. kungolea magugu ili kuzuia ushindani kati ya mmea na magugu kwa ajili ya kuupa mmea afya nzuri
  3. kupunguza mirundikana ya miche ili kupatia mimea afya nzuri
  4. kuweka mbolea kwa kukuzia  mmea
KUPUNGUZA MCHE
Mimea ya karoti inahitaji kupunguzwa mara mbili. Mara ya kwanza hupunguzwa ikiwa na majani matatu mpaka manne au wiki mbili tangu kupandwa na kuachwa katika nafasi ya sentimita tano mpaka saba. Mara ya pili hupunguzwa ikiwa na urefu wa sentimita 10 mpaka 13, na kuachwa katika nafasi ya sentimita 10 mpaka 15. Karoti zilizopunguzwa zinaweza kutumika kwa chakula.

MAGONJWA YA KAROTI.

  1. magonjwa ya bacteria (bacterial disease). ambayo husababisha kusinyaa kwa mimea (wilting), na kufanya mmea usikue (stunted growth) na shina kuoza (stem rot) pamoja na kuoza kwa karoti.
  2. magonjwa ya fangasi. (fungal disease).  kama kata kiuno (damping off) huu ugonjwa hushambulia sana miche hufanya miche ishindwe kukua vizuri na mara nyingi hupelekea mche kufa.

NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA SHAMBANI.
tumia mbegu safi wakati wa kupanda, zuia magugu shambani, zuia wadudu wote, na hakikisha shamba  linakuwa safi, (field sanitation) ili kuzuia magonjwa ya mmea nakufanya mmea ukue vizuri.
UVUNAJI.
karoti huvunwa baada ya miezi mitatu na huvunwa kwa kuvuta (uprooting) baada ya miezi mitatu pia inaweza kuvunwa siku 20 kabla ya kuvunwa. karoti hutoa tani (tonne) 30-50 per ha.

SOKO LA KAROTI.
karoti ni zao  muhimu sana ambalo hutumika kama mboga.
huuzwa kwa mafungu au moja moja ambayo kwa moja huanzia kwa  200 shilingi za Kitanzania. soko lake hupatikana sana karibu mikoa yote Tanzania kutokana na faida za karoti katika lishe.

PITIA
KILIMO BORA CHA ULEZI
Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo