KAZI YA KILIMO TANZANIA.


Watu wengi kwenye vyombo vya habari wanalalamika maranyingi wakiwemo vijana, wazee na watu wa umri wa kati kuwa hakuna kazi. Je, hivi nikweli kuwa hakuna kazi Tanzania? Anaye sema hakuna kazi inawezekana yupo sahihi lakini mara nyingi kazi zinakuwepo ila ni kuwa inawezekana kazi hiyo mhusika haipendi mathalani KULIMA.
Wazee wetu wa zamani waliishi tena miaka mingi lakini kazi zao hasa vitabu vya historia vinaeleza kuwa zilikuwa ni Kilimo, ufugaji, uwindaji na kurina asali. Hivyo je, dunia kubadilika kwa teknologia haswa mfumo mpya wa “Digital” ndiyo na watu waache kabisa mambo ya zamani?

Image result for tanzania kilimo
Shamba la KIlimo : Umwagiliaji


Ni ukweli usio pingika kuwa edeni ni kuzuri. Shambani ndipo sehemu matunda mazuri yenye baridi yaliyo iva au matamu yanapo patikana bila kemikali. Pata picha ukienda kwenye shamba la mizabibu, miembe, michungwa, mapapai, mapeasi na matunda mengineyo ni kuwa unayakuta shamba lime limiwa vizuri hakuna vichaka, kumenyeshewa vizuri kwa kumwagilia au mvua kijani kibichi-sipati picha.


Takwimu za dunia zina onyesha kunaongezeko la watu duniani, hivyo na mahitaji ya chakula yanaongezeka. Hivyo hii ni fursa kwa wakulima na wajasiriamali kuitumia fursa iliyopo ya uhitaji wa chakula duniani kuzalisha chakula kwa wingi kwa matumizi ya sasa nay a baadaye katika kujiwekea akiba kwani uhitaji huo utapeleekea njaa pasipo kuchukua tahadhari ya kuzalisha chakula kwa wingi na kuwa na tabia ya kujiwekea akiba. Mwaka 2016 idadi ya watu duniani ilikuwa takribabani bilioni 7.4 na kufikia 2050 wanaweza kufikia watu bilioni 9. Idadi ya watu hawa walio wengi ni masikini na wakulima wadogo. Kwa Tanzania takwimu zinaonyesha kilimo ni moja ya sekta muhimu katika nchi kama uti wa mgongo, inachangia pato la ndani (GDP) kwa asilimia 30%. Na watu zaidi ya 67% huajiriwa katika kilimo kama taarifa mbalimbali zinavyo ainisha. “Kijitabu cha The Economist Pocket World in Figures cha mwaka 2012 na mwaka 2017 kinaonyesha kwamba Pato la Taifa la Tanzania liliongezeka kutoka USD 21.4 bilioni mwaka 2009 hadi kufikia USD 48.1 bilioni mwaka 2014. Hii ina maana kwamba katika kipindi cha miaka 5 uchumi wa Tanzania ulipanuka mara mbili na zaidi. Licha ya Pato la Taifa kupanuka kwa 100%, kasi ya kuwaondoa Watanzania kwenye umasikini ni ndogo mno ambapo mwaka 2014 takribani asilimia 30 ya Kijitabu cha The Economist Pocket World in Figures cha mwaka 2012 na mwaka 2017 kinaonyesha kwamba Pato la Taifa la Tanzania
10
liliongezeka kutoka USD 21.4 bilioni mwaka 2009 hadi kufikia USD 48.1 bilioni mwaka 2014. Hii ina maana kwamba katika kipindi cha miaka 5 uchumi wa Tanzania ulipanuka mara mbili na zaidi. Licha ya Pato la Taifa kupanuka kwa 100%, kasi ya kuwaondoa Watanzania kwenye umasikini ni ndogo mno ambapo mwaka 2014 takribani asilimia 30 ya Watanzania walikuwa ni masikini” – Hotuba ya Arusha, 25/3/2017

PITIA
Nyanya zinahitaji matunzo ili upate mavuno


CHANGAMOTO ZA KILIMO BIASHARA.


Kukosekana kwa mitaji hasa kwa wakulima wadogo. Kilimo biashara kinahitaji rasilimali fedha kwaajili ya kununua pembejeo, teknolojia na gharama mbalimbali za kuwezesha kilimo husika. Ili kufanikisha kilimo biashara ni jambo la msingi kuwaelimisha wakulima wadogo namna ya kuweza kukopesheka na kuwawezesha kwa namna moja au nyingine kupata mikopo yenye riba nafuu na mazingira wezeshi. Katika utafiti nilio ufanya mwaka 2017 kwa wakulima wadogo wa miwa (outgrowers) mkoani Morogoro, utafiti ulionyesha kuwa wakulima wadogo walio wengi wanashindwa kumwagilia miwa yao kutokana na kukosa miundo mbinu ya umwagiliaji na pembejeo mbalimbali kuhudumia kilimo hicho cha miwa kama mbolea, madawa, n.k. Hii ipo maeneo mengi sana kuwa wakulima wadogo wanashindwa kufanya kilimo kuwa cha kibiashara na chenye tija zaidi kutokana na ukata wa fedha (mtaji) kupelekea wengi kulima kilimo cha kutegemea mvua na kilimo cha mazoea. Kilimo hiki cha kutegemea mvua kina changamoto na gharama (risk) ya kupoteza au kukosa mavuno kabisa kama kutatokea ukame kufuatia mabadiliko ya tabia ya nchi.


Kukosa mfumo wezeshi katika kuweka mikataba na wawekezaji wakubwa. Katika kutambua kuwa wapo wadau na mashirika mbalimbali duniani yanayoweza kutoa huduma na misaada mbalimbali kuinua wanyonge, ingefaa kuwaunganisha wakulima wadogo hasa wenye fursa na nia kulima kibiashara kupewa uwezo wa kulima kimkataba na wadau hao. Hii ingesaidia kwenye maswala ya masoko, ukosefu wa mitaji, pembejeo za kilimo na teknolojia mpya nzuri za kigeni. Vikundi vya wakulima wadogo vikiwezeshwa vitazalisha kwa tija na faida kupatikana.
Kupata soko la uhakika. Soko ndio jambo la kwanza kwa mkulima kuangalia, kama mkulima huyo analima kilimo cha kibiashara. Soko linaweza kupatikana kwa uhakika hasa kama kutakuwa na mpangilio maalum wa mkulima na mnunuzi wakubaliane kuwa mazao yatanunuliwa kwa bei elekezi na mambo kama hayo. Kimsingi ukuwaji wa sayansi na teknolojia na vyombo vya habari vimesaidia kukuza soko la bidhaa na huduma za mauzo kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa watu

wengi ulimwenguni. Kupitia mitandao ya kijamii wakulima washauriwe na kupewa elimu namna ya kuitumia vizuri kwa faida.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

MFAHAMU KUKU AINA YA KUCHI

Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na

Read More »

Jinsi ya Kulima tikiti maji

[vc_row][vc_column][vc_column_text] UZALISHAJI WA TIKITIMAJI Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo tumia siku 65-90 kutoka kupandwa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu uliyotumia na hali

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »