KILIMO BORA CHA KOROSHO (CASHEW NUT)

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

UTANGULIZI

koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae karne ya 16 ndipo lilipo fika afrika katika nchi ya msumbiji na baadae likafika Kenya na Tanzania.

kwa hapa Tanzania korosho ulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya kusini Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji.

Mvua;Korosho ustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm – 1250 mm wastani wa mvua kwa mwaka,
napia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari.

Udongo; korosho ukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyanzi kichanga.

KUANDAA SHAMBA

kama mazao mengine shamba la korosho linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho.

nakatika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.

KUPANDA
 Ni muhimu sana   kuchagua mbegu bora kwa kua mbegu utakayo panda ndo itakuonesha kiasi gani utavuna,

 • baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5 unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kiota, baada ya hapo unazianika vizuri hili ziweze kukauka napia unashauriwa kuto panda mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja, nafasi ya kupanda 12m x 6m kwenye maeneo mvua na kiasi cha miti kitakua 139/hectare kwenye maeneo yasio na mvua za kutosha ni 12m x 12m na kiasi cha miti ni 69/ hectare

MUHIMU
Kuna aina mbili ya kupanda mbegu ya korosho

 • kupanda moja kwa moja; hii ni njia mambayo ni risk sana na inaitaji umakini kwa sababu  kunauweze3kano mkubwa wa mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu 3 katika shimo moja na baada ya miezi mi 3 – 4 ngoa mimea na bakiza mmoja wenye afya na muonekano mzuri.
 • njia ya kitaru; hii ni njia ya pili na ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na muonnekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye afya.
PITIA
KILIMO BORA CHA MPUNGA

na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuadhiliwa na magonjwa au wadudu na yale yalio kauka.

MAGONJWA NA WADUDU
MAGONJWA

 • Anthracnose
 • powdery mildew

Hayo ni magonjwa yanayo athiri thana korosho

WADUDU

 • Cashew stem girdler
 • cashew weevil
 • coconut bug
 • heliotropes bug
 • meal bug
 • trips aphids

KUZUIA NA TIBA
ili kuzuia maagonjwa na wadudu unatakiwa

 •   palilia mapema
 • weka shamba katika hali ya usafi
 • tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza kuchanya pamba au maharage hiyo inasaidia kukimbiza wadudu wengine ambao wanakua hawapatani na mazao hayo
 • tumia pesticide kutibu magonjwa
 • tumia insecticide kuuwa wadudu waalibifu.

KUVUNA
Korosho ufikia hatua ya kuzaa matunda pale inapo kua na umri wa miaka 2 1/2 hadi miaka mitatu
napia matunda ukomaa pale inapo kua na miaka 9 hadi 10
uwezekano wa mkoroso kuishi ni miaka 30 hadi 40
na kuvuna hua kunaanza mwezi october hadi mwezi december 

MATUMIZI

 • chakula
 • hutumika kutengeneza rangi
 • kama zao la biashara
 • miti yake hutumkia kama kuni
 • kutengeneza dawa n.k
Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo