KILIMO BORA CHA MPUNGA

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Mpunga ni kati ya mazao ambayo yanalimwa sana dunian na pia ni kati ya mazao ambayo yanapendwa sana na watu kutokana na chakula chake juwa kitamu.,

leo nitakupa muongozo wa jinsi ya kulima mpunga kitaalam  ili kuvuna mazao mengi yenye thaman

 

siku zote maandalizi ya shamba vizuri ni jambo la msingi kwa kua bila kuandaa shamba lako vizuri huwezi kuvuna mazao yalio na ubora.

Pia kunahatu za muhimu ambazo lazma mtu uzifate ili kufanyikiwa kupata mazao bora

 1. KUSAFISHA SHAMBA

Hii ni atu ya kwanza kabisa, unatakiwa kukusanya taka na mabaki ya mazao na kuyazika shambani ili kutengeneza mbolea aina ya mboji.,mara moja moja unaweza kukusanya taka na kuzichoma pale inapo itajika lakn kwa kua kuchoma huua wadudu rafiki.

 1. KULIMA

Hii inaweza kufanya kwa kutumia jembe la mkono,trekta pamoja na jembe la ng’ombe.

kulima inasaidia mbolea kuchanganyika vizuri, miziz kupita vizuri, hewa kupita vizuri katika ardhi pamoja na maji.

unatakiwa kutifua 10-15cm na pia itasaidia magugu kuto ota mapema.

 1. KUTENGENEZA MAJARUBA

Hapa unatakiwa kutengeneza kingo imara ili kusaidia maji kutopenya nje ya jaruba  na kingo inatakiwa kuwa ndefu kiasi ili kusaidia maji ya kutosha kuhifadhiwa ndani ya jaruba 

 

 1. KUVURUGA

katika kuvuruga unatakiwa kuweka maji 3-5 cm kutoka usawa wa bahari na kisha unavuruga ili kuweza kusababisha maji na udongo kuchanganyikana vizuri., hii inaweza kufanywa na jembe la mkono, trekta na jembe la ngo’mbe pia.

 1. KUSAWAZISHA SHAMBA

Baada ya kuvuluga unatakiwa kusawazisha ili udongo uwe na kimo sawa na hii inaweza kufanywa na kutumia leki.

hii usaidia katika upandaji pia kwa sababu aldhi inakua katika kimo kimoja.

 1. UPANDIKIZAJI MPUNGA
PITIA
Kilimo Cha Maharage Ya Njano.

Ili kupata mavuno mengi na kukifanya kilimo cha mpunga kuwa cha faida ni muhimu  wakulima kuzingatia mbinu hii muhimu na kuachana na kilimo cha kiholela kwa kumwaga mbegu moja kwa moja shambani. Aidha kwa wakulima wanaofuata kanuni hii wamepata mafanikio makubwa.

Faida zinazopatikana kwa kupandikiza mpunga

 • Mkulima huweza kuchagua miche bora na mizuri ikiwa kitaluni.
 • Miche hukua haraka na yenye afya .
 • Kiasi kidogo cha mbegu huhitajika.
 • Mavuno huwa mengi.

NJIA ZA KUPANDIKIZA MPUNGA

 • Kupandikiza kwa mistari
 • Kupandikiza bila ya kufuata mistari (Mchaka mchaka).

Njia ya kupandikiza kwa msitari ndio njia bora zaid kwa kua inarahisisha katika  kupalilia pia inasaidia katika uvunaji napia utapata mazao mengi zaid kwa kua ulipanda kwa vipimo

MAANDALIZI YA KUPANDIKIZA MICHE

Kabla ya kupandikiza miche shambani ni muhimu kufanya maandalizi yafuatayo:

 • kumwagilia miche kwanza ili kupata urahisi wa kungo’a
 • Ili kuzuia miche isikatike ovyo, miche ing’olewe kwa kushikwa chini zaidi ya shina
 • Epuka kung’oa miche mingi kwa wakati mmoja
 • Miche ifungwe kwenye mafungu madogo madogo ili kurahisisha usafirishaji na upandikizaji  shambani
 • Miche bora tu ndio ichaguliwe. Sifa za miche bora
 • Iwe na kimo kinacholingana,
 • Iwe na majani mafupi yaliyosimama, yenye mizizi mingi na yenye afya, isiyoshambuliwa na wadudu wala magonjwa,

JINSI YA KUPANDIKIZA MICHE

 • Miche ishikwe  kwa vidole vitatu kama inavyoosha kweye picha chini
 • Pandikiza kati ya miche 2 -3 kwa kila shina
 • Kwa mafanikio zaidi, miche ipandikizwe katika kina cha sentimita 2-3.
Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo