Kilimo bora cha Mtama

UTANGULIZI

Mtama ni miongoni mwa mazao ya nafaka yanayolimwa kwa wingi nchini na duniani kote. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji. Mtama ni zao la nafaka lenye uwezo mkubwa wa kustahimili ukame likilinganishwa na mazao mengine ya nafaka

[wp_ad_camp_5]

HALI YA HEWA NA UDONGO

Mtama uhitaji wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto #18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto #25-33°C ili kukua vizuri. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia #pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi. Mtama unastawi vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa #milimita 300-800 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.

Mtama hustawi kwenye katika maeneo kuanzia usawa wa bahari hadi mwinuko wa #mita 1500 kutoka usawa wa bahari #(mita 0-1500).

KUANDAA SHAMBA

Picha Na; 1: Kuandaa shamba kwa kutumia trekta

Andaa shamba mapema mwazo wa msimu ili kuufanya udongo na majani kuoza vizuri kabla ya kupanda mtama. Kuandaa shamba kunahusisha shughuli kama vile kusafisha shamba, kufyeka,kuondoa visiki, kulima, pamoja na kulainisha udongo. Zana au vifaa mbalimbali vinazoweza kutumika kuandaa shamba hutegemea ukubwa wa shamba au uwezo wa mkulima. Unaweza kutumia jembe la mkono, majembe ya kukokotwa na ng`ombe, trekta au pawer tiller.

KUPANDA

Aina ya mbegu za mtama

Kuna aina mbali za mbegu za mtama amabazo hupandwa maeneo tofauti kulingana na hali ya hewa na uzalishaji wa aina ya mbegu. Aina hizi hutofautiana kulingana na rangi pamoja  na ladha Wakulima wengi hupendelea mtama mweupe. Pia mtama wa mbegu za kisasa huwa laini kuliko mbegu za asili. Mtama wa asili huwa ni mbegu ndefu kwenda juu na huchukua muda mrefu kupanda hadi kuvuna kuliko mtama wa kisasa ambao mwingi ni mfupi na huchukua muda mfupi zaidi na hutoa mavuno bora zaidi ya mtama wa asili.

 • Mbegu za kisasa za mtama ni; #PAN 8816, #PAN 8625, #PAN 8816, #PAN 8625, #PAN 8944, #Serena, #Seredo, #Gadam, #Hakika na #Wahi
 • Mbegu za asili za mtama; Lulu, Sandala, Imani, Tegemeo

 

 • Seredo:

Aina hii ya mtama hilimwa na kustawi zaidi katika maeneo yenye mwinuko wa mita 1500. Huchukua muda wa siku 110-130 kukomaa. Aina hii yam tama ina mbegu zanye rangi ya kahawia na inavutia. Mbegu hii hutoa mavuno kiasi cha kilo 4500-5000 kwa ekari.

 • Serena:

Hustawi katika maeneo yenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.

 • Gadam:
PITIA
Kilimo Bora cha Mahindi

Inafanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.

 • Hakika na Wahi:

Mbegu hizi za mtama zina uwezo wa kuoteshwa na kustawi maeneo yaliyoathiriwa na wadudu. Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.

Kiasi cha mbegu

Ikiwa mtama utapandwa kwenye mistari, kilo 7-8 za mbegu kwa ekta zitahitajika kwani hakutakuwa shughuli ya kupunguza mimea na ikipandwa kwa bila mistari, itahitajika kilo 8-10 za mbegu kwa ekta na itahitajika kupunguza mimea.

Kupanda

Kabla ya kupanda mbegu za mtama, hakikisha udongo umetifuliwa na kulainishwa vizuri ili kufanya mbegu ziweze kuota vizuri kwa sababu mbegu za mtama ni ndogo sana hivo zinahitaji udongo laini. Mtama unaweza kupandwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kupanda kwa mistari na nyingine ni kupanda kwa katawanya. Kupanda kwa kutawanya hufanywa kwa kurusha mbegu juu ya udongo na kufukia au kuchananya udongo na mbegu. Upandaji wa kutawanya huhitaji kupunguza mimea shambani baada ya kuota. Kupanda kwa mistari huzingatia nafasi kati ya mmea na mmea, msitari na msitari na upandaji huu hauhitaji kupunguza mimea baada ya kuota. Nafasi ya upandaji hutofautiana kilingana na aina ya mbegu iliyotumiaka pamoja na matumizi ya mazao.

Nafasi ya upandaji wa mtama

 • 75 sm x 10 sm
 • 60 sm x 20 sm
 • 90 sm x 20 sm
 • 90 sm x 50 sm

Panda mtama katika kina cha sentimeta 2 na fukia vizuri na udongo

Picha Na; 2: Nafasi ya upandaji wa mtama

Mbolea za kupandia

Mtama unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya samadi pamoja au mbolea za chumvichumvi kama vile DAP, TSP, na NPK. Mbolea iweke kwenye mistari na kuchanganywa na udongo ili isigusane na mbegu wakati wa kupada Kiasi cha mbolea kinachohitajika kwa ekari moja ni mfuko mmoja wa kilo 50.

KUPUNGUZA MIMEA

Ikiwa mtama ulipandwa kwa kutawanywa, shughuli ya kupunguza mimea ifanyike wiki 2 hadi 3 baada ya mimea kuota ambapo mimea inakuwa imefikia urefu wa sentimita 20-30 Kupunguza mimea hufanyika ili kuwe na idadi ya mimea inayotakiwa kufanya mimea ikue vizuri kwa kupata nafasi na mwanga wa kutosha.

KUPALILIA/PALIZI

Palizi ifanyike mara mbili kwa sababu kwenye mazao ya nafaka magugu hukua kwa kasi hivo palizi ikichelewa mazao hupotelea shambani. Shamba la mtama ni lazima liwekwe katika hali ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni.

Palizi ya kwanza ifanyike wiki 2-3 baada ya mimea kuota ambayo huambatana na kupunguza mimea na palizi ya palizi ya pili ifanyike kabla mmea haijaanza kutoa maua. Kipindi cha mwanzoni mimea ya mtama huitaji hali ya usafi zaidi kuliko unapokuwa mkubwa hivyo huitaji kupaliliwa mara mbili kupandwa hadi kuvunwa. Palizi inaweza kufanywa kwa kutumia jembe la mkono, trekta, power tiller au viua gugu kama vile 2, 4-D.

KUKUZIA

Kuzia mtama baada ya palizi ya palizi ili kurudisha virutubisho viliovyoondolewa na magugu wakati wapalizi. Kukuzia huongeza na kuupatia mmea virutubisho vinavyohitajika kwa ajili ya ukuaji wa majani na utengenezaji wa chakula. Mbolea za kukuzia zinazoweza kukumika ni CAN, UREA na SA. Kiasi cha mbolea kinachohitajika ni kilo 50 kwa ekari.

PITIA
KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI

WADUDU, VIUMBE WAHARIBIFU NA MAGONJWA KATIKA MTAMA

a)    Wadudu

         i. Usubi wa mtama

Mdudu huyu ni mmoja wa wadudu waharibifu muhimu sana wa mtama duniani kote. Usubi waliokomaa hutaga mayai kwenye maua ya mtama. Mabuu yanapoanguliwa hula mbegu zinazoendelea kukua, na kufanya maua kuwa na mbegu ambazo hazijajaa vizuri au kukosa mbegu kabisa.  Dalili ni pamoja na nafaka zilizonyauka ambazo matokeo yake ni maua ambayo hayana mbegu na masuke (au vichwa)

Picha Na; 2: Nafasi ya upandaji wa mtama

Jinsi ya kudhibiti

 • Panda mtama mapema na kwa wakati mmoja kwenye eneo kubwa
 • Tumia mbegu bora za mtama /au chotara za mtama zinazostahimili madhara
 • Tumia dawa kama Endosulfan, Ambush, Marshal au Karate kuangamiza wadudu.

     ii. Vipekecha shina wa mtama

Vipekecha shina ni wadudu waharibifu wakubwa sana wa mtama kote barani Afrika.

Vipekecha shina huchimba mahandaki ndani ya shina la mmea na kulisha kwenye tishu ndani na kusababisha mmea kudhoofika

Udhibiti

 • Panda mapema ili kuepuka ushambulizi mkubwa wa vipekecha shina.
 • Kuweka nitrojeni, kama mbolea ya madukani au mbolea ya samadi, huongeza uwezo wa mimea kuvumilia mashambulizi
 • Kupanda mseto na mimea isiyokuwa wenyeji wa vipekecha shimo, kama vile kunde au mihogo, pia hupunguza uharibifu.
 • Udhibiti wa kikemikali ni lazima tu kutumika wakati mashambulizi ni makali

   iii. Inzi wa bua (Antherigona soccata)

Madhara yanatokea siku 7 hadi 30 baada ya kuota . Viluwiluwi wanaotokana na mayai ya nzi wa bua hula ndani ya mmea na kusababisha  mimea kushindwa kukua vizuri na mimea mingine kuangua shambani. Madhara huwa makubwa kutokana na kuchelewa kupanda

Namna ya kudhibiti

 • Panda mapema ili mtama ukomae kabla mashambulizi ya wadudu hayajaanza
 • Ondoa na kuchoma mabaki mazao ya msimu uliopita wakati wa kuandaa shamba
 • Tumia mbegu bora zenye kustahili wadudu
 • Tumia madawa ya kunyunyizia kama vile aina ya chembechembe za Bulldock inayowekwa kwenye mimea ya umri wa wa wiki 4 kuzuia “vitoboabua”

   iv. Bungua mtama – (Sitophilus oryzae)

Bungua na viluwiluwi huharibu mbegu na kuifanya isiwe na matumizi yoyote

Jinsi ya kukabiliana na wadudu katika ghala

 • Vuna mapema mtama mara tu unapokuwa umekomaa ili kuzuia wadudu kutaga mayai ambayo huanguliwa wazao zikishapelekwa ghalani
 • Kausha vizuri mtama kutumia maghala ya kuhifadhia yenye ubora na ambayo yanapitisha hewa vizuri
 • Safisha vizuri ghala na kuweka dawa wiki 6 kabla ya kuvuna.
 • Nyunyuzia dawa ya kuua wadudu kama vile Actellic Super, Malathion au pyrethrum dust

b)    Ndege

        i. Kwelea kwelea (Queleaquelea)

Hawa ni ndege waharibifu sana katika zao la mtama, hushambulia mtama unapoanza kukomaa kwa kula mbegu katika masuke na kuacha masuke yakiwa matupu. Huruka kwa makundi makubwa na kushambulia mazao shambani kwa muda mfupi.

     ii. Njiwa

Ndege hawa pia kupendelea kula mtama kwa kiasi kikubwa. Hushambulia mtama unapoanza kukomaa.

Jinsi ya kukabiliana na ndege waharibifu

 • Kupanda mapema mbegu zinazokomaa wakati mmoja
 • Kutumia nyaya za miali kama vile ribbons, aluminum foils, kanda .
 • Mikebe ya mawe iliyofungwa na kamba ili kutoa sauti wakati kamba ikivutwa
 • Kuvuna wakati unaofaa
 • Kuharibu maeneo ya kuzaliana ndege karibu na shamba
PITIA
KILIMO BORA CHA MPUNGA

c)     Magonjwa

Kama yalivyo mazao mengine, mtama hushambuliwa na magonjwa kadha wa kadha. Miongoni mwa magonjwa yanayoshambilia zao la mtama ni pamoja na

        i. Fugwe

Fugwe ni ugonjwa unaosababishwa na ukungu aina ya  Sphacelotheca sorghi na  hushambulia  sana  mtama.    Mtama  ulioshambuliwa  na  ugonjwa  huu mbegu zake huwa na unga mweusi (umejaa viyoga) uliofunikwa na ngozi ngumu yenye  rangi  kati  ya  nyeupe,  maziwa  na  kikahawia.

Picha Na; 10: Mtama ulioshambuliwa na ugonjwa wa Fugwe

  ii. Kutu ya majani

Ugonjwa huu hushambulia majani yam mea na kufanya mmea kushindwa kukua vizuri. Dalili za ugonjwa ni kuwepo kwa kutu katika majani, kutu hii hufunika majani na hufanya mmea kushindwa kutengeneza chakula hivo huathiri ukuaji na uzakishaji wa mtama

Kutu ya majani

  iii. Mildew ya mtama

Majani mapya yanayotoka kwenye mimea iliyoambukizwa kupitia mfumo wa ndani wa kupitisha maji na virutubishi kwanza hupoteza rangi kabla milia myeupe kutoka, ambayo hupanuka zaidi kwenye majani yanayozaliwa baadaye hukauka

Njia za kudhibiti ugonjwa

 • Kuchagua na kuvuna masuke ya mbegu toka shambani kwa ajili ya kupanda msimu unaofuta kabla ya kuvuna mazao yote kwa ajili ya chakula.
 • Kuchagua masuke ambayo hayaonyeshi ugonjwa wa fugwe toka shambani.
 • Mbegu zilizochaguliwa kwa ajili ya kupanda zitengwe na mtama mwingine na hasa wakati wa kuvuna, kupiga na kupepeta wakati ambapo viyoga husambaa kwa wingi hewani.
 • Ng`oa mimea iliyoshambuliwa sana na kuchoma moto. Kama sehemu ndogo ya suke imeshambuliwa iondoe sehemu hiyo usisubiri mpaka mazao yanapokomaa na kutoa vinyoga.  Ondoa masuke mara tu unapotambua  kuwa yanaonyesha ugonjwa wa fugwe.

KUVUNA MTAMA

Mtama unatakiwa uvunwe mara tu baada ya kukomaa ili kuepuka mashambulizi ya wadudu na viumbe waharibifu kama ndege. Pia unaweza kuvunwa kabla haujakauka ila unaonesha dalili za kukomaa nakuanikwa mpaka masuke yakauke. Dalili za mtama uliokamaa ni pamoja kubadilika rangi ya suke na kuwa kahawia. Mtama huchukua siku tofauti kukomaa kulingana na aina ya mbegu iliyotumika. Kwa kawaida huchukua siku   120 – 150 kwa mbegu ya muda mrefu na siku 115-120 kwa mbegu ya muda mfupi. Mtama unaweza kuvunwa kwa kutumia kisu chenye makali au kwa kutumia mashine maalumu ya kuvunia (combined harvester)

UKAUSHAJI

Kausha mtama kwa kuuanika kwenye jua kwa kutumia mikeka au matrubai masafi. Baada ya kuvuna, mtama ukaushwe vizuri ili kurahisisha upigaji, na baada ya kupiga, mtama uanikwe vizuri ili ukake na kuwa na kiasi cha maji kinachofaa kwa kuhifadhi. Epuka kukausha mtama sehemu chafu, hii itasababisha kupoteza ubora wa zao

KUHIFADHI

Mtama uliokausha vizuri, uwekwe kwenye mifuko maalumu kwa ajili ya kuhifadhi. Endapo kuna dalili ya wadudu, tumia dawa kwa ajili ya kuangamiza wadudu hao kabla mazao hayajashambuliwa na wadudu. Pia kabla ya kuhufadhi mtama ghalani, hakikisha ghala lipo katika hali ya usafi na ubora. Ghala la kuhifadhi mtama liwe na sifa zifuatazo;

 • Liwe limeezekwa vizuri ili kuzua maji kuingia na kuharibu mtama kipindi cha mvua
 • Liwe na mfumo mzuri wa kupitisha hewa na mwanga
 • Liwe safi wakati wote ili kuzuia mazalia ya wadudu wanaoshambulia mazao kwenye ghala

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

AINA ZA UDONGO ZINAZOPATIKANA TANZANIA

Udongo ni rasilimali muhimu inayotumiwa katika shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo ambacho kinategemewa na watanzania kuendesha uchumi wa taifa. Lakini uharibifu wa mazingira umechangia kushuka kwa

Read More »

Huu ni mfano wa Kuigwa

  Shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mbogamboga la Ngongoseke lililoko katika kijiji cha Nsola wilayani Magu ni mfano wa kuigwa katika matumizi ya ziwa

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »