KILIMO BORA CHA SOYA

Soya ni zao jamii ya mikunde ambayo ina baadhi ya sifa za mbegu zinazozalisha mafuta. Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya juu kuliko iliyoko katika aina nyingine ya mazao ya mimea. Kiasi cha protini katika soya inazidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa.
Sifa nyingine za zao la soya ni pamoja na kuwa na mafuta yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol), uwezo wa mmea wa soya kuongeza mbolea aina ya nitrojeni kwenye udongo, uwingi wa protini unaoweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha, uwezo wa soya kustawi katika maeneo yanayostawisha mahindi na maharage unamaanisha kwamba zao hilo linaweza kulimwa sehemu nyingi nchini Tanzania.Sifa hizo zimefanya zao la soya kuwa muhimu katika chakula cha binadamu na mifugo na katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za vyakula na madawa. Vilevile gharama za uzalishaji wa soya ni ndogo ukilinganisha na mazao mengine.SoyaPamoja na manufaa hayo ya zao la soya, zao hilo halifahamiki kama ilivyo mazao mengine mfano maharage na mahindi. Wakulima wengi hawazijui kanuni za kilimo bora cha soya. Hii inatokana na kutojua umuhimu wa zao hilo na hivyo kutotilia maanani katika kulilima na kulitumia kuboresha afya na kipato hasa katika ngazi ya kaya. Makala hii imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kumuelekeza mkulima jinsi ya kulima soya.

2. HALI YA HEWA NA UDONGO

Soya ni zao linalostahimili ukame na huweza kulimwa  kwenye maeneo yenye mvua za kidogo, wastani hadi mvua nyingi kiasi vilevile soya hufanya vizuri kwenye udongo wa tifutifu japo hufanya vizuri pia kwenye udongo wa mfinyanzi.

Mahitaji ya Mvua

Soya huhitaji wastani wa #mililita 350 hadi #1,500 za mvua kwa mwaka na inayonyesha kwa mtawanyiko mzuri hususan katika kipindi chote cha ukuaji wa zao hilo. Soya pia inafaa katika kilimo cha umwagiliaji kwani katika maeneo hayo kunakuwa na uhakika wa unyevu muda wote. Jambo la kuzingatia ni kutowepo kwa mvua wakati soya inapokauka

3. KUANDAA SHAMBA

Shamba la soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa mazao mengine. Utayarishaji huo wa shamba ni pamoja na kuondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage). Shamba  la  soya  linaweza  kulimwa  kwa  sesa  au  matuta. Kilimo  cha  sesa  chaweza  kulimwa  kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi kama maksai na punda au kwa kutumia trekta.  Kilimo cha matuta kuzuia mmomonyoko wa udongo na kupunguza kasi ya maji kinafaa na kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinuko  Vilevile kilimo cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye mvua nyingi ili kupunguza madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua kubwa kunyesha.

PITIA
Umuhimu wa kitunguu swaumu katika kutibu magonjwa ya kuku

4. JINSI YA KUPANDA SOYA NA WAKATI SAHIHI WA UPANDAJI

Jambo la kuzingatia wakati wa kupanda ni kuhakikisha kuwa mbolea haigusani na mbegu kwa sababu mbolea itaunguza mbegu na hazitaota.Upandaji wa Soya hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika. Maeneo yenye mvua nyingi Soya huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Novemba mpaka katikati ya mwezi Desemba na Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi February hadi March.

  • Mkulima anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa na wataalamu. Nafasi hizo ni #sentimeta 10 kwa #sentimita 45 kwa soya fupi kama #bossier na kwenye sehemu zenye rutuba hafifu.
  • #Sentimeta 10 kwa #sentimita 60 kwa soya ndefu kama #UyoleSoya1 na kwenye sehemu zenye rutuba nyingi.
  • Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi #sentimita 5 ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya.

Mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya kabla ya kupanda.

4.1 KIASI CHA MBEGU NA UPANDAJI WA SOYA

Ni muhimu kuandaa mbegu bora na safi  mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa wastani #kilo 20 hadi #30 za mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua

4.2 MBOLEAKama ilivyo kwa mazao mengi, soya pia huhitaji udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji. Hivyo endapo soya italimwa katika sehemu yenye rutuba hafi fu, itahitaji mbolea kama mazao mengine ijapokuwa huvumilia udongo wenye rutuba hafi fu. Kwa hiyo uamuzi wa kutumia au kutotumia mbolea na kiwango cha kutumia utategemea rutuba iliyopo kwenye udongo katika eneo husika.  Hata hivyo, soya huhitaji wastani wa #kilo 80 hadi #100 za mbolea aina ya #DAP na #TSP kwa hekta moja na #kilo 60 hadi #80 kwa mbolea aina ya #CAN kwa hekta moja (Heka 2 na Nusu).

PITIA
MCHANGANUAO WA KILIMO BORA CHA NANASI NA FAIDA UTAZOZIPATA

4.3 KUZUIA MAGUGUSoya ni zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili baada ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili inategemeana na kiwango cha magugu shambani. Endapo magugu yatakuwa yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili inaweza isihitajike kama inavyoonekana kwenye #Picha Namba 1 ambapo soya iliyopandwa kwa nafasi zinazotakiwa imekua na kufunika magugu yote na hivyo palizi ya pili kutohitajika. #Picha Namba 2 inaonyesha soya iliyopandwa kwa nafasi pana na isiyotakiwa ambayo haijakua kufi kia kiwango cha kufunika magugu na hivyo kulazimisha palizi ya pili kufanyika. Magugu katika shamba la soya yanaweza kudhibitiwa pia kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata hivyo inafaa kufuata maelekezo ya kutumia ya dawa husika yaliyopo kwenye kibandiko

5. MAGONJWA,WADUDU NA VIUMBE WANAOSHAMBULIA SOYA

  • MAGONJWA

Tofauti na mazao mengine, magonjwa ya soya ni machache. Hata hivyo magonjwa ambayo hutokea kwa nadra ni yale yanayotokana na vimelea vya ukungu na bakteria.  Magonjwa hayo huenezwa kwa mbegu, masalia ya mimea shambani na wadudu mafuta.Njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo katika zao la soya ni kupanda mbegu safi na zilizopendekezwa mahali husika.  Aidha, panda kwa mzunguko (crop rotation) kwa kutumia mazao yasiyoshambuliwa na magonjwa ya soya kama alizeti na mahindi.

  • WADUDU WAHARIBIFU KWENYE SOYA

Soya haishambuliwi sana na wadudu kama ilivyo sehemu nyingine ambako zao hilo hulimwa kwa wingi. Hata hivyo endapo wadudu watatokea mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion 50% EC kwenye kipimo cha #mililita 40za dawa na #lita 20 za maji au kipimo kinacho pendekezwa katika dawa husika. Upuliziaji wa dawa ufanywe kulingana na kiasi cha mashambulizi ya wadudu kwenye mazao.Hakuna wadudu waharibifu wa soya ghalani. Hivyo zao hilo linaweza kutunzwa kwa muda mrefu ghalani bila kuwa na athari za wadudu. Kwa mkulima na wafanyabiashara, kutokuwepo wadudu waharibifu ghalani kunapunguza gharama za utunzaji hadi bei nzuri itakapofikiwa. Wanyama waharibifu

PITIA
UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

 5.3 WANYAMA WAHARIBIFU KWENYE SOYA

Kwa kawaida soya hupendwa sana na panya wa shambani na ghalani. Wanyama wengine ni pamoja na sungura, paa, swala, Ngedere n.k.  Mkulima anashauriwa kutumia mbinu na njia mbalimbali zikiwemo za asili, kukabiliana na wanyama hao bila kuharibu mazingira.

  • UVUNAJI WA SOYA
    • DALILI ZA KUKOMAA

NJIA ZA UVUNAJIDalili za soya kukomaa ni wakati majani yanapokuwa na rangi ya njano. Mkulima anshauriwa kuanza kuvuna baada ya majani kuanza kupukutika.
Baada ya soya kupukutisha majani shambani mkulima anatakiwa kung’oa soya kwa kutumia mikono au anaweza kuvuna kwa kutumia mashine maalumu za kuvunia.

  1. MBINU BORA ZA KUTUNZA SOYA BAADA YA KUVUNA

7.1 KUPUR

ASoya haitakiwi kupigwa kwa nguvu kwa sababu mbegu zake hupasuka kirahisi. Mara baada ya kupura, ondoa takataka na uchafu mwingine kwenye soya kwa kupepeta na kupembua. Kasha Kausha soya kufikia wastani wa asilimia 10 ya kiasi cha maji/unyevu (moisture content) kisha ihifadhi ghalani kwa matumizi au kusubiri soko.  

7.2 KUHIFADHI

Soya ikikauka, maganda yake hupasuka na mbegu hupukutikia chini. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi kuvuna soya mara inapokomaa na kuanza kukauka. Ili kuzuia upotevu wa zao shambani, inashauriwa kuvuna majira ya asubuhi au majira ambayo sio ya jua kali endapo soya imekauka na kuanza kupasuka wakati wa kuvuna.
Wataalamu wa uhifadhi bora wa mazao wanashauri kuwa ni vyema mazao yakawekwa juu ya mbao au vichanja maalumu vijulikanavyo kama pallets. Hivi vinazuia soya kuharibika na kukosa bei nzuri sokoni. Vile vile ghala linapaswa kuwa na sifa bora kama kutokupitisha wadudu waharibifu, paa lisilovuja na mzunguko mzuri wa hewa ili kufanya soya iliyohifadhiwa ikae kwa muda mrefu.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Mpunga / mchele

KILIMO BORA CHA MPUNGA

Mpunga ni kati ya mazao ambayo yanalimwa sana dunian na pia ni kati ya mazao ambayo yanapendwa sana na watu kutokana na chakula chake kuwa

Read More »

KILIMO-BIASHARA

Kilimo-Biashara ni neno moja linalo unganishwa na maneno mawili neno KILIMO na neno BIASHARA, na inaweza kuelezewa kuwa ni shughuli ya kilimo inayo husisha matumizi

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »