KILIMO BORA CHA ULEZI

Ulezi ni punje ya mlezi au mwele (aina ya nafaka) ambao hulimwa katika sehemu zenye hali ya ukame. Ulezi ni zao la asili, shirika la chakula duniani (FAO) likisema kuwa nafaka hiyo ni muhimu siyo tu kwa mlo bali pia kwa kuinua kipato cha wakulima wadogo. Katika tovuti yake FAO imesema unga wa ulezi ambao hujulikana pia kama wimbi, unaweza kutumika kutengeneza mkate, chapati maji, uji, ugali au hata kinywaji na zao hilo lina virutubusho vya madini kama yale ya chuma na Calcium.

ASILI YAKE
Ulezi ni zao muhimu katika maeneo ya semiarid tropics ya Asia and Afrika (Hasa nchi kama in India, Mali, Nigeria, and Niger), na asilimia 97% ya uzalishaji wa Ulezi katika nchi zinazoendelea. Zao linapendwa kutokana na uzalishaji wake na linastawi kwa mda mfupi katika msimu wa kiangazi, kipindi cha joto. Ulezi ni chakula muhimu katika historia ya mwanadamu, hasahasa Asia and Afrika. Asia mashariki wamekuwa wakilima hili zao kwa miaka 10,000 huko nyuma.
FAO inasema ulezi ulianza kulimwa katika kaya miaka 5,000 iliyopita huko Ethiopia na Uganda na hatimaye maeneo ya nyanda za chini barani Afrika. Miaka 3,000 baadaye India ilianza kulima zao hilo na sasa ni kitovu cha matumizi mbali mbali ya nafaka hiyo

HALI YA HEWA & UDONGO
Zao la Ulezi linahitaji joto la kiwango cha 30 C mpaka 340 C kwa mchana na 22 C mpaka 250 C kwa joto la usiku na jua. Na inamea hasa maeneo yenye mvua kiasi cha cm 100. Zao la Ulezi linakubali kwenye udongo mwepesi na kina kirefu kutoka juu ya ardhi na udongo wenye rutuba.

PITIA
MIGOMBA - KANUNI ZA KILIMO BORA

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Shamba la Ulezi linatakiwa kutayarisha baada ya mavuno ya msimu uliopita, wiki mbili au wiki tatu kabla ya kupanda, hakikisha shamba lako lina udongo wenye rutuba na hautuamishi maji, kama shamba halina rutuba weka mbolea za asili (samadi au mboji).

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Andaa mapema mbegu wiki moja kabla ya kwenda kupanda, Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu kwasababu ni safi hazijabunguliwa na wadudu, huzaa mazao mengi na pia hustahimili magonjwa.

UPANDAJI
Mara nyingi Ulezi hupandwa kipindi mvua zinapoanza kunyesha, Baada ya kuandaa shamba na kuandaa mbegu, Mbegu ni lazima zifukiwe ardhini usawa wa sentimita 3 kwenda chini, hii itasaidia kuepuka kuota wakati ambao si msimu kamili wa mvua. Pia zinaweza kufukiwa kiasi cha sentimita 2 wakati ardhi inapokuwa na unyevu. Ulezi unahitaji rutuba ya hali ya juu wakati wa kupanda na wakati wa kuota. Ni vizuri kutumia samadi au mboji iliyooza vizuri wakati wa kuandaa shamba. Nafasi ya kupanda ni sentimita 50 kwa 10 au 50 kwa 20.

MBOLEA
Katika mbolea inatakiwa mkulima aweke mbolea asili (samadi au mboji) kipindi cha kuandaa shamba, kama shamba halina rutuba na hakuna mbolea za asili unaweza kupandia DAP.

UPALILIAJI
Palizi ya mkono ifanyike walau mara mbili. Shamba la Ulezi ni lazima liwekwe katika hali ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni. Ni lazima kung’oa baadhi ya mimea inapokuwa na urefu wa sentimita 30, au siku 30 baada ya kupanda, ili kuwa na uhakika wa nafasi ya sentimita 10 kati ya mstari na mstari kwa msitari unaokusudiwa au nafasi ya sentimita 20 kati ya mstari kwa msitari.

PITIA
Kilimo Cha Zao La Choroko

MAGONJWA & WADUDU

UGONJWA WA BLAST YA ULEZI
• Ugonjwa hatari kuliko yote • Unasababishwa na fangasi Magnaporthe grisea • Inadhuru ulezi katika hatua zote za ukuaji • Upungufu wa mazao kwa asilimia 40-90 • Vijidudu vya blast hupendelea hali ya joto pamoja na unyevu angani • Vijidudu huendelea kuishi kwenye mabua kutoka msimu mmoja hadi mwingine na pia kwenye mbegu na magugu aina ya ulezi kama Eleusine indica

Jinsi ya kuzuia Blast ya Ulezi
• Tumia mbegu zenye afya na ubora • Tumia aina za ulezi zinazostahimili blast • Kuharibu na kuchoma mabaki ya mabua • Ondoa magugu na mimea inayoshikwa na blast • Madawa: Kama mchanganyiko wa Bordeaux Ulezi uliosagwa na kufungwa kwa matum,izi mbalimbali mbbalimbali Shingo na vidole vyenye blast blastBlasted fingers and neck crop husbandry Aina ya ulezi inayostahimili blast, na iliyohudumiwa vizuri.

UVUNAJI
Ulezi hukomaa na kuwa tayari baada ya miezi minne tangu upandwe, dalili za kuvuna hujitokeza pale ulezi unapokauka na kubadili rangi ya udongo mwekundu ulio iva. Kwa wakulima, ulezi pamoja na kwamba kiwango chake cha mavuno kwenye eneo dogo ni kikubwa, pia unaweza kuhifadhiwa kwa miaka miwili bila kemikali zozote hatarishi na ni mwokozi wakati msimu wa mavuno unapodorora.

MATUMIZI
1. Chakula • Uji ulio na chachu na usiokuwa na chachu • Ugali • Chakula cha watoto wanaoachishwa kunyonya • Chakula bora kwa wagonjwa • Chakula kwa mama wazazi wanaonyonyesha • Mikate na keki (mchanganyiko wa nafaka)

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo bora cha Mtama

UTANGULIZI Mtama ni miongoni mwa mazao ya nafaka yanayolimwa kwa wingi nchini na duniani kote. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mtama

Read More »

AINA ZA UDONGO ZINAZOPATIKANA TANZANIA

Udongo ni rasilimali muhimu inayotumiwa katika shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo ambacho kinategemewa na watanzania kuendesha uchumi wa taifa. Lakini uharibifu wa mazingira umechangia kushuka kwa

Read More »

KILIMO BORA CHA KAROTI

UTANGULIZI Karoti ni zao la mbogamboga ambalo ni zao mzizi, kwa kawaida hupatikana katika rangi ya machungwa, zambarau, nyeusi, nyekundu, nyeupe na njano. Karoti za

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »