Kilimo cha Karoti

KILIMO CHA KAROTI
KILIMO CHA KAROTI

KILIMO CHA KAROTI : Zao la karoti asili yake ni Asia ya Kati. Zao hili lilienea nchi za Ulaya kwa kupitia Bahari ya Mediterranean. Baadaye lilipelekwa Amerika Kusini na Kaskazini, kisha Afrika.

Karoti hutumika kama kiungo cha mboga katika vyakula mbalimbali. Huweza kutafunwa mbichi au kutengenzwa kachumbari. Karoti ina vitamin A ambayo husaidia macho kuona vizuri. Mbegu za karoti hutoa mafuta ambayo hutumika kuongeza harufu nzuri kwenye chakula.

MAZINGIRA:

Karoti hustawi vizuri kwenye sehemu za joto la wastani (nyuzi joto 15 hadi 27 za sentigredi). Kiasi cha mavuno yanaweza hutegemea aina ya karoti na rutuba ya udongo. Zao hili hustawi vizuri katika udongo mwepesi, wenye rutuba ya kutosha, kina kirefu na usiotuamisha maji.

AINA:

Kuna aina nyingi za karoti. Zifuatazo ni aina zinazolimwa nchini Tanzania.

 Nantes – Hii ni ndefu, huvunjika kwa urahisi, ina umbo la kuchongoka na ncha kali. Aina hii hupendwa sana kutafunwa na kutokana na ladha yake tamu. Aina hii haifai kwa kwa kusindikwa.

• Chantenary – Hizi ni nene kwa umbo, na zenye ncha butu. Unene wa nyama ya nje na ndani hulingana, hivyo zinafaa sana kwa kusindikwa. Huwa na rangi ya machungwa iliyofi fi a na ladha yake siyo tamu. Aina hii hustawi vizuri kwenye udongo mzito.

• Oxyheart – Ni fupi na nene. Huvunwa baada ya muda mfupi kulingana na aina zingine.

• CapeMarket – Aina hii hupendwa sana kutafunwa zikiwa mbichi, pia zinafaa kusindikwa.

 Flacoro – Aina hii huzaa sana na mizizi yake ni mirefu. Hufaa kwa kuhifadhiwa na kusafi rishwa, kwa sababu haziharibiki haraka.

• Topweight – Aina hii ina sifa kama za fl acoro. Kwa kuwa na mizizi mirefu inahitaji kina kirefu cha udongo-tifu.

PITIA
Kahawa Inayoleta Utajiri

UTAYARISHAJI WA SHAMBA:

• Ili kupata mavuno mengi na bora, eneo la kupanda inabidi litayarishwe vizuri. Iwapo shamba ni jipya, miti na visiki vyote vikatwe. Visiki na takataka zote ziendolewe shambani. Baada ya hapo shamba lilimwe vizuri kwa kina cha kutosha. Lainisha udongo ili kurahisisha utoaji wa mbegu za karoti ambazo ni ndogo sana.

• Kama eneo lina udongo wa mfinyazi au wa kichanga ni muhimu kuweka mbolea za asili zilizooza vizuri. Mbolea hizi hufanya udongo wa mfinyazi uwe mwepesi wa kuweza kuruhusu maji na hewa kupenya kwa urahisi.

• Endapo karoti zitastawishwa wakati wa mvua nyingi, zipandwe kwenye matuta yaliyoinuliwa.

Karoti huwa na wingi wa vitamini A na hutumika kama kiungo kwenye mapishi mbalimbali

KAROTI SHAMBANI
KAROTI SHAMBANI

UPANDAJI:

• Karoti hupandwa moja kwa moja shambani katika matuta au sesa. Kiasi cha gramu 80 ( sawa na vijiko vidogo vya chai 16) kinatosha kupanda eneo la mita mraba 100. Heka moja huhitaji kilo 8 za mbegu.

• Hakikisha mbegu unazozipanda zina uwezo wa kuota kwa kuzifikicha. Ukifikicha mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali. Ili mbegu ziote haraka ziloweke katika maji kwa muda wa saa 24. Baada ya hapo changanya mbegu hizo na mchanga kwa kiasi kinacholingana ili kupata mchanganyiko mzuri wakati wa kupanda.

• Kama utapanda karoti katika matuta, tengeneza matuta yaliyoinuliwa kidogo, kiasi cha sentimita 10 mpaka 15. Matuta yawe na upana wa sentimita 60 na urefu wowote. Sia mbegu katika mistari kwa nafasi ya sentimita 30 mpaka 40 kati ya mistari na kina cha sentimita moja mpaka moja na nusu. Baada ya kupanda, weka matandazo kama vile majani makavu na kisha mwagilia maji asubuhi na jioni mpaka mbegu zitapoota. Kiasi cha kumwagilia hutegemea hali ya unyevu ardhini. Mbegu huota baada ya siku 10 mpaka 15, zikishaota ondoa matandazo.

PITIA
Kilimo Safi cha Mahindi

UTUNZAJI WA SHAMBA:

• Umwagiliaji : Hakikisha udongo umeandaliwa vizuri pia kuna unyevu wa kutosha hasa siku za mwanzo. Karoti zilizokosa maji kwa muda mrefu huzaa mizizi midogo. Pia udongo mkavu ukipata maji mengi ghafla husababisha karoti kupasuka. Hivyo kumwagilia shamba mara kwa mara kuhakikisha udongo una unyevu wakati wote.

• Palizi : Zao hili linahitaji kupaliliwa mara kwa mara. Palilia kwa kupandisha udongo na kuwa mwangalifu ili usikate mizizi.

• Mbolea : Tumia mbolea ya chumvichumvi aina ya Sulphate of Amonia kama mbolea za asili haipatikani. Kiasi kinachotakiwa ni kilo 100 kwa hekta. Weka kilo 50 kwa hekta iwapo mbolea za asili zimetumika. Mbolea iwekwe wakati wa kupunguza miche mara ya pili. Weka katikati ya mistari kwenye mifereji kisha fukia.

• Kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu : – Madoamajani (leafsport) husababishwa na ukungu na hutokea wakati mimea ina urefu wa sentimita 13 mpaka 15. Hushambulia majani na kuyafanya yawe na madoa meusi yaliyochanganyika na kijivu au kahawia. Sehemu zilizozunguka madoa haya hubadilika rangi na kuwa njano.Ugonjwa ukizidi, majani hukauka. Ugonjwa huu huzuiwa kwa kunyunyizia dawa za ukungu kama vile Copper hydroxide, Copper Oxychloride na Cupric Hydroxide.

 Kuoza mizizi (Sclerotinia Rot) : Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia mizizi na majani. Dalili zake ni kama kuoza mizizi na majani. Baadaye sehemu hizi hufunikwa na uyoga mweupe.

• Epuka kustawisha karoti kwenye maeneo yaliyoshambuliwa.

• Nyunyizia dawa za ukungu kama vile Dithane M-45, Blitox,Topsin-M70 na Ridomil.

• Madoa meusi (Black Leaf Spot) : Huu ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia majani na mizizi. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya njano ambayo baadaye hubadilika na kuwa kahawia. Mizizi huwa na madoa meusi yaliyofifia. Ugonjwa huu huweza kuzuiwa kwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalam, kubadilisha mazao na kuepuka kujeruhi karoti wakati wa kupalilia, au kuvuna au kusafirisha.

PITIA
KIPANDE CHA LIMAO KILA SIKU CHATOSHA KUDHIBITI UGONJWA WA SARATANI

WADUDU

• Minyoo fundo :

Minyoo hii hushambulia mizizi na kuifanya iwe na vinundu. Hali hii husababisha mmea kudumaa na kupunguza mavuno. Minyoo fundo huweza kuzuiwa kwa kubadilisha mazao. Baada ya kuvuna usipande mazao ya jamii ya karoti au mazao yanayoshambuliwa na wadudu hawa. Unaweza kupanda mazao ambayo hayashambuliwi na minyoo fundo kama vile mahindi. Pia hakikisha shamba ni safi wakati wote.

• Inzi wa karoti :

Inzi hawa hutoboa mizizi. Wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa kama vile dichlorvos, sapa, diaznon na fenvelerate. Pia badilisha mazao na wakati wa kupalilia pandisha udongo kufunika mizizi.

• Karoti kuwa na mizizi mingi :

Hii hutokea kama karoti zimepandwa kwenye udongo wenye takataka nyingi na usiolainishwa vizuri. Vilevile utumiaji wa mbolea za asili zilizooza vizuri unaweza kusababisha karoti kuwa na mizizi mingi. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kulainisha udongo vizuri na kutumia mbolea za asili zisiooza vizuri.

UVUNAJI

Karoti huwa tayari kuvunwa baada ya wiki 10 tangu kupandwa. Muda huo hutegemea. Wastani wa mavuno kwa hekta moja ni tani 25 au zaidi.

KILIMO CHA KAROTI
FAIDA ZA KAROTI

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

CORONA VIRUS EDUCATIONAL POST

Naomba twende polepole Vyanzo vya vifo duniani na idadi (WHO, 2019) Heart diseases – mil 9.43Stroke – mil 5.73COPD – mil 3.04Pumu – mil 2.96Alzheimer’s

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »