Kilimo cha Kunde

KUNDE – COWPEAS (vigna unguiculata)

UTANGULIZI
Kunde ni zao ambalo linaweza kulimwa kwa ajili ya chakula na bishara ni zoa lenye kiasi kukubwa cha protini na majani yake yanaweza kutumika kama mboga za majani.Ni zao ambalo linatoa mavuno ya Kiasi cha kilogram 500 hadi 1500 kwa ekari.

HALI YA HEWA IFAAYO
Ni zao linalostahimili ukame, Kunde hukubari vizuri katika mwinuko wa mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari.kunde huweza kulimwa katika maeneo yapatayo mvua kidogo kiasi cha milimita 500 hadi 1200 kwa mwaka.Hukuwa vizuri katika joto la nyuzi 28 had 32 C.
3.ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA KUNDE
Huweza kulimwa katika udongo usiotuamisha maji  wa aina tofauti tofauti kuanzia kichanga hadi mfinyazi.Zinaweza kupandwa katika udongo usio na rutuba ya kutosha lakini hustawi vizuri katika udongo wa tifutifu kichanga au tifutifu mfinyanzi au  mchanganyiko wa mfinyazi na kichanga wenye p.H kati ya 6 hadi 7

.MAANDALIZI YA SHAMBA LA KUPANDA KUNDE
Shamba la kunde liandaliwe mapema kabla shughuli ya upandaji kuanza, Kama ni la kukata miti mikubwa miti ikatwe mapema,Kama ni la kufyeka nyasi na miti midogo shughuli hii ifanyike mapema kabla hatua ya kulimwa kwa shamba kwa kutumia trekta,Pawatilla,jembe la ng’ombe au la mikono.shamba lisawazishwe na kukusanywa mabaki ya mimea au visiki na mawe madogomadogo kama yapo.

www.kilimofaida.blogspot.com
MBEGU BORA ZA KUNDE
Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za kunde ambazo zimegawanyika katika makundi makubwa mawili.Kunde zinazosimama na kunde zinazotambaa.

BAADHI YA MBEGU BORA NA SIFA ZAKE
1.TUMAINI

Hukomaa kwa muda wa siku 75 – 90. Aina hii ya kunde husambaa ina maua yenye rangi za zambarau na mbegu zake ni mviringo. Maeneo yanayoshauriwa kupanda ni yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Inahitaji udongo mwepesi wenye rutuba na usiotuamisha maji. Kunde hizi hutoa mazao hadi tani 3 (kilogram 600 – 1500 kwa  ekari)kwa hekta moja. Huvumilia virusi vya mozaiki vinavyotokana na wadudu mafuta wa kunde na bakiteria. Aina hii ya kunde ilizalishwa mwaka 1992 na Kituoa cha Utafiti cha Ilonga kwa ushirikiano na Naliendele.

2.FAHARI

Aina hii hukomaa kwa siku kati ya 75 – 90. Mmea husambaa na maua yana rangi ya zambarau. Mbegu zake ni za mviringo. Hustawi maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Hutoa hadi tani 3 kwa hekta moja (kilogram 600 – 1500 kwa ekari ). Huvumilia magonjwa ya CABMV na mabaka. Fahari ilitolewa mwaka 1982 na Kituo cha Utafiti Ilonga kwa kushirikiana na Naliendele
3.VULI_1
Inakomaa kwa siku 55 – 65. Hukua ka kunyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake ni nyekundu na za mviringo. Inastawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Ikipataiwa matunzo mazuri huto hadi tani 2 kwa hekta moja (Kilogram 450-800 kwa ekari). Vuli – 1 inavumilia CABMV, BP na BB Vuli – 1 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.
4.VULI_2
Inakomaa baada ya siku 65 – 70 baada ya kupandwa inaota ikiwa imenyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake zina weupe uliofifia na ni mviringo. Aina hii husitawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Katika matunzo mazuri aina hii huzalisha hadi tani 3.5 kwa hekta moja(Kilogram 800 -1200 kwa ekari) . Vuli – 2 huvumilia CABMV, BP na BB Vuli – 2 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.

PITIA
Faida zitokanazo na Mapapai

KUPANDA KUNDE
Kunde hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua ili kuziepusha kukauka wakati mvua inaendelea kunyesha.na pia unweza kupanda wakati zao jingine linakaribia kuvunwa au katika shamba lilivunwampunga na lina unyevu wa kutosha.Muda mzuri wa kupanda kunde ni akuanzia mwezi Februari mwishoni hadi Machi na Aprili kwa maeneo ambayo mvua huchelewa kuisha.KUMBUKA mbegu zinazotambaa za kunde zipandwe miezi miwili kabla ya mvua kuisha kwani hizi huchukua siku nyingi kukomaa na Mbegu zinazosimama zipandwe mwezi mmoja kabla ya mvua kuisha.
Kunde huitaji kiasi cha kilogram 4-12 za mbegu kwa ekari.kiasi cha mbegu kitategemea ukubwa wa mbegu,(mbegu kubwa zitahitajika kilogram nyingi) nafasi za upandaji,Ukipanda karibu karibu na mbegu itahitajika nyingi,Ubora wa mbegu katika uhotaji.Zisizoota vizuri huitaji mbegu nyingi zaidi

NAFASI YA UPANDAJI

Unaweza kutumia nafasi zifuatazo kwa kupanda kunde zako
KUNDE ZINASOSIMAMA-Tumia sentimeta 45 hadi 50 mstari hadi msatari na sentimeta 15 hadi 20 shina hadi shina katika mstari /  Sm ( 50 X 20 )
KUNDE ZINAZOSAMBAA-Tumia nafasi ya Sentimeta 70 hadi 75 mstari hadi mstari Kwa sentimeta 25 hadi 30 shina hadi shina katika mstari / Sm ( 75 X 30 )
Panda kwa kufikia kiasi cha sentimeta 2.5 hadi 5 ardhini na tumia mbegu tatu kwa kila shimo na baadaye punguza uache 2 kwa kila shimo kama unauhakika wa mbegu zako unaweza kupanda moja kwa moja mbili mbili kwa shimo

PALIZI  NA KUPUNGUZA MIMEA KATIKA MISTARI

Palilia na Punguza mimea mapema katika shamba lako la kunde.ili ikuwe ikiwa na afya bora

MBOLEA

SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Kama shamba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari moja na uhakikishe mbolea hii imemwagiwa au imenyeshewa na mvua ya kutosha kuiozesha kabla ya kupanda kunde zako na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya  TSP kiasi cha Kg 50 kwa ekari na baadaye kuzia mbolea ya SA kiasin cha Kg 50 kwa ekari.

WADUDU NA MAGONJWA KUNDE

KUDHIBITI WADUDU WAHARIBIFU WA KUNDE
Wadudu waharibifu wa zao la Kunde wako katika makundi mawili:-
1. Kundi la kwanza ni la wadudu wanaoshambulia mimea ikiwa shambani. Ina maana mmea hushambuliwa baada ya kuona hali inapokomaa na kutoa mbegu. Kundi la wadudu hawa lina tabia ya kufyonza (Sap = supu) ya mmea kwenye majani, matawi, mashina, maua hata mbegu hasa zikiwa changa kama vitunda. Njia hii ndiyo pekee kwa wadudu wa kundi hili kujipatia mlo ili waishi na kuzaliana. Katika kundi la pili kuna wadudu wenye tabia ya kukata mashina na kuangusha mimea michanga na wengine hutafuna majani na maua. Zaidi ya uharibifu katika kula mimea, wadudu wengi ni hifadhi ya viini vya magonjwa ya virusi.

PITIA
SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO

2.Kundi la pili ni la wadudu waharibifu baada ya mavuno kuwekwa ghalani. Athari ya wadudu hawa inapelekea wakulima kupoteza chakula ghalani pia kupunguza chakula ghalani pia kupunguza ubora wa mazao yanapopelekwa sokoni mfano Mahindi yanapofunguliwa soko lake ni duni. Jamii za wadudu na athari zao zinaelezwa katika aya zifuatazo:-

1. KUNDE:

(ii) Foliage beetle (Ootherca mutabilis)

Wadudu hawa hushambulia mimea ya kunde baada ya mbegu kuota (Seedling stage). Wakiwa kwenye hatua ya mdudu kamili (adult stage) hushambulia majani kwa kula sehemu kati ya vihimili vya majani (area between leaf veins).

Mashambulizi ya wadudu wengi husababisha mmea kupoteza majani yote na hatimaye mmea kufa.
Kuzuia jamii ya wadudu hawa:
Dawa za chemikali aina ya endosulfan, Karate n.k. huagamiza mashambulizi kwa mpulizo mmoja.

(i) Aphids (Aphis gaccivora)

Hawa ni kati ya wadudu wenye kusababisha hasara kubwa katika zao la kunde. Wanapendelea kula mvunga wa majani (under leaf), sehemu za vishina na hata vitumba (pools) vya mbegu. Athari za mashambulizi: Mmea hudumaa, majani husinyaa na kukunjamana pia hupukutika kabla hayajazeeka hatimaye mmea hufa.

Kuzuia Aphids: Dawa za chemikali aina ya phosphomiolon na dimethoate kwa cc 40 katika lita 10 za maji.

(iii) Flower thrips (Megalurothrips sjostedti)

Hatua ya mdudu kamili hushambulia maua. Mimea ikishambuliwa sana haizai matunda kwasababu maua yameharibika. Mashambulizi yakiwa makubwa zao lote huangamia.

Kuzuia: Kwa kutumia chemikali aina ya Cypermethrin – kiwango cha cc 40 katika lita 10 za maji.

(iv) Podborers (Maruca testulalis)

Wadudu hawa hula mvungu wa majani, ganda la shina na vitumba vya mbegu katika hatua ya kukomaa. Athari: Mmea hudumaa, umbo la majani huharibika (olistorted leaves) na hupukutika kabla ya kuzeeka. Mimea mingi hasa michanga hufa.

Uzuiaji: Kwa kutumia chemikali aina ya phosphomidon na dimethoate kwa kiwango cha cc 40 katika lita 10 za maji.

(v) Podsucking bugs (Anoplemenia,dentires, Acanthomia SPP)
Wadudu hawa hushambulia mikunde katika hatua ya kuweka vitumba (pods). Hasara, inayosababishwa, na wadudu hawa hufikia 90%. Madhara makubwa huletwa na hatua ya wadudu kamili (adult stage/ kwa kufyonza “Sap = Supu” ya vitumba teketeke ambavyo husinyaa na kukauka bila kukomaa wala kuwa na mbegu.

Kuzuia: Kwa kutumia chemikali za Endosulfan au dimethoate kwa kiwango cha cc 40 katika lita 10 za maji.

(vi) Cowpea storage weevils (Callosobrunchus macuhates callosobrun ams chinensis).

www.kilimofaida.blogspot.com
Mashambulizi ya wadudu hawa wawili huanzia shambani wakati kunde zimekaribia kukomaa. Wadudu hutaga mayai kwenye vitumba vilivyokomaa. Mayai yakiangauliwa, funza hupenya kupitia kwenye matobo yanayosababishwa na wadudu wengine. Funza wakianguliwa hushambulia mbegu na uharibifu hufikia 70% ya mbegu safi.

PITIA
NAMNA SAHIHI YA KUWALISHA KUKU WA MAYAI.

Kuzuia: Tumia chemikali aina ya Acteric Super Dust 100 mg za unga wa dawa katika 10 Kg za mbegu safi (Seed grain)

NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA YA ZAO LA KUNDE:
Magonjwa hatari yanasababishwa na vimelea vya virusi na vya bacteria aina tabia na uzuiaji wa magonjwa haya ni kama ifuatavyo:-

(i) Cowper aphid-born mosaic virus

Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hupelekea mkulima kupata hasara ya 13 – 87% ya zao. Dalili za ugonjwa huu ni michirizi ya rangi ya kijani iliyochanganyika na njano au ya ugoro (mosaic & mottling) kwenye majani.

Kuzuia: Kwa kutumia aina za kunde zenye kustamili ugonjwa huu kama Tumaini, Fahari na Vuli.
(ii) Bacterial blight (Xanthomonus vignicola)

Ugonjwa huu hushambulia sana miche na kiasi cha 60% ya miche yote hufa.

Dalili: Majani,vitumba au mashina ya mimea  iliyoathirika huwa na vidonda vyenye rangi kati ya njano ya chungwa. Katika mashambulizi makubwa vidonda vidogo huungana (merge – coleasce) na eneo kubwa la majani huharibika. Ugonjwa hushamiri katika kipindi cha mvua nyingi (Kifuku) na umwagiliaji kwa juu (Overhead irrigation).

Kuzuia: Tumia mbegu zinazovumilia ugonjwa kama Tumaini, Fahari na Vuli.

(iii) Bacterial blight (Xanthomonas Spp)

Ugonjwa hushambulia aina ya kunde pori na zinazolimwa.

Dalili: Vidonda vidogo huonekana uvunguni mwa majani. Katika mimea dhaifu (more susceptible) vidonda huungana na kuwa na umbo la duara lenye ukubwa wa: kipenyo cha 1-3 cm. Mwanzoni vidonda huonekana kufutuka mvunguni mwa jani kadiri vinapokomaa huwa na rangi ya kahawia upande wa juu na majani. Baada ya muda vidonda hukauka na hubakisha migonyeo sehemu zilizoathirika. Majani mengi yaliyathirika hubadilika kuwa njano na baadaye huanguka / hupukutika.
Ueneaji: Ugonjwa huenea kwa kasi wakati wa kifuku (mvua nyingi) na umwagiliaji unapokuwa wa juu. (overhead irrigation). Kimelea cha bacteria huyu hudumu kwenye punje (mbegu). Kwa hiyo mbegu za namna hii huota zikiwa na viini vya ugonjwa.
Kuzuia: Kutumia mbegu zenye kustahimili ugonjwa huu kama Tumaini, Fahari na Vuli
(iv)Powdery Mildew (Ukungu)

Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia au kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.

Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu (Fungicide).
anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na hali halisi ya ugonjwa.

UVUNAJI
Vuna kunde zako baada ya kukomaa na kuanza kukauka kwa kung’oa mashina au kuchuma kwa mikono.Kisha zisambaze kunde zako au amshina yako juani ili zikauke zaidi na uweze kuziondoa kwa urahisi kutoka katika maganda yake.Unaweza kuondoa maganda uyake kwa mkono au kuupigapiga taratibu au kwa kutwanga katika kinu taratibu bila kuzipasua kunde.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Pilipili

Pilipili   hoho  ni  moja  ya  mazao   ya  viungo  ambalo  hulimwa  kwa   wingi    Mikoa  ya   Arusha,  Kilimanjaro,  Tanga,  Morogoro, Mbeya  na   Iringa. Zao   hili   hutumika    kama 

Read More »

IJUE TANGAWIZI NA FAIDA ZAKE

Tangawizi ni zao ambalo hustawi sehemu mbalimbali duniani na hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali, dawa kwa tiba ya magonjwa ya binadamu na wanyama na

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »