Kilimo cha Mihogo (Cassava)

KILIMO BORA CHA MIHOGO

Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 – mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

TEKNOLOJIA ZILIZOPO
Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
Naliendele
Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

Kiroba
Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

Mbinu bora za kilimo cha muhogo
Uandaaji wa shamba
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
– Kufyeka shamba
– Kung’a na kuchoma visiki
– Kulima na kutengeneza matuta
· Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.
· Upanadaji
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
– Kulaza ardhini (Horizontal)
– Kusimamisha wima (Vertcal)
– Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

PITIA
Dondoo za Ufugaji wa Kuku bora wa Nyama

Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.

· Palizi:
– Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
– Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
– Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
– Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

· Uvunaji:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

· Usindikaji bora
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
– Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
– Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
– Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

Njia bora za usindikaji
– Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
– Kwa kutumia mashine aina ya chipper
– Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

PITIA
Kilimo cha Kunde

Matumizi ya Muhogo
– Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
– Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
– Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

[​IMG][​IMG]

Utangulizi
Mihogo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kigoma, Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuna, Tanga, Morogoro, Mbeya, na Shinyanga. Muhogo una kiwango kikubwa cha wanga ukilinganisha na nafaka (zaidi ya asilimia 40 kuliko mchele, na zaidi ya asilimia 25 kuliko mahindi). Majani yake hutumika kama mboga na yana virutubishi muhimu hususan vitamini B na protini.
Uzalishaji wake ni wastani wa tani 1,292,000 kwa mwaka. Ili kupata mazao mengi na bora ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora cha mihogo hasa zifuatazo:

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Uzalishaji
Kuchagua aina ya mbegu

 • Chagua mbegu kufuatana na mahitaji ya soko, zilizo safi zinazostahimili magonjwa, wadudu waharibifu na zenye uwezo wa kutoa mazao mengi na bora.

Palizi

 • Palilia ili kupunguza ushindani wa virutubishi kati ya mmea na magugu.
 • Palilia na kupandishia udongo kwenye mashina.
 • Palizi ifanyike mara kwa mara mpaka mihogo inapokomaa.

Kudhibiti magonjwa na wadudu
Muhogo hushambuliwa na wadudu waharibifu kama vidung’ata, vidugamba, mchwa na magonjwa kama batobato na ugonjwa wa michirizi ya kikahawia. Visumbufu hawa wanaweza kusababisha upotevu wa mazao kwa zaidi ya asilimia 90. Hivyo ni muhimu kukagua shamba mara kwa mara ili kuona kama kuna mashambulizi na kuchukua tahadhari mapema.

Maandalizi kabla ya kuvuna
Kukagua shamba

 • Kagua shamba ili kuhakikisha kama muhogo umekomaa. Kwa kawaida muhogo hukomaa katika kipindi cha miezi 9 hadi 24 tangu kupanda kutegemea aina na hali ya hewa. Wakati huo muhogo huwa na unyevu wa asilimia 60 na wanga asilimia 35.
PITIA
KANUNI 5 MUHIMU ZA KUFANYA KILIMO BORA CHA MAHINDI

Dalili za muhogo uliokomaa

 • Udongo unaozunguka shina hupasuka.
 • Mti wa muhogo huonekana kupevuka.
 • Muhogo uliokomaa ni mnene na ukiutafuna utahisi wanga mwingi na maji kidogo.

Kuandaa vifaa vya kuvunia, kubeba, vyombo vya usafiri, na vifungashio

Vifaa vya kuvunia na kubeba

 • Jembe, Panga, Vikapu, Matenga, na Magunia

Vifaa vya kufungashia

 • Maboksi ya mbao/plastiki, viroba, Matenga

Vyombo vya usafiri

 • Baiskeli, Matoroli, Mikokoteni, Magari na matela ya matrekta.

Kuvuna
Ni muhimu kuvuna mapema ili kupunguza uharibifu unaoweza kusababishwa na mashambulizi ya magonjwa na wadudu waharibifu. Kabla ya kuvuna matawi yote yakatwe ili kurahisisha uvunaji.

Njia ya kuvuna muhogo
Chimbua shina la muhogo kwa kutumia jembe na ng’oa muhogo wote kutoka ardhini. Tenganisha muhogo na shina kwa kutumia panga kali.

Utayarishaji, Hifadhi na Usindikaji wa Mazao ya Mizizi baada ya Kuvuna

Tahadhari
Epuka kukata muhogo wakati wa kuvuna kwani mihogo iliyokatwa au kuwa na majeraha huharibika mapema, kutokana na kuingiwa kwa urahisi na vimelea vya magonjwa.

Kuchambua Na Kusafisha

Kuchambua
Lengo la kuchambua ni kuondoa mihogo isiyofaa, iliyooza na iliyokatwa vibaya na kuharibika.

 • Mihogo iliyooza isitumike kwa chakula bali ifukiwe.
 • Mihogo iliyokatwa au yenye michubuko itumike kwa chakula mapema iwezekanavyo au ioshwe vizuri na isindikwe mara moja.
 • Mihogo iliyodumaa itumike kwa chakula cha mifugo.

Kusafisha na kuimarisha maganda

Kusafisha
Mihogo iliyovunwa huoshwa mara tu baada ya kuvuna ili kuondoa udongo na uchafu mwingine. Mihogo ambayo haikuoshwa vizuri hupunguza ubora wakati wa kukausha na kusindika. Mihogo huoshwa kwa maji na kurudiwa hadi maji yanapokuwa safi na kuona kuwa mihogo imetakata.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

ZIFAHAMU AINA NNE ZA MTAMA

Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »