Kilimo cha Mpunga Tanzania

MPUNGA
Hili ni zao la chakula linalolimwa kwa wingi kwenye maeneo ya ukanda wa joto.

Zao hili linastawi zaidi kwenye udongo wa tifu tifu na eneo lenye maji ya kutosha. Baadhi ya maeneo (,Mikoa) yanayolima zao hili kwa wingi na kulitumia kama zao la biashara ni Morogoro,Mbeya, Tabora, singida na shinyanga.

NAMNA YA KULIMA MPUNGA
Kwa Tanzania mpunga huzalishwa kwa mifumo ya aina mbili. Yaani kumwaga/ kusia na kupandikiza miche.

1: KILIMO CHA KUMWAGA/ KUSIA
Huu ni mfumo wa kulima mpunga kwenye maeneo yenye uhaba wa maji. Katika kilimo hiki mkulima hukwatua shamba na kulitifua tifua/ kupiga piga mabonge na kuanza kumwaga mpunga katika eneo lote la shamba. Baada ya kumwaga mpunga hutifua tifua tena ili kuufukia mpunga kwenye udongo tayari kwa kuoteshwa.

Wakati mwingine kama eneo lina maji basi mkulima huloweka mbegu kwa masaa 24, huiopoa na kuivundika kwa siku tatu. Ikianza kuota basi hubebwa na kumwagwa shambani bila kufukiwa tayari kwa ukuaji. Katika umwagaji huu hatua ya kukatua na kuvuruga/ kutifua eneo haikwepeki. Baada ya kumwaga mkulima anatakiwa kuhakikisha ulinzi wa ndege unakuwepo.

Kutokana na maendeleo ya teknologia kazi zote zinzfanywa na mashine kwa wenye mitaji. Mfano kazi ya kukatua hufanywa na trekta, kazi ya kutifua / kuvuruga hufanywa na trekta na pawatila zenye rota. Vile vile kazi ya kumwaga mpunga hupandikizwa kwa kutumia mashine maalumu.

Maeneo mengi nchini hutumia mfumo huu lakini maeneo maarufu ni Morogoro na Kyela Mbeya.

GHALAMA ZA UZALISHAJI KWENYE KILIMO CHA KUMWAGA

Ghalama za kilimo hiki ni kama ifuatavyo.

a) Kukodi shamba ……. Tsh 50,000 – 100,000 kwa heka kutegemeana na location kwa Moro ni 50,000 kwa heka.

PITIA
Kilimo chenye Tija

b) kukatua shamba kwa disc ……. Tsh 40,000 – 65,000.

c) kumwaga ……..Tsh 30,000

d) Kung’olea/ kupalia ……..Tsh 30,000- 60,000

e) kuvuna ……… Tsh 30,000 – 60,000

Ghalama nyingine ni roundup, 2-4D ambazo ni Tsh 30,000- 45,000, kufukia mpunga kwa rota 30,000 – 50,000, Mbegu debe 2-3 kwa Tsh 20,000/30,000.

Jumla ya ghalama za uzalishaji kwa kilimo cha kumwaga kwa wastani ni Tsh 200,000- 300,000.

Kipato kwa kilimo cha kumwaga wastani ni gunia 4- 8.

2: KUPANDIKIZA MICHE
Huu ni mfumo ambao hutumia mbegu iliyooteshwa kwenye vitalu katika kupandikiza mpunga. Mbegu hii huandaliwa kwa namna mbali mbali kama vile.

i) kumwaga mpunga mkavu moja kwa moja. Katika njia hii mkulima huandaa kitalu, na kumwaga mpunga alioutenga kwaajili ya mbegu. Baada ya kumwaga humwagilia maji ili mpunga upate maji tayari kwa kuota. Kitalu ili kilete manufaa inashauriwa kifunikwe kwa turubai la mifuko ya maroba au nyasi.

Kipimo kizuri cha kitaru kwa heka moja ni hatua/ mita 10× 15 na mpunga ni debe 3 kwa mpunga usio na taka taka. Ukikata kitaru cha 10×15 basi unatakiwa kugawanya Mara tatu yaani upate vitaru vya 3×10 ambavyo utamwaga debe moja la mpunga kwa kila kitaru.

ii) Kumwaga mpunga uliooteshwa
Katika mfumo huu, mbegu ya mpunga huandaliwa na kulowekwa kwa masaa 24. Baada ya kulowekwa huvundikwa kwenye mfuko au katika kifaa chenye sifa sawa na hicho kwa siku tatu na kwenda kumwaga. Kitaru kitakuwa na sifa sawa na zile za 2(i) lakini hapa lazima kiwe na unyevu wa kutosha kama sio ubichi kabisa ili mbegu isiungue. Kitaru kisiwe na maji ili kuepusha mbegu kuoza.

PITIA
MFAHAMU KUKU AINA YA KUCHI

Kwa wanaotumia planter wao hutumia njia hii lakini wao huvundika kwenye trei au kumwaga kwenye vitalu vinavyotandikwa kitambaa au kitu mfano wa kapet maalum. Hapa sitaeleza sana maana hapa nchini ni wakulima wachache wanaotumia planters.

Kwa kawaida miche ya mbegu huwa tayari kupandikizwa baada ya siku 21 na haishauriwi kuipandikiza ikiwa na siku 45. Kuna wale watu wa shadidi mbegu zao huwa tayari kupandwa ndani ya siku 7-14.

Mfumo huu wa kuwatika mbegu unatumiwa sana maeneo mengi yanayoendesha kilimo cha umwagiliaji hasa Mbarali (Mbeya), na maeneo mengine yenye mvua za uhakika.

GHALAMA ZA UZALISHAJI KWA HEKA

a) kukodi Shamba …… Tsh 100,000 – 300,000 kutegemeana na location

b) kukatua ……. Tsh 60,000- 70,000

c) kukata matuta …… Tsh 15,000

d) kuvuruga/ kuchabanga …….Tsh 60,000- 70,000.

e) Kupanda …… 60,000- 90,000

f) kungo’olea/ kupalia …… Tsh 30,000- 45,000

g) kulinda/ kuamia ndege….. Tsh 30,000- 40,000

h) kuuvuna …..Tsh 200,000 kwa combine/ 150,000 kwa kutumia nguvu kazi.

Ghalama nyingine ni mbegu debe 3 (30,000), 2-4D (10,000-15,000), mbolea mifuko 2-4 ( 120,000- 200,000), kuandaa kitalu cha mbegu 10,000.

Jumla ya ghalama za Uzalishaji kwa heka kwa wastani ni Tsh 500,000 bila mbolea na 700,000 pamoja na mbolea

Kipato ni gunia 10 – 35 kwa heka kutegemeana na eneo na matunzo.

MATUMIZI YA CHEMIKALI KWENYE KILIMO CHA MPUNGA.

Kilimo cha mpunga hutumia chemikali za aina mbali mbali kama vile.

1. Dawa za kuunguza majani aina zote.

Hizi dawa hutumika kuangamiza majani yote shambani ili shamba likatuliwe au kuvurugwa. Dawa zinazotumika na muda wa kuisha makali shambani ni kama ifuatavyo; Round up ….. Siku 21, melaxone…. Siku 7 na chemikali nyingine zenye sifa sawa na hizo.

PITIA
UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU

2: Dawa za kuua majani yenye asili ya majani mapana na ndago. Hizi hufahamika kama 2-4D, hutumika kudhoofisha na kuua kabisa magugu yasiyotakiwa kwenye mpunga. Majani yenye asili ya mpunga hayafi ndio maana inashauriwa baada ya kupiga dawa ungolee ili kuondoa magugu yasiyokufa kwa dawa. Dawa hizi zipigwe siku 21 toka siku ya kupanda mpunga na kwa wanao mwaga wapige siku 28 -30 toka siku ya kumwaga. Haishauriwi kupiga awamu mbili au zaidi kwani licha ya kuua magugu hudhoofisha mpunga.

3: Dawa za kuzuia magugu kuota.

Hizi ni dawa ambazo hupigwa siku ya tatu baada ya kupanda mpunga wakati shamba likiwa katika hali ya tope tope. Huzuia mbegu za magugu zisipasuke na kuota. Haishauriwi kupigwa kwenye mpunga wa kumwaga maana hatà mpunga hautaota . baadahi ya dawa hizo ni RILO R500, na Maguguma na dawa nyinginezo zenye sifa sawa na hizo.

4:Mbolea

Kuna aina mbali mbali za mbolea lakini kwa kifupi ni

DAP… Kupandia, hupigwa siku saba toka siku ya kupandikiza au siku ya kupandikiza.

UREA……Kukuuzia hupigwa siku 21 toka siku ya kupandikiza.

S.A ….. Mbolea ya magadi hupigwa pamoja na mbolea za kukuuzia au kuzalishia.

CAN….. mbolea ya kuzalishia hupigwa wakati mpunga umeanza kufunga(mimba)

AMIDAS….. Kukuuzia, kuondoa magadi, kuzalishia.

Utaratibu wa upigaji mbolea ni siku 14 toka mbolea ya awamu ya mwanzo.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo Cha Maharage Ya Njano.

Kilimo cha maharage ni rahisi na kinalipa sana kikifanyika kwa utaalamu. Gharama nafuu na ushindani wa soko sio mkubwa sana. Huhitaji kusafiri, kinachofanyika ni kuwaita

Read More »

Kilimo cha Pilipili Manga

Kilimo cha Pilipili Manga, kuanzia mbegu bora, magonjwa, utaalamu mpaka masoko Katika kuabarishana fursa lukuki zilizoko kwenye maeneo tofauti tofauti ndani ya inchi yetu leo

Read More »
Bata Dume

UFUGAJI BORA WA BATA

UFUGAJI BORA WA BATA : Wafugaji wengi wadogo wa bata hapa nchini hufuga bata machotara ambao wamechanganyika damu aina mbalimbali. Matumizi makubwa ya bata hawa

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »