Kitambue Kilimo cha Kahawa

UTANGULIZI

Kahawa ni miongoni mwa mazao ya biashara ya biashara yanayoliingizia taifa mapato mengi, kahawa ni zao la pili la biashara baada Tumbaku.

Asili:kwa mujibu wa wataalam asili ya kahawa ni katikati ya Ethiopia.

kusambaa: kutoka Ethiopia kahawa ilisambaa hadi India, Uturuki, Italia, Uingereza na Africa mashariki

  1. Tanzania–Hulimwa sehemu tofauti tofauti ikiwemoMiteremko ya Mlima Kilimanjaro na kusini mwa Mlima Meru, Nyanda za juu za Ngorongoro, Miteremko ya Milima ya Uluguru, Kaskazini mwa Mkoa wa Mara (Hususani wilaya ya Tarime), Mkoa wa Kigoma (Wilaya za Kasulu, Kibondo), Mkoa wa Mbeya wilaya za Rungwe, Mbeya, Mbozi and Na Tanga katika miteremko ya Milima ya Usambara.
  2. Kenya– Hulimwa maeneo ya Ol Donyo Sabuk, Machakos, Nakuru na Rift Valley.
  3. Uganda– Hulimwa Maeneo ya Bugisu Mlima Elgon, Kigezi, Ankole, Toro na Nile

MVUA NA MAHITAJI YA MAJI

Kahawa kwa sasa hulimwa sana katika maeneo ya kitropikia,

JOTO; Kahawa inahitaji jotoridi la nyuzijoto 17 hadi 23

Pia kahawa huitaji kiasi cha mvua milimita 1500 – 1200 mm kwa zaidi ya miezi 8

Kahawa ni miongoni mwa mazao ambayo huathirika na jua kali hivyo ni muhimu sana kupanda miti ya kivuli shambani (wengi hupanda migomba kwa sababu hiyo)

PH-kahawa husitawi vizuri kwenye udongo wenye kiwango cha Uchachu wa pH ya 4.5 hadi 5.6, pia udongo wenye uwezo wa kuhifadhi maji lakini kahawa hustawi vizuri sana kwenye udongo wenye asili ya volicano na udongo ambao haujawahi kulimwa (virgin soil)

KUANDAA SHAMBA

Katika kuandaa shamba la kupanda kahawa miti mikubwa na miamba mikubwa hung’olewa

Kwa maeneo ambayo yanaweza kutifuliwa mbolea kama phosphorus inatakiwa kuwekwa mara nyingi shambani kabla ya kuamishia mche shambani. Na maeno ambayo hapawezi kutifuliwa mashimo huweza kuwekwa na buldoza.

PITIA
Kahawa Inayoleta Utajiri

Mashimo ni lazima yawe makubwa na yenye kina kirefu  kuwezesha kutovunja mizizi wakati wa kuhamishia mimea shambani.

Kahawa hupandwa kwa kutumia miche ambayo imekuzwa kwenye vifuko.

Nafasi ya kupada ni 3m x 3m kwa kiasi cha mimea 1280 kwa hekta (/ha).

— Miti ya kivuli kama vile Leucaena au migomba inaweza kupandwa kwa 6m x 6m.

MBOLEA

— unatakiwa kuzingatia kutumia udongo wenye rutuba ya kutosha.

— Unaweza pia kutumia mbolea ya asili.

KUVUNA

— Kahawa hua tayari kuvunwa miezi 8 hadi 9 kutoka kipindi ambacho maua ya mechomoza unatakiwa kuvuna matunda ambayo yamesha yamesha iva na kubadilika rangi kua nyekundu .

— Ukivuna matunda ambayo bado hayaja iva usababisha kahawa kua chungu sana

— Katika maeneo ya kitlopikia unaweza kuvuna mara moja kwa mwaka.

MAGONJWA NA WADUDU

Magonjwa ya tunda /Coffee Berry Disease (CBD) (Colletotrichum Kahawae)

Ugonjwa huu pia hujulikana kama Chulebuni

Tokeo la picha la coffee berry disease

Chulebuni ama kama ujulikanavyo kama Coffee Berry Disease (CBD), ni ugonjwa mbaya sana na huenea kwa kasi. Mbuni ulioshambuliwa haufi ila mkulima anaweza kupoteza mpaka asilimia 90 ya mavuno kama hatazingatia namna bora ya kuuzuia. CBD huathiri matunda ya kahawa hasa kanda za juu na kati.Ushambuliaji ni mkubwa zaidi wakati wa masika kwani CBD hupenda hali ya unyevu na hali ya baridi kwa sababu husababishwa na vimelea aina ya fangasi.Dalili na madhara ya CBD:

* CBD hushambulia mibuni katika hatua tatu muhimu ambazo ni:
. Maua yanapochanua.
. Punje zikiwa changa na laini.
. Punje zinazoiva.* Madhara makubwa hutokea walati punje zikiwa changa na laini amnapo:
. Maua yaliyoshambuliwa hunyauka na kuanguka.
. Vidonda vyeusi na vilivyobonyea huonekana kwenye matunda yaliyoshambuliwa. Mengi huoza na kudondoka. Yaliyobakia hukaukia kwenye mti na kuwa chanzo cha uambukizaji kwenye mavuno ya msimu unaofuata.* Matunda yaliyoiva hukaukia kwenye matawi na huvunwa kama buni.* Hupunguza zao kwa asilimia kati ya 30 na asilimia 60 wakati mwingine hufikia hadi asilimia 90.* Kudhibiti CBD hufikia hadi asilimia 35 ya gharama za uzalishaji.* Hupunguza ubora wa kahawa kwa kiasi kikubwa.

PITIA
Kilimo cha Pilipili

Jinsi ya kuzuia chulebuni (CBD):
– Panda aina mpya ya kahawa inayohimili mahambulizi ya Chulebuni ambayo ni mkombozi dhidi ya ugonjwa huu hatari.
– Punguza kivuli shambani.
-Kata matawi kwa wakati na sahihi. Ondoa maotea mara kwa mara.
– Ondoa masalia ya buni zilizoathirika na teketeza kwa moto.
– Kwangua magamba kwenye mashina machafu ya kahawa.
– Anza kunyunyizia vizuia kuvu kukinga matunda machanga ndani ya wiki tatu kabla ya mvua za msimu kuanza.
– Hamasisha majirani kuzuia chulebuni kwa wakati mmoja.

Kutu za majani/Coffee Leaf Rust (Hemileia Vastatrix)

— Huu ni ugonjwa wa fangas ambayo hushambulia majani tu na unaweza kuzuia kwa kuwekea nyasi kuzunguka mmea wakati wa kupanda na kuweka mbolea na unatakiwa kupulizia dawa ya fungusi (fungiside).Madhara yake:
. Kutu ya majani hupunguza eneo la jani la kutengeneza chakula. Pia hudababisha kupukutika kwa majani yanayolisha matunda na kukuza mmea.
. Kwa hali hiyo husababisha madhara ya mmea kutoa punje ndogo zenye ubora hafifu.
. Ugonjwa ukishamiri hukausha matawi, shina zima na hatimaye mti mzima kufa.Hali zinazochangia kuenea kwa kutu ya majani:
– Unyevu wa hewani unapokuwa zaidi ya aslimia 80 na unapoambatana na kivuli cha kupita kiasi kwenye shamba.
– Msongamano wa machipukizi na matawi katika mti wa kahawa.Jinsi ya kudhibiti ugonjwa wa kutu ya majani:
– Punguza kivuli kuzunguka mti wa kahawa.
– Pogolea machipukizi na matawi katika mti wa kahawa.Kuzuia kutu ya majani:-Panda aina mpya zinazovumilia magonjwa ya kutu ya majani na chulebuni.-Boresha huduma muhimu ikiwa ni pamoja na lishe ili kuongeza uvumilivu wa magonjwa hususani ugonjwa wa kutu ya majani.-Tumia viua kuvu kwa wakati na vipimo sahihi. Unyunyiziaji wa kwanza ufanywe ndani ya wiki tatu kabla ya mvua kunyesha, na kuendelea hadi mara tatu mpaka nne kwa msimu.– Shirikisha na majirani kudhibiti kutu ya majani.

PITIA
KILIMO BORA CHA SOYA

Ubuli unga/Coffee wilt disease, Pia inajulikana kama Tracheomycosis (Gibberella xylarioides)

— Hii ushambulia sehemu za chini za mmea na hushambulia zaidi mimea midogo, pia unaweza kuzuia kwa kutumia dawa za fangasi.

Pia unatakiwa

  1. Kuweka mazingira safi
  2. Mbolea ya kutosha
  3. Maji

Ili kuweza kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA PAMBA

Pamba ni moja la zao ambalo pia hurimwa nchini Tanzania, hukuzwa kwa kutumia tunda lake pia hilo tunda hua na nyewele nyeupe, hizo nywele ndio

Read More »

KILIMO CHA UYOGA

Kwa kuwa #uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za #kuoteshea, urahisi wa

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »