KUFUGA KUKU WA KIENYEJI KUNALIPA

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......
Kuku wa Kienyeji wa Mayai
KUFUGA KUKU WA KIENYEJI KUNALIPA
KUFUGA KUKU WA KIENYEJI KUNALIPA

KUFUGA KUKU WA KIENYEJI KUNALIPA : Kufuga kuku wa kienyeji ni jadi ya Watanzania waishio vijijini. Aghalabu katika kila kaya utakuta idadi ndogo ya kuku au bata, mifugo hiyo ni sehemu ya shughuli za wakulima wenyeji. Hesabu isiyo rasmi ni kwamba nchini mwetu kuna takribani millioni 20 ya kuku wa kienyeji. Kuku wa kigeni ambao kwa kawaida hufugiwa sehemu za mijini, wanakisiwa kuwa milioni mbili na nusu.

Ingawa kuku wa kienyeji hukua polepole sana, wadogo kwa umbo, pia hutoa mayai machache, lakini wanazo sifa za kipekee. Kwa kawaida hujitafutia chakula chao kutoka kandoni mwa makazi ya watu, wanavumilia sana magonjwa, nyama na mayai yao yana ladha nzuri sana. Sifa hizi husababisha bei ya kuku hawa kuwa kubwa kuliko ya kuku wa kigeni.

Uzito wa kuku wa kienyeji aliyekomaa ni kati ya kilo 0.75 na 1.0. Anao uwezo wa kutaga mayai 40 hadi 60 kwa mwaka, lakini akitunzwa vizuri idadi inaweza kuongozeka maradufu. Kwa ulinganifu, uzito wa kuku wa kigeni ni kati ya kilo 1.5 na 2.5, aidha anao uwezo wa kutaga mayai 200 hadi 250 kwa mwaka.

Vema ieleweke kwamba umbo dogo la kuku wa kienyeji, na uchache wa nyama na mayai, huchangiwa na matunzo hafifu, hasa kutopata chakula cha kutosha. Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa faida, una kanuni zake. Kutumia jogoo lenye sifa nzuri, kujenga banda lenye nafasi ya kutosha, lililo imara na safi, kulisha kuku chakula wanachostahili, kuzuia na kutibu magonjwa.

BANDA LA KUKU

Kuku wanahitaji kuishi kwenye mazingira yanayostahili. Banda liwe na ukubwa wa kutosha, linalopitisha mwanga na hewa, lisilovuja wala kuwa na hali ya unyevunyevu sakafuni. Ni vema kusiriba kuta za banda ili kuzuia nyufa ambazo ni maficho ya wadudu waharibifu, kwa mfano viroboto. Vilevile sakafu isiribwe kwa udongo wa mfinyanzi, mfugaji akiwa na uwezo asakafu kwa kutumia saruji.

PITIA
UFUGAJI WA KAMBARE KITAALAMU I

Kuta za banda zaweza kujengwa kwa kutumia matofali ya saruji, au ya kuchoma, au miti / fito / mabanzi. Sehemu zenye hali ya joto sana, vema kuku wajengewe uchaga umbali wa nusu mita kutoka kwenye sakafu. Hii itaruhusu upitishaji wa hewa nyingi ndani ya banda na kupunguza uwezekano wa kuwepo kwa wadudu. Banda lenye mita za mraba 10 linatosha kufugia kuku 40 hadi 60.

KUBORESHA KUKU WA KIENYEJI

Kuku wa kienyeji wana sifa ya kuvumilia magonjwa, uwezo mkubwa wa kuatamia mayai, na kuangua vifaranga vingi na kuvilea. Pamoja na sifa hizi, nyama yake huwa ndogo, pia mayai yake ni machache. Ili kuongeza sifa ya kuku wa kienyeji, inashauriwa kupandisha majike kwa kutumia majogoo aina ya kigeni. Mzao wa mchanganyiko huu, utakuwa bora zaidi. Iwapo ni vigumu kupata jogoo wa kigeni, fanya uchunguzi mahali ulipo ili upate jogoo wa kienyeji mkubwa na sifa zinazotakiwa. Jogoo mmoja anaweza kuhudumia wastani wa majike 10.

Kuku anao uwezo wa kuhatamia mayai 12 hadi 15 kwa mara moja. Kiota cha kuhatamia mayai kitayarishwe mapema
kabla utagaji haujaanza. Tenga sehemu ya kuweka kiota, izungushie wavu ili kulinda mayai yasishambuliwe na maadui. Kuku akijitengenezea kiota mahali manapofaa, bora umuache atagie hapohapo. Kila baada ya kuangua, kiota kisafishwe vizuri, kisha sehemu hiyo inyunyiziwe dawa ya kuondoa vijidudu kama utitiri na viroboto.

Vifaranga vilivyoanguliwa inabidi vitunzwe vizuri. Vipatiwe chanjo dhidi ya magonjwa kama mdondo, mahepe na gumboro, na dawa ya kuzuia minyoo. Hakikisha kuku mwenye vifaranga anawekwa sehemu iliyo salama ili visishambuliwe na mwewe, kunguru, vicheche, nakadhalika.

CHAKULA CHA KUKU

Mfugaji anaweza kuchagua kati ya njia hizi tatu tunazoshauri.

PITIA
UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU

1.Kununua chakula kilicho tayari kwa nfano;

Broiler starter – inafaa kwa vifaranga wote – kuanzia kuzaliwa hadi kukaribia kutaga.

Layers mash – kwa kuku wakubwa wanaotaga au wanaokaribia kutaga.

2. Njia ya pili ni kutumia chakula (concentrate) kwa mfano, Farmers concentrate kutoka Farmers centre, kwa viwango vifuatavyo:

Broiler concentrate – Inafaa kwa vifaranga pamoja na mama yao kwa wiki za mwanzo kuanzia wanapozaliwa hadi kuanza kutaga.

• Changanya kipimo kimoja kwa vipimo vitatu vya pumba ya mahindi. Kwa mfano, kopo moja kwa kopo tatu, au debe moja kwa debe tatu.

• Layers concentrate – Inafaa kuwapa kuku wanaotaga katika kipimo hicho hicho cha 1:3

3. Njia ya tatu ni kujitengenezea chakula mwenyewe, kwa mfano ufuatao.

UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU
UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU

DOKEZO JUU YA KUJITENGENEZEA CHAKULA CHA KUKU

Pumba za mahindi pamoja na vichanganyio vyingine ni lazima viwe vikavu, chakula kikiwa na unyevu hakipaswi kuhifadhiwa kwa zaidi ya siku moja, baada ya hapo chakula huharibika na kinaweza kuleta maradhi kwa kuku.

Uchanganyaji ni lazima uwe mzuri, vinginevyo vitu vyingine muhimu ambavyo ni kidogo havitachanganyika, hivyo kuku wengine watapata ziada ambayo ni vibaya na kuku wengine hawatapata kabisa. Soya ni lazima ikaangwe kabla kusagwa na kutumika kwa

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo