NJIA RAHISI UNAYOWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara. Tunaposema chotara tuna maanisha ni mchanganyingo wa aina mbili za kuku. Mfano mchanganyiko wa kienyeji na kenbro wanajulikana kama kuku wa kenya. Sifa ya kuku chotara ni kama ifuatavyo, 

  1. Wanastahimili sana magonjwa.

2 Wanataga mayai mengi mpaka 240 kwa mwaka kama ukiwalisha vizuri kwa miaka mitano

  1. Wanakua haraka sana. Wanafikisha mpaka kilo 3 kwa muda wa miezi mitatu kama ukiwalisha vizuri

4.Anatumika kama kuku wa nyama na mayai

Ukitaka kufuga kuku kibiashara usimwachie kuku kuhatamia mayai kwani unampotezea muda wa kutaga. Kusanya mayai weka kwenye mashine ya kutotolea vifaranga. Ukitaka kupata faida kubwa usinunue chakula bali tengeneza mwenyewa kwani bei za vyakula zimepanda sana. Kwenye ufugaji asilimia 80 inaenda kwenye ulishaji na asilimia 20 inaenda kwenye madawa.

 

Hatua ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku, banda la kuku linatakiwa liwe linapitisha hewa ya kutosha.

Hatua ya pili,  andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya kocks au aina yoyote ile ambayo inafaawachanganye kuku wa kienyeji na jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kumbuka jogoo mmoja (1)anatakiwa kuwa na matetea kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano.

Hatua ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako, unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.

Kuku wa kienyejiHatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako vitakuwa tayari kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa. Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa. Vifaranga kwa muda wa wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema.

Chanjo na dawa muhimu kwa vifaranga mpaka wakiwa wakubwa

PITIA
MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI WA MIFUGO

Siku 2-6 Pullorum Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin’total au Broiler booster maji

Siku ya 7 Mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota maji

Siku 14 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji

Siku 16-20 Coccidiosis Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin maji

Siku 21 mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota) maji

Siku 28 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji

Wiki ya 6-8 Ndui Fowl pox vaccine sindano kwenye bawa

Wiki ya 13 minyoo Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin maji

Wiki ya 10 hadi ya 15 ukataji midomo Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi maji

KUMBUKA

Dawa ya minyoo na chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo