MAGONJWA MBALIMBALI NA TIBA KWA SUNGURA

SUNGURA ni wanyama wastahimilivu wa mazingira mbalimbali kiasi cha kushindwa kuugua ovyo kama ilivyo kwa wanyama wengine wa kufuga, lakini wanyama hawa ni laini, kiasi ambacho wanaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa yanayochanganya, hata kama watatunzwa vizuri namna gani.

Kama ilivyo kwa hali yoyote ambayo inaweza kuwaathiri sungura wako au mnyama mwingine wa kufugwa, kulitambua tatizo mapema na kulishughulikia haraka kwa kuwatibu linaweza kuleta mabadiliko makubwa kuhusu kuishi kwa sungura wako na kupona kabisa.

Sungura siyo wanyama wanaokula nyama wala si wanyama hatari na mara nyingi wako hatarini kuliwa na wanyama wengine. Kwa sababu ya hali hiyo, sungura pia wanaweza kupatwa na maumivu au ugonjwa, na kuonyesha dalili ambazo zinaweza kuwa ishara kwa wanyama hatari kuwashambulia. Ninazungumzia kuhusu asili yao ya kuishi porini n ahata unapowafuga.

Hii inamaanisha kwamba ni vigumu kwetu kama wafugaji wa sungura kubaini kwa urahisi wakati mambo yanapokwenda mrama, na kujifunza kuhusu baadhi ya dalili za mwanzo za tatizo kunaweza kuwa changamoto ya kujifunza kwa undani.

Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ya msingi yanayowapata sungura ambayo yanaweza kuwa vigumu kuyatambua katika hatua za mwanzo, na jinsi ambavyo unaweza kuyagundua.

No MAGONJWA CHANZO TIBA KIASI
1 Kudhoofu na kukonda Ukosefu wa vitamin mwilini  Amilyte au vitamin 20% otc  Weka kwenye maji yao ya kunywa.
2 Minyoo kuharisha na kukosa kula  Uchafu katika banda, kuwawekea majani chini badala ya kuning’iniza na kutobadilisha chakula kinachobaki  Bimectin  Cc1 ka sungura 1 unamnywesha.
3 Animonia, kufa bila kuugua na magonjwa kwa ujumla Animonia kutokana na baridi au uchafu wa banda  Amprolium changanya na tylodox.  Wachanganyie katika maji na uape kwa siku5
4 Fangas za kwenye pua na sehem zingine  uchafu  Liquid paraffin ya kupaka na ant parasite  Mpake sehem zenye ukurutu na kumchoma sindano ya ant parasiteMwenye mimba usimchome yeye mpake tu.
5 Infections za machoni  Bacteria wa uchafu huhamia jichoni baada ya kulikuna  Belmycin au ointment pia kwa ajili ya kuzuia unaweza kumchoma ant biotic na mtaalamu  Pata maelezo toka kwa mtaalamu au muuzaji.
PITIA
Mambo unayopaswa kufuatilia katika ufugaji wa kuku


UGONJWA WAT UMBO (GASTROINTESTINAL STASIS)
Ugonjwa huu ambao kitaalamu unajulikana kama Gastrointestinal stasis unahusisha tatizo la mfumo wa mmeng’enyo wa sungura wako ambao hujifunga na kushindwa kucheua wala kukisaga chakula. Mmeng’enyo wa chakula wa sungura unapaswa kuwa katika kiwango bora ili kuwawezesha waishi, na hii inamaanisha kuwa na uwezo wa kupata chakula cha kutosha katika kiwango kinachotakiwa.

Siyo tu ni hatari kwa sungura wako ikiwa mfumo wao wa umeng’enyaji chakula umegoma, lakini pia ni vigumu kuuanzisha upya katika hali ya kawaida, hata kwa mtaalamu bingwa wa magonjwa ya mifugo. Kama utaona sungura hali chakula, au hanyi kinyesi cha kutosha kama ilivyo kawaida, hii itakuwa dalili kwamba mfumo wake wa chakula una matatizo.

Kama utahisi kwamba umeng’enyaji wake wa chakula umesimama, jaribu kusikiliza kwenye tumbo la sungura wako kwa dalili za mmeng’enyo; unatakiwa usikie sauti ya mmeng’enyo baada ya dakika kadhaa kama utasikiliza kwa makini. Kama umeng’enyaji umesimama, fanya hima mtafute mtaalamu wa mifugo ili akupe ushauri unaofaa na ikiwezekana unaweza kumfanyia upasuaji halafu akaendelea kuishi.

MATATIZO YA MENO
Sungura wanasumbuliwa sana na meno yao, kwa sababu meno ya sungura huendelea kukua tu hata kama watakuwa wakubwa na hayakomi kama ilivyo kwa binadamu na wanyama wengine. Ni muhimu kuangalia meno ya sungura wako kila wakati kwa kumtumia mtaalamu wa mifugo, na sungura wako anaweza kuwa anahitaji kupunguzwa meno yake kwa kumtumia mtaalamu huyo ili kuyafanya yawe katika urefu unaotakiwa.

Kama sungura wako ataonekana hapendi kula, ana matatizo wakati wa kula, ana uvimbe usoni ambao unaweza kuwa dalili ya matatizo ya meno, au ataonekana anadondosha chakula kingi wakati anakula, mpeleke au mwite ofisa mifugo haraka amwangalie.

PITIA
BANDA BORA LA SUNGURA - Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

 KUSHAMBULIWA NA WADUDU
Sungura wanaweza kusumbuliwa na chawa, kupe na viroboto au hata kunguni kama ilivyo kwa paka na mbwa, na sungura wa kufugwa wanaweza kusambaza kwa urahisi wadudu hao kwenda kwa wenzao na kwa wanyama wengine wa kufugwa.

Hakikisha unamtumia daktari wa wanyama mwenye uzoefu wa ufugaji au mambo ya sungura kutibu viroboto kila wakati, na kwamba sungura wako wanachunguzwa kila wakati hasa kwenye masikio kuona kama wana wadudu, kama wanatoa majimaji kwenye masikio au wanajikuna sana kichwani. Kuwa mwangalifu kuhusu dawa za kuua wadudu hao unazozitumia kwa sungura wako kwa sababu siyo dawa zote unazozitumia kutibu paka na mbwa zinafaa pia kwa sungura.

Mwisho, wakati sungura wako anacheza bustanini au yuko kwenye banda lake la kuchezea, mtazame kwa makini kwenye mwili wake kama ana dalili zozote za kupe, na tumia kifaa maalumu cha kuondolea kupe.

KUKAKAMAA KICHWA
Kukakamaa kichwa ni hali ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali, kuanzia kuwa na maumivu katika sikio la ndani au matatizo makubwa ya ugonjwa kama pasturella au enchephalitozoon cuniculi, ambapo yote ni hatari na yanahitaji matibabu ya haraka. Kama sungura wako ameweka kichwa isivyo kawaida au ameinamisha kichwa upande mmoja, wasiliana na ofisa ugani ama daktari wa mifugo haraka.

MAAMBUZIKI KATIKA MFUMO WA UPUMUAJI
Sungura wanaweza kupata magonjwa haraka kupitia mfumo wa upumuaji, ingawa hawapatwi na mafua. Maambukizi na mizio kwenye njia ya juu ya upumuaji ni matatizo ya kawaida kwa sungura, na daima utayagundua kutokana na kukoroma, mapigo ya moyo na wakati mwingine kutokwa na majimaji kwenye macho na pua.

Kama sungura wako wanasumbuliwa na matatizo ya pumzi, wanapumua haraka au kutoa sauti au wanatoa majimaji hiyo inaashiria ni tatizo, wasiliana na ofisa ugani haraka. Kwa kifupi, haya ndiyo matatizo matano sugu ambayo yanawasumbua sungura, lakini ni matatizo ambayo hayagunduliki haraka wakati yanapoanza.

PITIA
Ufugaji wa kuku aina kuloirel

Wafugaji wote wa sungura wanapaswa kujifunza kwa makini kuhusu maradhi ya msingi na matatizo yanayowakabili sungura, kujua dalili zake na namna ya kukabiliana nayo.

KUMBUKUMBU ZA MRADI
Katika ufugaji wa sungura kibiashara n lazima kwa mfugaji kuweka kumbukumbu zake vizuri juu ya ufugaji wake na kumbukumbu hizo huweza kuhusisha

  • Gharama za kuanzisha mradi yaani ujenzi wa mabanda na ununuzi wa mbegu
  • Kumbukumbu za uzazi wa kila sungura jike
  • Kumbukumbu za utengenezaji wa chakula
  • Kumbukumbu za matumizi yote yahusuyo mradi

Umuhimu wa kutunza kumbukumbu ni ili kuweza kutambua kama biashara hii inaleta faida au hasara.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

MFAHAMU KUKU AINA YA KUCHI

Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »