MAGONJWA MBALIMBALI YA NG’OMBE – Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

MINYOO YA NG’OMBE:  Ugonjwa wa minyoo husababisha hasara kwa mfugaji wa ng’ombe . Utafiti unaonyesha kuwa ng’ombe wengi wanaathirika na minyoo hiyo hupunguza uzalishaji. Aidha utafiti unaonyesha kuwa tatizo la minyoo kwa ng’ombe limeenea hapa nchini kwetu.

 AINA ZA MINYOO: Minyoo inayoathiri ng’ombe imegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo;  Minyoo inayoishia kwenye maini ya ng’ombe (liverflukes).,Minyoo inayoishia kwenye mapafu (lungworms). ,Minyoo mikubwa ya mviringo (large roundworms). , Minyoo midogo ya mviringo (small roundworms).

 MZUNGUKO WA MAAMBUKIZI: Minyoo hupitia njia zifuatazo: ,Mnyama kuambukizwa na mwingine. Kupenya kwenye ngozi ya ng’ombe. ,Ndama kupata minyoo kupitia kwa mama (ng’ombe) alieathirika kwa minyoo wakati wa kuzaliwa., Ng’ombe kula mayai ya minyoo yaliyomo kwenye majani wakati wa malisho. MNdama kupata minyoo wakati wa kunyonya maziwa ya ng’ombe aliyeathirika.

 DALILI ZA NG’OMBE ALIYEAMBUKIZWA.
            – Kupoteza uzito
– Kukosa hamu ya kula
– Kuhara
– Kupungukiwa na damu
– Kuwa na homa
– Afya yake kufifia na hatimaye kufa
– Tumbo kuwa kubwa kupita kiasi (ndama).
TIBA: Wanyama wapewe dawa za kutibu minyoo mara kwa mara. Mfano:  NILZAN ,NILVERM . PIPERAZINE. ANACUR. THIABENDAZOLE. YOMESAN. OXYDOZIDENE

 JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI NA KUZUIA MINYOO ISIENEE.
Minyoo hukingwa kwa njia zifuatazo:  Kuepuka kulisha ng’ombe kwenye majani yenye mayai ya minyoo. Ng’ombe wote wagonjwa watibiwe. Epuka kulisha na kunywesha kwenye mabwawa. Usafi wa banda uzingatiwe. Ng’ombe wasiruhusiwe kukanyaga malisho yao hasa kwenye zero grazing.

MADHARA YA MINYOO
Husababisha upungufu wa damu. Husababisha upungufu wa maziwa. Ng’ombe huweza kufa.

2.  UGONJWA WA MAPELE NGOZI
Mapele ngozi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kama Capripoxvirus. Virusi hivi huweza kukaa kwenye ngozi iliyokauka hadi siku 18. Ugonjwa huu huwapata ng’ombe wa umri wowote, aidha virusi hivi hufa kwa muda mfupi katika kemikali mbalimbali kama ether 20% chloroform, farmalin 1% na phenol 2%

PITIA
Tambua faida ya matumizi ya Choya (rosela) kiafya

JINSI UGONJWA HUU UNAVYOAMBAUKIZWA.
Virusi vya mapele ngozi hupatikana kwenye mapele, mate na majimaji mengine ya mnyama mgonjwa. Ugonjwa huu unaambukizwa kwa kuumwa na mbu jamii ya Andes Culex baada ya kumuuma mnyama mwenye virusi.

DALILI ZA UGONJWA HUU.

Homa kali ambayo inaambatana na kutokea kwa mapele katika ngozi. Mapele haya yanaweza kuwa na ukubwa wa sentimeta 1 hadi 7 na huonekana katika sehemu ya kichwa, shingo, kiwele na miguuni. Mapele haya hukauka, kunyofoka na kuacha vidonda ambavyo huweza kushambuliwa na bakteria.

Mapele haya yanaweza pia kutokea katika mdomo. Dalili nyingine ni homa kali ya nyuzi joto sentigredi 40-41.5, mnyama hukosa hamu ya kula, kutoa machozi, kutokwa na makamasi mazito, kuvimba matezi, kupunguza uzalishaji maziwa na kutupa mimba. Baadae mapele hutokea mwili mzima.

JINSI YA KUZIA UGONJWA HUUU.
Mapele ngozi unazuilika kwa kuchanja ng’ombe na kurudia chanjo mara moja kila mwaka ili kuongeza nguvu ya kinga.

ZINGATIA KANUNI ZIFUATAZO:

1. Ogesha mifugo kwa kutumia dawa ambazo zinaua wadudu ikiwa ni pamoja na mbu wanaoeneza magonjwa ya mifugo.
2. Hamasisha wafugaji wengine kuchanja dhidi ya mapele ngozi na magonjwa mengine ya mifugo kama vile homa ya mapafu, ugonjwa wa miguu na midomo na ndigana kali.
3. Toa taarifa kwa mganga wa mifugo aliyekaribu nawe unapoona dalili za ugonjwa huu ili hatua zinazopaswa zichukuliwe.
4. Tenga wanyama wagonjwa na kuwapatia matibabu ya vidonda.
5. Nunua ng’ombe kutoka eneo ambalo halina ugonjwa.

UDHIBITI WA MAGONJWA YA NG’OMBE
Magonjwa huweza kusababishwa na matunzo hafifu lishe duni na visababishi vya magonjwa kama vile protozoa bacteria.Virusi, riketsia na minyoo.  Aidha wadudu kama kupe na mbung’o wanasambaza visababishi vya magonjwa.

PITIA
Ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili): kanuni bora za ufugaji

AFYA BORA YA NG’OMBE INATOKANA NA KUZINGATIA MAMBO YAFUATAYO:
 Ndama apate maziwa ya awali (dang’a) ya kutosha kwa siku 3 – 4 baada ya kuzaliwa ili kuongeza kinga ya magonjwa mwilini. Chovya kitovu cha ndama ndani ya madini joto (Tincture of Iodine) mara baada ya kuzaliwa kuzuia kuvimba kitovu kutokauka au kutohudumiwa ipasavyo mara baada ya ndama kuzaliwa.  Kitovu huvimba na kutoa usaha hukojoakwa shida na wakati mwingine huvimba viungo.

Ndama apewe dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 kama atakavyoshauri mtaalam wa mifugo.  Minyoo huwashambulia ndama zaidi hasa wale walioana kula majani. Zingatia usafi wa vyombo na band a epuka kumpa ndama maziwa yaliyopoa na machafu ili kuzuia kuharisha.

Zingatia ujenzi wa mabanda kuruhusu mzunguko wa hewa ili kuzuia ndama kupata ugonjwa wa vichomi.  Vichomi huwapata ndama wa umri wa miezi 5 au zaidi wanaofugwa ndani katika mabanda machafu yasiyo na mzunguko wa hewa ya kutosha.

Ogesha ng’ombe kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo ili kuua kupe wote wanaoleta magonjwa yatokana yo na kupe (ndigana kali na baridi, kukojoa damu na maji moyo) na mbung’o (ndorobo) na Ng’ombe wapatiwe chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali chanjo muhimu ni za ugonjwa wa kutupa mimba, kimeta, ugonjwa wa miguu na midomo na chambavu.

Mfugaji anashauriwa kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo anapoona ng’ombe wake ana baadhi ya dalili zifuatazo:-

 • Joto kali la mwili na manyonya kusimama
 • Amepunguza hamu ya kula
 • Amezubaa na kutoa machozi
 • Anasimama kwa shind ana kusinzia
 • Anapumua kwa shida na pua kukauka
 • Anatokwa na kamasi nyingi
 • Anajitenga na kundi
 • Anaconda na
 • Anapunguza utoaji wa maziwa ghafla
PITIA
CHAKULA BORA CHA SUNGURA - Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

KUMBUKUMBU NA TAKWIMU MUHIMU
Kumbukumbu ni taarifa au maelezo sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio muhimu ya kila ng’ombe na shughuli zote zinazohusiana na ufugaji.  Mfugaji anashauriwa kuweka kumbukumbu na takwimu muhimu katika shughuli zake za ufugaji wa ng’ombe.

Kumbukumbu zinamsaidia mfugaji kujua mapato na matumizi na kufanya maamuzi sahihi kuhusu mifugo husika na mifugo husika na mazao yake.  Aidha humwezesha kuweka mipango ya shughuli zake.

Mfugaji anapaswa kuweka kumbukumbu muhimu zifuatazo:-

 • Uzazi (uhimilishaji na matumizi ya dume, tarehe ya kupandwa, kuzaa kuachisha kunyonya)
 • Kinga na tiba
 • Utoaji wa maziwa
 • Ukuaji
 • Idadi ya ng’ombe kwa makundi – majike, ndama, mitamba, madume,maksai

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Karoti

KILIMO CHA KAROTI KILIMO CHA KAROTI : Zao la karoti asili yake ni Asia ya Kati. Zao hili lilienea nchi za Ulaya kwa kupitia Bahari

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »