Mambo unayopaswa kufuatilia katika ufugaji wa kuku

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......
Kuku wa Kienyeji wa Mayai

Ili uweze kuwa mfugaji bora wa kuku basi unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi ambayo nimeyaeleza katika makala haya kama ifutavyo;

Mfumo wa banda
Hili ni jambo muhimu sana unalohitajika kuwa makini  nalo, haijalishi ni idadi gani ya kuku unayofuga, banda linaweza kukutengenezea au kukuharibia mafanikio katika ufugaji.

Ukifanikiwa kufanyia kazi mfumo wako wa banda utakuwa umepunguza zaidi ya asilimia 40% ya matatizo. Nimekutana na wafugaji ambao wana mabanda yasiyoridhisha. Kuku wao wamekuwa wakipata shida.

Hakikisha kuwa wewe unafanya kazi yako ya ufugaji kuwa rahisi. Kumbuka kuwa banda ndicho kitu cha pili chenye gharama nyingi ukiachana na chakula katika ufugaji.

Ulishaji na chakula
Unahitaji kuzungukia kujifunza ufugaji kuku kabla hujaamua kuanza chochote, hii itakusaidia kufanikisha malengo yako, chakula na ulishaji vinachukua sehemu kubwa ya gharama za ufugaji hivyo maandalizi mazuri yatakufanya ufurahie safari yako. Unaweza kuchagua labda uzalishe chakula chako mwenyewe au ununue chakula ambacho tayari kimeandaliwa. Chakula bora kinawafanya kuku wako wakue vizuri na kuwahimarisha kinga yao ya mwili.

Kutengeneza mwenyewe chakula kunaweza kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji kwa asilimia 50%. Wafugaji wapya wasitengeneze chakula wenyewe hadi wahakikishe wamejua vizuri. Kumbuka kutengeneza chakula mwenyewe kutakugharimu kununua mashine za kufanya kazi hizo. Wafugaji wenye kuku kuanzia angalau 500 wanaweza kutengeneza chakula wenyewe kwa sababu hiyo inaweza kukulipa.

Utunzaji kumbukumbu                                                                                                   
Hili ni eneo lingine muhimu sana. Utunzaji kumbukumbu mzuri unaweza kukusaidia kukua haraka,inakusaidia kuona ulipofanikiwa na kushindwa, wapi urekebishe, weka kumbukumbu ili uweze kuongeza uzalishaji.

PITIA
Dondoo za Ufugaji wa Kuku bora wa Nyama

Baadhi ya wafugaji hawajui idadi ya kuku walionao, wangapi wamekufa..

Mabadiliko na tofauti                                                                                                   
Unahitaji kugundua tofauti katika kuku wako, hii ikihusisha ukuaji, ulishaji, kupunguza utagaji, idadi, na sauti zao.

Hii itakusaidia wewe kama mfugaji kujua mabadiliko yao. Kwa mfano: Kuku wa mayai wanapoanza kutaga hupiga kelele, ulishaji na uzito huongezeka, na muda mwingine ikiwa kuna mlipuko wa ugonjwa utagundua haraka kwa kupunguza utagaji wao, kama siyo kawaida kama siku zote basi kuna tatizo, unaweza muita mtaalamu aliye karibu nawe. Gundua mapema mabadiliko ya kuku wako.

Aina ya kuku                                                                                                                     

 Hili nalo ni jambo la muhimu unalopaswa kuzingatia wakati unafikiria ufugaji kibiashara. Ni kuku wa mayai au nyama? Unahitaji kuchagua kuku bora, ukizingatia na kizazi cha kuku hao.

Wapi unatilia mkazo
Tunapozungumzia ufugaji kibiashara ni muhimu uwe na eneo ulilowekea mkazo. Je unataka kufuga kwajili ya kuzalisha mayai au ni nyama, au kuangulisha vifaranga, ni kwajili ya chakula kwa kuchinja na kupaki?

PITIA
NJIA RAHISI UNAYOWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA

Mtaji                                                                                                                                   

Mtaji ni moja wapo ya vitu muhimu vitakavyoamua nini kifanyike. Mtaji ni kiasi cha fedha ulizowekeza katika biashara, sababu kuu kwa nini kuku wanahitaji pesa ni kuwa wanahitaji huduma nzuri ili wakuzalishie vizuri.

Vifaa vya kuku
Ni vizuri kuandaa vifaa vyote kabla ya kuanza mradi ili usije kukwama. Vifaa vinavyohitajika ni:
Vyombo vya chakula
Vyombo vya maji
Trei za mayai
Chanzo cha joto(vyungu tunavyo tuwasiliane)
Sehemu ya kuweka taka
Chakula
Dawa
Eneo la kuhifadhi kuku wagonjwa.

Eneo la kufugia kuku
Inatakiwa eneo ambalo lipo mbali na makazi ya watu ili kuepusha bughudha ya harufu, kuhifadhi uchafu iwe rahisi, unaweza kufuga kuku hata nyumbani kwako lakini unapofikiria kufanya mradi mkubwa wa maelfu ya kuku, jaribu kuweka mbali na makazi ya watu.

Ikiwa mambo haya yatazingatiwa, wafugaji wa Tanzania na Afrika wataona mafanikio ya wanachofanya. Hatuhitaji tena kuudharau ufugaji, bali tuuchukulie kwa umakini kama kazi nyingine

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo

Translate »