KILIMO BORA CHA MAPAPAI

KILIMO CHA MIPAPAI

•Kwa jina la kisanyansi ni Carica papaya,jina la kawaida ni papai.

•Tunda la mpapai lina virutubisho vya vitamin A,B na C kwa wingi,na ni tunda tamu sana.

•Jani la mpapai hutumika kama dawa kutibu magonjwa ya kuku kuhara damu.

•Tunda hili husaidia sana kwa mmeng`enyo wa chakula tumboni.

•Ni chanzo kizuli sana cha kipato pale utakapo amua kujikita kwa kuzalisha kitaalamu na kwa tija.

•Mmea wa mpapai ipo ya kiume na ya kike, vilevile na baadhi ya mimea ya mipapai yana homoni zote za kike na kiume.

•Hivyo basi kwa kuzingatia jinsia za mmea wa mpapai hakikisha mipapai dume haizidi asilimia 20 ya mipapai jike,Dume libaki moja kwa kila majike 25.

MAHITAJI

•Hali ya hewa inayo itajika kwa uzalishaji bora wa mipapai ni ile ya kitropiki yani isiwe baridi kali wala joto kali.

•Udongo uwe wa kupitisha maji na sio wa kutuamisha maji kwani udongo unao tuamisha maji hupelekea miche ya mipapai kufa hasa pale inapo kuwa midogo hata mikubwa kwani mpapai hauna mzizi mkuu.

•Udongo uwe wenye rutuba ya kutosha ili uwezeshe mizizi kuchukua rutuba kwa urahisi kwani mti wa mpapai hauna mzizi mkuu.

•Mvua zinazo hitajika kwa mwaka ni milimita 1500 hadi milimita 20000.

•Umbali kutoka usawa wa bahari ni mita 1000.

•hustwi zaidi kwenye mazingira yaliyo wazi na sio kivuli,pia zuia sana upepo mkali.

JINSI YA KUOTESHA MBEGU

Kuna aina mbili za mbegu red royal F1-Uvumilia sana magonjwa na ukomaa kwa muda wa miezi 6 hadi 7 pia huvunwa kwa muda wa miaka 5 mfululizo.

UANDAAJI WA MBEGU

PITIA
Kilimo Bora cha maharage

-Hakikisha mbegu zinatoka kwenye tunda lililokomaaa na kuiva vizuri.

-Kisha osha kwa maji hizo mbegu na kuzianika kwenye kivuli mpaka zitakapo kauka.

Kuna namna mbili za huoteshaji wa mbegu za papai.

-Kuotesha kwa moja kwa moja shambani,na

-Kuotesha kwenye kitalu na kisha kuamishia shambani.

KWA KUOTESHA MOJA KWA MOJA SHAMBANI

-Andaa mashimo yenye urefu wa sentimeta 60 kwenda chini kwa kuweka samadi ili kuhakikisha udongo kuwa na rutuba na mashimo haya yaandaliwe kabla ya wiki mbili pia waweza tumia mbolea ya NPK kwa kupandia panda mbegu 3-5 kwa kila shimo kwani mbegu zingine zinaweza zisiote kutokana na sababu mbali mbali kama wadudu baada ya kuota achia mche mmoja wenye afya na nguvu za kutosha kuimili halitofauti tofauti za hewa.

-Mashimo hayo yachanganywe na samadi debe moja kwa nusu ya udongo uliochimba kutoa kwenye shimo.

-Kisha mwagilia shimo hilo kwa muda wa wiki mbili na kisha pandikiza mche kwa urefu wa futi 1 mpaka 2 kwenda chini ya ardhi.

-Panda kwa nafasi ya mita 2 kwa 3 au 3 kwa 3 kutoka mmea hadi mmea.

KWA KUOTESHA KWENYE KITALU

Joto linalo itajika ni sentrigrade 21 mpaka 27 kwa uotaji ulio sahihi.

Hatua zifuatazo zifauatwe

•Andaa udongo wako wenye rutuba ya kutosha unaweza weka udongo kwenye mifuko ya plastiki(viriba) na kupanda mbegu 3 mpaka 5 kwasabu ya kuepuka mbegu zingine kuwa dume au kufa kabisa,pia puliza sumu ya COPPER OXYCHLORIDE kwa gramu moja kwa lita moja ya maji ili kuzuia fangasi au ukungu.

•Amisha miche ya mipapai kwa kupandikizwa kwenye shamba ulilo andaa baada ya mche kuwa na majani kuanzia mawili mpaka matatu na mche kuwa na urefu wa sentimeta 30.

PITIA
KILIMO BORA CHA KAROTI(CARROT)

•Panda kwa nafasi mita 2 mpaka mita 3, yani mita 2 mstari hadi mstari na mita 3 shimo hadi shimo.Urefu wa shimo uwe sentimeta 60 panda mche sentimeta 1 mpaka 2 ili kuufanya mche upate joto la wastani ili usikauke.

Kwa muda wa miezi 7 mpaka 8 matunda uanza kutengenezwa.

Kwa muda wa miaka 3 hadi 5 pumzisha shamba lako kwa kupanda zaotofauti na mpapai ili kuepukana na wadudu na magonjwa kuzaliana kwa wingi.

Uhai wa mti wa mpapa ni miaka 3 mpaka 5,Mazao yake kwa mwaka ni tani 35 hadi 40 kwa heka.

*KUMBUKA

—Panda miti kuzunguka shamba la mipapai kuepuka upepo mkali na miti hiyo yaweza kuwa ya milusina,mijohoro,miembe na miti hii yapaswa kuwa mirefu zaidi ya mimea ya mipapai kwa urefu wa mita 10 juu zaidi , hila haishauriwi sana kupanda mipapai sehemu zenye upepo mkali upelekea miti kuanguka kwani shina la mpapai ni rahisi sana kuvunjika.*

UDHIBITI WA MAGUGU

Udhibiti wa magugu shambani ufanyike mara kwa mara na ondoa majani kuzunguka mmea wa mpapai kwa umbali wa mita moja kutoka kwenye mti wa mpapai.

Pia kwa udhibiti mwingine wa magugu ni kwa kutandaza matandazo yaweza kuwa ni nyasi kavu kuzunguka mti wa mpapai na kama itawezekana tandaza shamba zima ili kuepuka kabisa uotaji wa magugu.

Pia kwa kutuma sumu kwa ajili ya kuua magugu.

Ondoa magugu kabla hayaja komaa.

Usifukue sana chini kwa majani yaliyo karibu na mti kwani mizizi ya mpapai sio mirefu sana.

UMWAGILIAJI

Umwagiliaji waweza fanyika hasa kwa kile kipindi cha kutoa maua ambapo hapa mmea unaitaji maji kwa wingi pia usiruhusu mimea ya mipapai kukosa maji baada ya wiki nane(8) kama mvua hakuna hakikisha maji yana patikana hasa kwa kufanya umwagiliaji.

PITIA
Somo la kilimo bora cha nyanya: Mbegu, kitalu, shamba, matuta na kupanda miche

Kwani maji yakikosekana kwa mpapia madhara yafuatayo yatajitokeza

-Maua yataanguka kutoka kwenye mmea.

-Mmea utadumaa

-Maua hayatatengeneza matunda.


UANGALIZI 

-Fanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye shamba la mipapai kuhakikisha hakuna wadudu wala magojwa kama ya fangasi na virusi.

-Ondoa machipukizi pembeni ya mti wa mpapai ili kuwezesha ukuaji wa mti kuwa wa haraka na matunda kuwa makubwa kwani matawi yakiwa mengi hupelekea chakula kinachotengenezwa kuishia kwenye matawi na matunda kuwa madogo.

-Pia kwa kuweka miti pembeni ya mpapai kuupa sapoti hasa pale mti unapotoa matunda mengi usipelekee upepo kuangusha mti wa mpapai.

-Ondoa matunda yote na majani yote yaliyo shambuliwa na magonjwa pamoja na wadudu kuzuia kusambaa kwa miti mingine.

WADUDU WANAO SHAMBULIA MMEA WA MPAPAI

WADUDU 

•Wadudu wanao shambulia sana matunda nao ni mites na fruit fly kwani hushambulia matunda na uyaozesha kuzuia wadudu hawa tumia sumu kuangamiza madudu hawa pia waweza fanya usafi wa shamba mara kwa mara,kuondoa matunda yaliyo anguka na kuoza pamoja na majani yaliyoanguka chini.

•MAGONJWA

-Virusi vya mosaiki

Virusi hawa husambazwa na funza mafuta na hushambulia mti(shina)

Jinsi ya kuzuia

Ondoa jani lililoshambuliwa

Zuia funza mafuta

-Athrankinosi

Hutokea kwenye matunda na huozesha matunda kwa namna ya kama shimo kwenye tunda

Jinsi ya kuwazuia

Tumia sumu za kuangamiza fangasi

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »