MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI WA MIFUGO

MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI WA MIFUGO : Maendeleo ya Sayansi na teknolojia yamewezesha sekta za utengenezaji madawa (Phamaceutical Industries) kutengeneza madawa ya aina nyingi hususani yale ya kuua na kudhibiti viumbe hai tegemezi wa mifugo na binaadamu. Kwa hivi sasa madawa ya aina hiyo yamo katika makundi makuu matatu ambayo ni ya kuangamiza minyoo, protozoa na yale ya kuangamiza wadudu watambaao na kuruka (insecticides).

MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI
MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI

DAWA YA UHAKIKA LAZIMA IWE NA SIFA ZIFUATAZO:

• Usalama kwa mifugo na watumiaji

• Kufanya kazi kwa matokeo mazuri

• Wigo mpana wa kuangamiza au kudhibiti wadudu na vijidudu hai tegemezi

• Uwezo wa kutokomea mwilini mwa mifugo kwa haraka

• Uwezo wa kudhibiti usugu wa walengwa

Matumizi ya madawa licha ya kudhibiti vijidudu au wadudu tegemezi kwenye mifugo pia yawe na usalama mkubwa kwa walaji.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA UTUMIAJI WA MADAWA HAYO NI KAMA YAFUATAYO:

• Kuchagua dawa inayofaa, kujua tabia/ maisha ya vijidudu au wadudu hai tegemezi, kujua maisha tabia/maisha ya mnyama husika

• Kujua ubora/wingi toshelezi (dose) wa dawa husika, njia sahihi ya kutumia na uhusiano (compatibility) na mnyama
husika.

• Jinsi ya kufanya maandalizi; yaani utumiaji wa dawa hizi wakati muafaka, umakini katika utumiaji (rational use); kuangalia hali halisi ya mahali husika, kujifunza matokeo mabaya mwilini mwa mnyama na kuepuka kuzuka kwa walengwa sugu.

MAKUNDI YA MADAWA KATIKA VIUMBE HAI TEGEMEZI (ANTIPARASITIC DRUGS)

 1. MADAWA YA KUDHIBITI MINYOO (ANTIHELMINITIC AU VERMIFUGE)

Haya ni yale ya kudhibiti aina mbalimbali za minyoo kama vile, minyoo mviringo (Roundworms), minyoo ya aina ya tegu (Tapeworms Cestodes), minyoo bapa (Flatworms, Trematodes).

Hii ni moja ya mashambulizi ya minyoo kwenye sehemu ya utumbo wa kondoo

1.1 Madawa ya kudhibiti minyoo mviringo (antinematodes) ni kama vile albendazole (Trichloforn), Levamisole, Ivermectin, Pyrantal, na Piperazine (Carbon disulfide).

1.2 Kudhibiti minyoo ya aina ya tegu kama vile, Arecoline, Copper Sulphate na Niclosamide.

1.3 Kudhibiti minyoo bapa kwa mfano; Carbon tetrachloride (Albendazole), Lorothedol Bithun, Niclofahan na Closantel.

1.4 Kudhibiti minyoo ya kibofu (Schistosomes). Kama Antimony Potassium titrate, Praziquantel, Nithiocyanate nakadhalika

2.0 KUDHIBITI PROTOZOA: KAMA ANTICOCCIDIAL, ANTITRYPANOSOME, NA ANTIPIROPLASMA

2.1 Anticoccidial kama vile Monensin, Sulphaquarxaline Diclazuril na Salinomycin

2.2 Antitrypanosomal kama vile Diminazine nakadhalika.

2.3 Antipiroplasm kwa mfano Trypan blue nakadhalika

3.0 KUDHIBITI WADUDU WARUKAO NA WATAMBAAO (INSECTICIDES)

• Kudhibiti wadudu tegemezi waishio nje ya miili ya mifugo kama vile utitiri, mange mites, kupe (ticks), viroboto (fleas), mbu, inzi, funza wa inzi (maggots) na vinginevyo

PITIA
CHAKULA BORA CHA SUNGURA - Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

• Viuadudu vya kudhibiti wadudu hawa vimegawanyika katika makundi ya Organophosphates, Organochlorides na
Parathroids kwa mfano, Paranex, Drop- On, Ecotix, Amitraz (Tiktik), cyromazine nakadhalika.

SIFA SAHIHI NA ZA UHAKIKA ZA MADAWA YA KUUA WADUDU TEGEMEZI

1.USALAMA: Dawa hizi ni sumu. Dawa iwe na uwezo mkubwa wa kudhibiti wadudu lakini isilete madhara kwa mnyama husika. Usalama huu hupimwa kitaalamu kwa kutumia kipimo kijulikanacho kama Therapeutic index = LD 50/ ED 50, kiwango cha usalama Th. I ikiwa kubwa basi dawa hiyo ina usalama mkubwa ikitumika kwa mnyama. Dawa yeyote inakuwa na usalama kama Th. I yake ni zaidi ya 3 kwa mfano; Tricholoform, Piperazine, Mebendazole, Zoalene, Amprolium, Robenidine, Nuclofelen, Prazequantel zina usalama mkubwa lakini dawa kama Diminazene, Copper sulphate zina usalama mdogo.

2. KUFANYA KAZI VIZURI: Dawa inayofanya kazi vizuri ina uwezo wa kuua au kuzuia uharibifu wa wadudu katika hatua zote wanazopitia katika maisha yao kwa mfano hatua za mayai, funza (larva) na mdudu kamili.

• Dawa yenye kufanya kazi vizuri ina roughly calc. deworming rate zaidi ya 70% na mifano ya dawa hizo ni kama Praziquantel, Levamisole na Thiabendazole.

3. WIGO MPANA WA KUDHIBITI WADUDU (BROAD SPECTRUM ACTIVITY) : Mara nyingi wadudu wa aina nyingi hushambulia mifugo kwa wakati mmoja (Polyinfections). Kama minyoo ya aina nyingi hushambulia mnyama kwa pamoja. Hali ikiwa hivyo inakuwa jambo la busara kutumia dawa zenye uwezo wa kudhibiti aina zote za minyoo.

Dawa zenye uwezo huo ni kama praziquantel, bithionol na mebendazole. Dawa za aina nyingine zina uwezo wa kudhibiti aina moja tu ya minyoo kwa mfano oxantel ambayo ina nguvu ya aina ya pekee ya kudhibiti minyoo ya Trinella spp. Dawa kama hizi zitumike ipasavyo.

4. UWEZO WA KUTOWEKA HARAKA MWILINI MWA MNYAMA :

• Dawa za aina fulani hukaa mwilini mwa mnyama kwa muda mrefu kuliko itakiwavyo.

• Dawa za aina hii huleta madhara kwa mnyama husika na pia kwa binaadamu watakaotumia mazao ya mnyama huyo kama vile nyama, mayai na maziwa.

• Mamlaka ya madawa (Drug Authority) hutoa maelekezo (regulations) kuhusu matumizi ya madawa hayo. Kwa mfano, bidhaa kama za maziwa na nyama visitumiwe na binaadamu kwa siku 30 baada ya kutumia dawa ya tiabendazole.

5. DAWA ZISISABABISHE HALI YA USUGU KWA MNYAMA HUSIKA :

PITIA
DUME ZURI KWA UZALISHAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA

• Usugu wa wadudu kwa dawa ni tatizo katika mpango mzima wa kudhibiti minyoo.

• Madawa mengi yana tabia ya kukaribisha usugu, kama Naphthalene, Zoalene, Aprinocid na Phenyl sulfonyurea

• Njia ya kuondoa tabia hiyo ni:

– Kutumia dawa ya aina nyingine kwenye kundi hilohilo, kama kutumia dawa ya Nicarbazin badala ya Coccidian ambayo inasababisha usugu.

– Kutumia njia ya mzubaisho (Shuttle programme) kwa kutumia dawa za aina mbili zenye uwezo wa kudhibiti ugonjwa wa aina hiyo kwa vipindi tofauti vya uzalishaji (Production cycle) kama anticoccidal drugs.

– Kutumia dawa za aina mbili au zaidi kwa pamoja( Drug combination) kama

Zoalene na robenidine > Coccidian

Sulfaquinoxalene na amprolium > Coccidian

Piperazine na carbon bisulfide na dipterex, Thiophenyl na piperazidine na levamisole :-

Mchanganyiko wa aina hiyo hudhibiti minyoo mviringo (nematodes wa aina nyingi.)

NAMNA YA KUTUMIA KIUHAKIKA MADAWA YA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI.

 1. KUCHAGUA DAWA KWA UMAKINI – Mchunguze mnyama husika (hali, umri n.k)

– Tumia maagizo kuhusu uwezo wa dawa kufanya kazi, uwezo wa kutoleta madhara kwa mnyama, uwezo wa kudhibiti vijidudu/wadudu, wa aina nyingi, urahisi wa kutumia, bei nafuu

– Chagua dawa inayoweza kudhibiti vijidudu vingi kwa kuitumia mara moja tu halafu baada ya muda kupita tumia dawa kidogo ili kutokomeza vijidudu/wadudu wote.

 1. KUELEWA TABIA ZA VIUMBE HAI TEGEMEZI

• Aina zao na uwezo wao wa kuhimili makali ya dawa (sensitivity) kwa mfano:

(a) Huweza kudhibiti kiurahisi minyoo mviringo ya ng’ombe, mbuzi na kondoo hasa minyoo ya mapafu (lungworms) na Trichuris, trichura.

(b) Haina uwezo mkubwa wa kudhibiti minyoo aina ya tegu (tapeworms) na bapa (flatworms).

-Makali ya dawa yana uwezo tofauti katika hatua mbalimbali za maisha ya vijidudu toka kwenye yai mpaka ukubwani (Adult stage). Ni jambo la busara kutumia dawa inayoweza kudhibiti vijidudu au wadudu katika hatua zao mbalimbali za maisha.

 1. KUZIELEWA TABIA NA MAUMBILE YA MNYAMA HUSIKA

• Wanyama wapo wa aina tofauti (Species) na tofauti hizi huwafanya watofautiane kustahimili makali ya dawa kwa mfano kuku, ng’ombe hudhurika na dawa ya aina ya dipterea

Farasi > Thiabendazole na bithulorothedol
Ngamia > Thiabendezole

• Wanyama wa aina moja pia hutofautiana (umri, jinsia n.k) mathalani benzoylenazole haitumiki kwa madume ya kuzalisha ubora wa mbegu.

 1. ZINGATIA UBORA WA DAWA, MADHARA, KIPIMO CHA DAWA NA NJIA YA KUTUMIA

 Ubora – Uwezo wa kudhibiti vijidudu, usalama wa mnyama mfano usafi wa dawa husika, kama zimekwisha muda wake wa matumizi au kupungua ubora nakadhalika

PITIA
UFUGAJI WENYE TIJA: ANZA KUFUGA KUKU WATANO UPATE KUKU 200 NDANI YA MIEZI SITA

• Kipimo kilichoelekezwa – Hii ina maana iwapo utazidisha kipimo inakuwa ni sumu kwa mnyama na ikipunguzwa kipimo basi kuna hatari ya kushindwa kufanya kazi ipasavyo na kukaribisha usugu kwa vijidudu/wadudu

• Njia ya kuitumia dawa mfano kwa kumeza au kunywa ni kwa kuchanganya na chakula (uniform mixture) au kuchanganywa katika maji ya kunywa (fully dissolved).

• Utumiaji wa dawa nje ya mwili wa mnyama: Kunyunyizia mara kwa mara wanyama, kuwadunga sindano kwa mfano Carbon tetrachloride na praziquantel.

• Kutumia dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja: Kwa mfano,

UTUMIAJI WA DAWA ZAIDI YA MOJA KWA WAKATI MMOJA
UTUMIAJI WA DAWA ZAIDI YA MOJA KWA WAKATI MMOJA

• Mchanganyiko wa dawa usiokubalika ni kama vile:

– Amprolium + Vitamini B1 : Sio mzuri kudhibiti wadudu au

– Mec loc i l l ine + Bromosali c y lanide : Mchanganyiko huu waweza kusababisha uharibifu wa mimba kwa ng’ombe au vifo kwa wanyama kama kondoo.

• Tiba ya ziada ni bora kwa matokeo mazuri, kwa mfano:

– Ifanywe kabla ya kulisha mifugo au uache kulisha mifugo yake masaa 12 kabla ya kutoa aina hii ya tiba.

 1. MATAYARISHO:

• Dawa ; vyombo na vifaa vitakavyotumika

• Usafi wa nyumba

• Fanya jaribio kwa wanyama wachache na uchunguze matokeo yake

• Antidotes: Dawa za kupunguza nguvu ya dawa

• Malezi bora

• Kutenga wanyama dhaifu au wagonjwa.

• Kuchunguza wadudu kwenye kinyesi cha mnyama

• Usafi wa vyombo wa mara kwa mara

 1. TUMIA DAWA KATIKA MUDA MUAFAKA, MATHALANI,

• Wanyama wadogo; wenye mimba

• Wenye mimba wiki mbili kabla ya kuzaa

• Wengine ni mara mbili kwa mwaka.

 1. TUMIA DAWA KWA KUZINGATIA MAZINGIRA YALIYOPO (LOCAL CONDITIONS).

• Magonjwa husika yaliyopo (Epidemiology)

• Madawa yaliyopo: Aina na jinsi ya kuyatumia: vipimo na marudio ya njia ili kutathmini athari zitokeazo

 1. JIFUNZE MATOKEO MABAYA YA MATUMIZI

– Kipimo kidogo au zaidi muda mrefu, matumizi mabaya ya dawa, kutozingatia njia zinazoshauriwa n.k

– Fanya jaribio dogo la matumizi ya dawa ili kutathmini matokeo.

 1. USIRUHUSU KUTOKEA KWA USUGU KWA DAWA

– Badilisha dawa mara kwa mara

 1. LINDA AFYA ZA BINAADAMU

• Mabaki ya dawa mwilini mwa mnyama

• Nyama, maziwa, mayai yatokanayo na wanyama hao huleta madhara kwa binaadamu.

• Nchi nyingi zimeweka viwangi vya mabaki ya madawa vinavyoruhusiwa (Residue limit). Viwango hivyo vikizidi mazao ya wanyama husika hayaruhusiwi kuuzwa na kuliwa na binaadamu.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

kilimo cha korosho.-Lindi

Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi anawaalika watanzania wote wenye nia ya kulima korosho kuja katika halmashauri yake na kuunga mkono jitihada hizo. Mpaka sasa Halmashauri

Read More »

Kilimo cha Kabichi

Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho

Read More »

ZIFAHAMU AINA NNE ZA MTAMA

Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya

Read More »

MFAHAMU KUKU AINA YA KUCHI

Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »